Je ni sahihi kufanya mapenzi na mwenza kama majaribio kabla ya kuoana na kufunga ndoa?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Katika mahusiano kumekuwa na tabia ya kufanya mapenzi kama majaribio kabla ya kuoana na kufunga ndoa na hii inahusisha jinsia zote mbili.

Mwanaume wakati mwingine anajaribu kujiridhisha kama mwanamke anaendana na vigezo vyake hali kadhalika kwa wanawake pia.
Vijana wengi wamekuwa wakitumia kauli za dhihaka kama (Usiniuzie mbuzi kwenye gunia)

Mara nyingi majaribio kama haya yamekuwa yakifanyika na wakati mwingine ndoa nyingi zimekuwa zikifungwa huku wanandoa walishapata watoto hapo awali.

Wakati mwingine ndoa inawekewa vikwazo kwasababu za kujificha lakini ukweli ni kuwa wanandoa walishashindwana kwenye majaribio.

Je wewe una maoni gani kuhusu tabia ya kufanya mapenzi kama majaribio kabla ya kuoana na kufunga ndoa?

 
Ni uzinzi tu umewajaa vijana! Watu wangekuwa hawafanyi mapenzi kabla ya ndoa dunia wala isingefika hapa na hata mapenzi ya jinsia moja yasingeenea kwa kiasi hiki!

Maana ushoga kwa asilimia kubwa hufanyika kwenye mazingira ya uzinzi! Haiwezekani wanaume wawili mabikira wafunge ndoa eti wakashikishane ukuta hiyo experience wamepata wapi?
 
Umeeleza vema kabisa, uzinzi/uasherati umeshamiri na ndio chanzo cha mengine yote!

Watu tungeingia ndoani sealed ingekuwa poa sana.
 
Tabia mbaya sana hii. Ningeweza rudisha muda nyuma ningehakikisha sigegedi papuchi mpaka pale ninapata mke
 
Kinachoskitsha zaid imekuwa kama n destur au utamaduni, na pia imeondoa uaminifu baina ya wanandoa maana unayemtest ukamuacha atakuja mwngne atamst na kumuoa n rahs sana mwanaume huyu kuamini kuwa mkewe anatoka nje na maex wake hata kama s kweli.

N vle tu hawajawah kujua athar za kukutana kimwli kabla ya ndoa, wadada wameanza kutumika tangu wakiwa na miaka 14 huko vjana nao ndo usiseme wamekubuhu. Hii n mbaya na inamadhara.....​
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie napita tyuuh.
 
Yaani kabisa nioe mtu aje awe sio ninaetaka, utawezaje kuvumilia kitu cha namna for the rest of life?
Nasema hiyo ni sahihi.

For the rest of life!!?..... utafikiri tunafikaga nao huko the rest of life. Miezi, Mwaka tunajikutaga tuko na wanawake wa the rest of life wa wengine..
Hiyo sentensi tusiwe tunaiweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…