Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?


Post muhimu, hii inabidi ipigiwe kelele na ikemewe. Mimi nimekuja kwenye harusi, C umelipwa, kwanini tena utume picha zangu mitandaoni nikiwa nafurahia sherehe, tena bila ruhusa yangu. Kwenye kumbi huko ndio balaa, niko zangu nimelewa labda na Bar maid, au mchepuko una rekodi unatuma instagram. hii ipigwe marufuku.

Nafikiria kuja kuwashtaki hawa wahuni. Yaanbi wanafanya mambo kienyeji tu.
 
Pole sana unaenda kunywa au unaenda kupigwa picha?
 
Mjini kuna club ambazo huwezi ona video wala picha picha
Ila hizo bar sjui club zenu kitambaa cheusi kidimbwi nk mapichapicha mavideo watu wanajipigia tu

Ova
 
Umejiiba na mchepuke unashangaa picha zako hizooo
Tayar ushaletewa kesi ya kujibu 😄

Ova
 
MCs wa maharusi naona ndio trend na wanamulika zaidi pale mtu anapofanya vitu vya kijinga hata sababu ni pombe.
Binamu yangu mmoja ni Kanali, alichukua memory card ya kamera ya mpigapicha wa MC na kuondoka nayo na kumwambia ni marufuki kupiga picha au kuchukua video kwenye eneo la jeshi bila kibali maalumu.
Hiyo ilikuwa kwenye harusi pale "Golf Club".
 
kwa uhalisia kwenye sherehe inatakiwa mwenye sherehe amkanye MC haruhusiwi sambaza Video za tukio husika, wapiga picha binafsi hawaruhusiwi.
Privacy, yeye achukue pesa yake arekodi alete Flash
Camera man wanarecord then wanaenda kuedit/kufanya final cut na kukabidhi mzigo kwa wenyewe......
Vile vipande tata wanabaki navyo kwaajili ya kutupia youtube au kuuza kwa magroup
 
Natuliaga Kwenye Grocery Ya Bibie Shamimu Toto Nzuri La Tanga Naburudikaa Na Value Zangu Twala Zetu Na Kitimoto rosti Safiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…