Je, ni sahihi kusimamisha magari barabarani ili kusubiri kiongozi kupita?

Joined
Sep 3, 2022
Posts
40
Reaction score
90
Je, ni sahihi kusimamisha magari barabarani ili kusubiri kiongozi kupita hii leo niko eneo la songwe airport ili kusubiri waziri mkuu apite hii imekaaje wana Jamiiforums.

Tunekaa almost 2 hrs kusubir na bado hajapita, huu ni kujifanya Mungu mtu na yeye pia jambo hili analifurahia; huu ni utumwa wa kifikra.
 
Hizo ni norms and culture zetu
Huwezi hama nchi

Hizi ni baadhi ya tabia za kipuuzi sana, hakuna mtu anakula nyumbani kwa kiongozi hadi azuiwe zaidi ya masaa mawili barabarani, kisa kiongozi aliyeko madarakani kwa wizi wa kura anapita. Katika mambo yanayopaswa kupigiwa kelele ya nguvu, na kuwekwa wazi kwa wananchi ni pamoja na hili.

Tabia hizi ikishika kasi sana chini ya utawala wa Magufuli, eti hata msemaji wa CCM watu walikuwa wanakalishwa pembeni ili apite. Bila machafuko huu upuuzi hautakaa uishe.
 
Je ni sahihi kusimamisha magari barabarani ili kusubiri kiongozi kupita hii leo niko eneo la songwe airport ili kusubiri waziri mkuu apite hii imekaaje wana jamiiforums

...... tunekaa almost 2 hrs kusubir nabado hajapita huu ni kujifanya mungu mtu na yeye pia jambo hili analifurahia huu ni utumwa wa kifikra
Ni upuuzi wa hizi nchi zetu, na hasa zaidi jeshi la polisi.

Hata kama ni kumpisha, haiwezi kuwa masaa mawili! Tatizo upeo wa polisi ni mdogo sana, hawathamini muda, wala hawana hata ile sense ya time cost, hawafikirii wala kujua ni gharama kiasi gani kwasimamusha watu zaidi ya masaa mawili bila kufanya kazi.

Kuna wakati iliwahi kutokea Waziri Mkuu anatoka Shinyanga, tayari Mwanza maeneo ya Usagara, Buhongwa,Nyegezi mpaka mjini, magari yakaanza kusimamishwa. Waziri Mkuu alipofika Misungwi akasimama kuhutubia. Mpaka kufika Mwanza ilichukua masaa 4, watu bado wamesimamishwa barabarani. Na polisi kwa akili zao ndogo wanaona ni kawaida, na wamefanya kazi vizuri.

Nchi hii maendeleo yatabakia habari za kusikia, kwa sababu watu hawajui hata ni kitu gani kinasababisha maendeleo. Kama huwezi kujua thamani ya muda, wewe sahau habari ya maendeleo.
 
Tatizo tuna viongozi wenye upeo mdogo na wasuojitambua. Hata huyo Waziri Mkuu anashundwa kukemea upuuzi jama huo.

Hivu ni nini cha pekee alivhowapelekea hao watu mpaka watu wote wasifanye kazi kwa sababu ya ujio wake?
 
Hizi ni baadhi ya tabia za kipuuzi sana, hakuna mtu anakula nyumbani kwa kiongozi hadi azuiwe zaidi ya masaa mawili barabarani, kisa kiongozi aliyeko madarakani kwa wizi wa kura anapita. Katika mambo yanayopaswa kupigiwa kelele ya nguvu, na kuwekwa wazi kwa wananchi ni pamoja na hili.

Tabia hizi ikishika kasi sana chini ya utawala wa Magufuli, eti hata msemaji wa CCM watu walikuwa wanakalishwa pembeni ili apite. Bila machafuko huu upuuzi hautakaa uishe.

subiri mkichukua nchi mtakuwa mnapanga foreni na wapiga kura,kwa sasa hamuwezi hata kupanda nao dala dala ila mna magari binafsi yenye AC.
 
Ni upuuzi wa hizi nchi zetu, na hasa zaidi jeshi la polisi.

Hata kama ni kumpisha, haiwezi kuwa masaa mawili! Tatizo upeo wa polisi ni mdogo sana, hawathamini muda, wala hawana hata ile sense ya time cost, hawafikirii wala kujua ni gharama kiasi gani kwasimamusha watu zaidi ya masaa mawili bila kufanya kazi.

Kuna wakati iliwahi kutokea Waziri Mkuu anatoka Shinyanga, tayari Mwanza maeneo ya Usagara, Buhongwa,Nyegezi mpaka mjini, magari yakaanza kusimamishwa. Waziri Mkuu alipofika Misungwi akasimama kuhutubia. Mpaka kufika Mwanza ilichukua masaa 4, watu bado wamesimamishwa barabarani. Na polisi kwa akili zao ndogo wanaona ni kawaida, na wamefanya kazi vizuri.

Nchi hii maendeleo yatabakia habari za kusikia, kwa sababu watu hawajui hata ni kitu gani kinasababisha maendeleo. Kama huwezi kujua thamani ya muda, wewe sahau habari ya maendeleo.

wewe ukiona wanakuchomesha mahindi tanua uwahi,polisi wengi hawajui sheria na hawajasoma wala akili hawana.

unakaaje barabarani masaa 4 wakati kuna sehemu muhimu unawahi kufanya mambo ya maana??
 
Je, ni sahihi kusimamisha magari barabarani ili kusubiri kiongozi kupita hii leo niko eneo la songwe airport ili kusubiri waziri mkuu apite hii imekaaje wana Jamiiforums.

...... tunekaa almost 2 hrs kusubir nabado hajapita huu ni kujifanya mungu mtu na yeye pia jambo hili analifurahia huu ni utumwa wa kifikra.
Kiongozi wa nchi ni lazima aheshimiwe,Subira yavuta heri.
 
Je, ni sahihi kusimamisha magari barabarani ili kusubiri kiongozi kupita hii leo niko eneo la songwe airport ili kusubiri waziri mkuu apite hii imekaaje wana Jamiiforums.

...... tunekaa almost 2 hrs kusubir nabado hajapita huu ni kujifanya mungu mtu na yeye pia jambo hili analifurahia huu ni utumwa wa kifikra.
Mkifahamu scenario ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu utawala wa Nyerere, bwana Edward Moringe Sokoine, hakika hizi lawama zote mtazifuta, huwezi kufananisha viongozi top wa kitaifa na katibu wa kitongoji.
 
Back
Top Bottom