Je, ni nani aliyeharibu CHADEMA kati ya Mbowe aliyepeleka wanachama Bungeni na Lissu aliyeondoa wanachama Bungeni?
HIi ni hoja nzito sana na sii ya kuchukuliwa kirahisi
Ili Chama cha Siasa kikue lazima kiwe na idadi kubwa ya Wanachama wenye wadhifa mkubwa katika nchi
Mbowe alizalisha viongozi wengi na wakubwa sana akiwemo Lissu anayejivunia leo kuwa kiongozi wa CHADEMA
Lissu baada ya kukabidhiwa wadhifa wa kiongozi mkuu wa CHADEMA hali ilibadilika sana
Kwanza aliwaeleza Wanachama wake kuwa wale wote wanaotaka kuwa Wabunge wasahau hilo
Kauli hiyo haikuishia hapo pasipo matendo, badala yake alitenda na kuhakikisha hakuna Mwanachama aliyepata nafasi ya Ubunge
Lengo la hoja hii nikutaka CHADEMA ijisahihishe makosa yake na sio kudhihaki
Nalazimika kutumia lugha kali kwasababu hata CHADEMA ni wakali vilevile
Namna nzuri ya kuzungumza nao ni ile ya kukabana koo na kuchaniana mashati