Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Inaboa sana
Kuna night club moja hapa Dom pia Niliwahi kukutana na huo upuuzi Yaani nimekaa zangu nakunywa pombe na mchepuko wangu(mke wa mtu) nashangaa tunamulikwa na mwanga wa flash ya picha nilistuka sana na kumrukia yule mpiga picha ili nimng'oe meno ila yule dogo akajitetea kwamba amepewa kazi na wahusika ikabidi niombe kuonana na manager lakini naye akanijibu majibu ya kihuni tangu siku hiyo siendagi tena hapo Yaani ni upuuzi sana kupiga watu picha halafu wanaweka mitandaoni!
Imagine huyo afande jirani yangu angeona picha mitandaoni niko bar nakunywa pombe na mkewe ingekuwaje?!
Ogopa mke wa mtu unahatarisha afya ya sehemu yako ya nyuma
 
Huna akili,bila watu kuenda hivyo vinywaji watawauzia nani.

Kutokufata sheria ndio kunasababisha ufunguaji wa kiholela wa vigrosari/vijibaa mitaani.Hili nalo ni uvunjifu wa sheria za mipango miji.

Nchi hii uvunjifu wa sheria ni mkubwa sana na kuna mijitu tangu izaliwe hawajui kufata sheria🥱
Kaa nyumbani Kama haupendi kupigwa picha
 
Hii kitu haijakaa sawa.. Kwa mfano maeneo ya starehe pale kuna watu aina tofauti, wapo wengine na wake\waume za watu na heshima zao. Haya sasa umewachukua picha unapost social media bila kujali ubinafis wa mtu... Huon kuna mkanganyiko hapo ndan ya jamii
 
Hii inanihusu mim MME MWENZA, kwanzia leo nikienda club na mke wa mtu navaa musk, mume mwenzangu asinifaham endapo flash ya kamera ikipita
 
Kaa nyumbani Kama haupendi kupigwa picha
Nakondoo kama nyie ambao hamjui bila iyo elfu mbili yako huyo mmiliki wa bar ni fala tu ndio mnaongoza kwa kugongea bia.

Mtu yeyote mwenye anajua kutafuta hela na kuitumia hawezi kutoa majibu ya kifala kama yako.

Wewe ni aidha chawa au bado unalelewa hujiu kutafuta hela wala hujui hao wamiliki wanavyohaha hizo baa zikichacha🤗

Biashara ya baa ni ya msimu na kismati huo ushamba wa sheria za kiwaki unafanywa na malimbukeni kwa washamba wenzao.Ukijiwekea sheria za kifamba wakati faida ya chupa moja ya bia ni jero mpaka buku.Hiyo biashara yako haitasurvive miaka mitano.

📌📌📌Wamiliki wajifunze kuheshimu wateja wao unless mtu kafungua baa kutakatisha pesa hapo weka nyodo na sheria zako za kifala utakavyo,lakini kama unataka profit in baa business jxt be humbe and act kiprofessinal.
 
Kwenye masherehe naunga mkono hoja!
Ila kwenye bata hapana tunajitakia - mtu na heshima zako unaendaje kitambaa cheupe?
Kuna mahala pa kwenda huko hata ukipigwa picha watu wanaogopa! Na pakistaarabu huwa wanafanyaga promotion wanamlipa mtu ama wakipiga picha unakuta zile za familia
Naunga mkono hoja.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Miaka Ya Hivi Karibuni Kumeibuka Wimbi Kubwa La Wamiliki kuchapisha Picha Au Video Za Wateja Wao Katika Mitandao ya Kijamii Hali Ambayo Kwa Namna Moja Sio Nzuri Kwa Baadhi Ya Wateja.

Unaweza Kwenda Kwenye Baadhi ya Kumbi za Starehe Kipindi Ukipata Kinywaji Iadara Ya masoko Na Habari Wao hufanya Kazi Za Kurekodi Video Kwa Ajili ya Promotion .

Kwa Jicho La Marketing Strategy ni Nzuri Kwa Night Club hizo Kwani huongeza engagement Kwa Wateja Wao Na Kufikia Wateja Wengi Zaidi

Lakini Kwa uwanda Mwingine Huwa inashusha Heshima Na Hadhi hasa Pale unapojikuta Katika Mitandao ya Kijamii Bila ya Kuwa Na Idhini Mtaalam

Katika Hatua Nyingine Masters Of Ceremony Nao Wamekuwa Wakichapisha Picha Au Video Kipindi Cha Harusi Jambo Ambalo Sio Zuri Hasa Pale Ambapo Hakuna Ridhaa Kutoka Upande Wa Mteja

Watu Wengi Sana Wamekuwa Wakikuta Katika Mitandao ya Kijamii Jambo Ambalo Linatatiza Kuchanganya Katika Midhania Isiyo Sahihi

Kuna Mambo Ambayo Yanatakuwa Yafanyike Kuhakikisha kunakuwepo Na Usawa Katika ya Pande Mbili Ili kupunguza Migongano kati ya Wateja Na Wamiliki Wa Kumbi za Sherehe Au MC Katika Kazi Zao

Kisheria, wamiliki wa night club wanapaswa kuwa waangalifu wanapohusisha picha au video za wateja wao kwenye mitandao ya kijamii au kwenye matangazo bila idhini yao. Kwa ujumla, kuna kanuni kadhaa zinazopaswa kuzingatiwa:

1.Sheria za Faragha : Katika nchi nyingi, kuna sheria zinazolinda faragha ya watu binafsi. Kuchukua picha au video za mtu bila idhini yake inaweza kuzingatiwa kama uvunjaji wa faragha.

2. Idhini Wamiliki wa mali kama vile night club wanapaswa kupata idhini wazi kutoka kwa wateja kabla ya kuchapisha picha au video zao mtandaoni. Hii ni muhimu ili kuhakikisha kuwa wateja wanajua na kukubali kuwa picha zao zitashiriki Katika Machapisho ya Mitandao ya Kijamii

3. Matumizi ya Picha za Umma Katika hali fulani, kama vile matukio ya umma ambapo watu wanajulikana kuwa wanachukuliwa picha, sheria zinaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, ni vyema kuzingatia maadili na kuheshimu haki za binafsi.

4.Mkataba wa Huduma Wakati wa kuingia katika night club, kunaweza kuwa na mkataba (kwa mfano, kupitia alama au matangazo) ambao unaweza kueleza jinsi picha na video zitakavyokuwa zikitumiwa. Ni muhimu wamiliki wajue ikiwa hilo linaweza kutumika kisheria.

Katika hali yoyote, ni bora kwa wamiliki wa night club kufuata taratibu za kisheria na maadili ili kulinda haki za wateja wao na kuepuka matatizo ya kisheria.

Soma Pia: Tahadhari kwa MC's wa maharusi bongo
Bro kichwa cha habari umeuliza swali, halafu ndani kwenye habari umejijibu mwenyewe... daah😃😃 Wanda shall never end...


Anyway, bongo hakuna privacy, kila kitu ni public. So best option ni kubaki nyumbani
 
Bro kichwa cha habari umeuliza swali, halafu ndani kwenye habari umejijibu mwenyewe... daah😃😃 Wanda shall never end...


Anyway, bongo hakuna privacy, kila kitu ni public. So best option ni kubaki nyumbani
Bongo kuna sehemu zingine ukienda picha l,video kuchkua marufuku

Ova
 
Back
Top Bottom