Je, ni sahihi kwa DSTV kuziweka ITV, EATV, Clouds TV na Channel Ten kwenye chaneli za kulipia?

Je, ni sahihi kwa DSTV kuziweka ITV, EATV, Clouds TV na Channel Ten kwenye chaneli za kulipia?

Uzaa dstv nunua unachoweza, acha kulialia... wakiona wateja wamepungua watafunga ofisi au watajitathimini kuboresha huduma...

Mkulima kala mbegu
 
Mbona mnapenda Bure sana ??! Hamjui hata vituo mnavyoviangalia vinaandaliwa kwa gharama na hawa DSTV nao wanauziwa hizo channel ?!
Unachanganya hizo ni FTA channels na kwa kanuni zilizopo TCRA zinapaswa kuwa bure. Na bahati mbaya waziri Nape siku za nyuma aliwaaminisha watu kuwa hizo ni bure.

Ikiwa hazitakiwi kuwa bure basi kanuni zibadilishwe. Unafikiri wakisema kuanzia sasa hakuna channels za bure watu hawatazilipia?
 
Mie namshauri Nape awape kibali DSTV nao warushe mpira ligi ya bongo
DSTV Tanzania wana hela ya kuwalipa TFF? na ikitokea wamewalipa wanaweza kuwa na gharama ya chini kama Azam?

Maana ili uone UEFA gharama yake ni zaidi ya kisimbuzi kipya full kit ya DSTV
 
Huenda mimi ndio sielewi basi nielimishwe, lakini kwa upeo wangu mdogo ninavyojua mimi hizo channel ITV, eatv, clouds na channel ten ni FTA channels sasa inakuwaje kifurushi cha Dstv kikiishia wanakuachia Tbc peke yake?

Mimi nina king'amuzi pia cha Star times hawa air time ikikuishia free channel zote zinabaki na unaangalia kama kawaida, sasa iweje Dstv inakata free channels?

Mheshimiwa Nape Nnauye kuli wewe tupo pamoja hapa JF kitambo tu tunakuomba ulipokee hili na ulifanyie kazi haraka, tusilazimishane hela za kula kununua vifurushi.

Kifurushi kikikata kama bajeti hairuhusu then uwe na access ya local free channel basi ili uchague taarifa ya habari uangalie wapi.

Sijawataja Wasafi hapo kwa sababu najua Wasafi ni channel ya kulipia, siyo free channel.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tuliwambia humu kuwa DSTV hawawezi kuweka channel ziruke bila kulipia kifurushi....hata Nape wenu tulisema hapa pengine hakuwa anajua anapigania nini!

DSTV hawawezi kukubali channel za bure zaidi ya TBC...lipeni ili mradi zimesharudi wekeni kifurushi si kuna hadi cha 9000?
 
Mbwembwe nyingi zilitumika kuaminisha watu kuwa hizi ni FTA Channels..... Halafu Waziri mwenyewe ndo alitumika kututapeli.

Kuna uzi uko kule nilisema was azi hata waziri pengine hajui alikuwa anapigania nini...ilikuwa ni propaganda tuu! Lakini cha msingi channel zipo watu walipie wazione sio mbaya kimsingi kama uanataka kuona maisha magic na umeweza kulipia basi hakuna shida lakini kamwe DSTV hawawezi kuonesha hizi channel bure wako radhi waziondoe kabisa!
 
DSTV Tanzania wana hela ya kuwalipa TFF? na ikitokea wamewalipa wanaweza kuwa na gharama ya chini kama Azam?

Maana ili uone UEFA gharama yake ni zaidi ya kisimbuzi kipya full kit ya DSTV
Unalinganisha DSTV na ITV nini? Sidhani kama unaifahamu kampuni ya DSTV
 
Aliyeziondowa alikuwa Dr Mwakyembe, wewe wahi zamu ya kulinda kaburi Chato.

Yule Dr mpuuzi Mwakyembe alikata hadi redio station kusoma magazeti kurasa za ndani waishie front page tu.

Awamu ya tano ilikuwa ni serikali ya mashetani yalioongozwa na Lucifer mkuu Pombe waliotamani Tanzania tuishi kama North Korea.

Tunamshukuru mama sasa anaifunguwa nchi, hata hili naamini litafanyiwa kazi.

Mkuu punguza mihemko Mwakyembe alikuwa ana simamia sheria maana kwa sheria DSTV alikuwa apaswi kuonesha channel za ndani na watoa huduma wa ving’amuzi walisema kama DSTV anataka kuchukua na channel za ndani basi alipe gharama kama wao walizo ingia...DSTV wakaambiwa wafate huo utaratibu ndio wakashindwa kwa hiyo wakaona waondoe hizo channel!

Halafu ving’-amuzi vingine walikuwa wanaona DSTV atawachukulia wateja wao ndio maana wakawa wanapinga yeye kuweka hizo channel bila kuingia gharama walizo ingia!

Nape alikuja akawaruhusu kuweka hizo channel lakini Nape hakuwa anaelewa wananchi walikuwa wanataka nini maana alikuwa ana furaha sana..lakini DSTV msimamo wao uko vile vile toka mwanzo kuwa wao hawatatoa huduma bure ...,(FTA) zaidi ya TBC kwa hiyo wako radhi waziondoe kama waziri akilazimisha!
 
Tena kama we bumunda si ulishangilia sana Nape aliposema zinarudi ukawa unamtukana Magufuli?

Hizo chanel zilitolewa kwenye DSTV baada ya Magufuli kusema zinapaswa kuonesha bure!

Ila mataputapu mkashangilia Nape aliposema zinarudi bila kujiuliza kilichofanya ziondolewe ni nini.


Copyright Crimea
 
Kwangu kifurushi kiliisha na channels zote za local zilikata, Ila baada ya siku mbili, ITV ,EATV, Clouds Tv, Channel ten na upendo TV zilirudi zote bure, baadae wiki moja mbele ndio nikalipia kifurush

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilishaachana na local channels!!! Zilinishinda kabisa upumbavu mtupu dstv oyeeeeeee siwezi kosa pesa y'a kulipia
uzaa dstv nunua unachoweza, hacha kulialia... wakiona wateja wamepungua watafunga ofisi au wata jitathimini kuboresha huduma...

mkulima kala mbegu
 
Back
Top Bottom