Je, ni sahihi kwa baba kumnunulia mtoto wake wa kike PEDI?

Je, ni sahihi kwa baba kumnunulia mtoto wake wa kike PEDI?

Baba kumnunulia mtoto wa kike pedi mwisho n miaka 20 na hiyo ni kama yuko shuleni hasa za bweni. Mtoto wa kike akifika umri huo akikuomba pesa ya matumizi wewe kama baba usianze uliza ni ya nini. Jiongeze tu utajua na pedi iko umo umo.
 
Haya mambo ya kumnunulia yanakujaje sasa?
Mnaishi wawili tu nyumbani na je hakuna mfanyakazi?
Hili swali halijamaliziwa lote
Kama mtu anaona sawa kwa mwanae wa kike je anaweza kumuuliza pia baada ya siku kadhaa kuwa damu zimekata?
Majukumu tunayo mengi msituongezee yasiyo ya lazima kwani wanawake wenzie hawapo
 
Panga ratiba ya kumpa hata 10,000 binti yako kila mwezi na umwambie ni kwa mahitaji madogomadogo yeye atajiongeza.

Lakini kwenda kumnunulia hapana. Kwa mazoea yepi? Mpaka anahitaji ped inamaanisha tayari amepuvuka anaweza kwenda dukani mwenyewe. Kwa nini uende wewe? Si sawa
 
Baba atafikishiwa ujumbe na mama kama Kuna badget kama izo na atatoa pesa kupitia kwa mama ila ilee ya moja kwa moja mtoto akadai kwa Baba haipendezi.. ila baba anatakiwa atoe huduma hii kama mtoto yupo nyumbani/chini yake
 
Back
Top Bottom