Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Na Thadei Ole Mushi.

Nimeisoma Barua ya Msando yote aliyowaandikia USA.

1. Achana na Makosa ya Address aliyoyafanya Brother Msando twende kwenye Hoja nyingine za barua ya Msando. Kwenye barua ile kuanzia mwanzo Hadi Mwisho Msando kaonyesha kuwa hata Marekani huwa wanavunja haki za binadamu. Msando anataka kutuaminisha kuwa Marekani leo wakiamua Kula Kinyesi na sisi ni sawa kukila. Hakuna mahali ambapo Msando kaweza kusema Kama ni kweli haki za Binadamu zinavunjwa ama lah!... Kwa kifupi Msando anatuambia kuwa ni Kweli tumekiuka haki za Binadamu simply kwa kuwa Marekani nao wanazivunja.

2. Issue za Kidiplomasia hujibiwa Kidiplomasia na hupitia Chanel ambazo ni sahihi. Kilichofanywa na Msando ni kutaka kufurahisha watawala lakini akumbuke kuwa barua yake inazidi kuzorotesha uhusiano wetu na Marekani. Mh Kabudi sio mjinga kutafakari, Serikali kwa ujumla sio wajinga kutokumjibu Pompeo, wanatafakari kwa namna gani wanaweza kusulihisha mgogoro huu wa Kidiplomasia. Fani hii ya Diplomasia watu huisomea huwezi kukurupuka tu from no where mtu individual ambaye Hana taaluma hiyo kuanza kutuhumu mataifa Mengine. Kwa bahati mbaya kabisa barua ile copy yake ameielekeza kwa Rais wetu. Msando Hana tofauti na vijana waliovamia ubalozi wa S.A kudai Bombadia.

3. Msando naye kaingia kwenye Makosa yale yale kuwa naye anatetea ukiukwaji wa haki za Binadamu. Kwa maana hiyo Msando Siku akiwa Kiongozi hawezi kutuwakilisha Tena Marekani pamoja na washirika wake.

4. Serikali na hasa Rais hahitaji utetezi Sana anachohitaji ni Solutions, tunatetea Sana badala ya kutoa solutions. Barua ya Msando haitoweza kuitisha Marekani na Wala Marekani haitobadili msimamo kwa sababu ya barua ya Msando. Kwa maana hiyo bado tatizo linabaki na linaweza kukuzwa kwa barua hii ya Msando. Tumepoteza uwezo wa kutoa Solutions kwa sababu ya kusaka madaraka na Vyeo.

5. Kuna kasumba imeibuka kuwa ili uwe mzalendo Kila Jambo la Serikali ni la kutetea, nchi hii haiwezi kujengwa kwa kutetea makosa, nchi hii itajengwa kwa kuyaondoa makosa, kuambiana ukweli kuwa hili hapana lile sawa.

Wahenga walisema "two wrongs don't make a right". Narudi Jalalani..

Ole Mushi
0712702602
Nimeona nisipoteze muda kujibu ulichoandika hapa kwani kwa uelewa wako unadhani alichofanya msando ni formal reply kwa hatua ya Marekani.
 
1. Makonda ban
2. Mary ******* ban
3. Msando ban
4. Mambo sasa ban
4. Sabaya ban
5. Jaffo ban and the Hague
6. Magu ban and the Hague
7. Heri James ban and the Hague
8. Mwigulu ban ,ban,ban, ban and the Hague kunyongwa
9. Kabud ban ila macho yake yamemsaidia kuona mbali
10. Pole pole ban
11.
12.
13.
Silioni jina lako hapa
 
Msando Ni balozi au kitu gani
Hapana! Si balozi, bali kwa barua yake anajaribu zari achaguliwe kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.

Msando ana "akili" kweli kweli. Anajua msimamo na hulka ya Jiwe dhidi ya "mabeberu" ni kutoa majibu kwa "hoja za kimapambano" dhidi yao mabeberu. Je, unakumbuka zile "hoja za kitaalam" zilizotolewa na wasomi wetu wa masuala ya mazingira katika kutetea mradi wa umeme kwenye Stigler's Gorge? Basi Msando naye "kapita mule mule"!
 
Ole Mushi Msando hajaandika kwa niaba ya serikali au chama chochote au kikundi chochote kilicho sajiriwa.
Kuna hoja ya msingi ya Msando kwamba kuna mikataba tuliyo tia sahini ambayo imeweka utaratibu wa jumuiya za kimatifa kuichukulia nchi flani hatua nchi au mtu mmoja anapotuhumiwa mambo ya uhalifu na uvunjanji haki aliotuhumiwa Makonda na serikali ya Tanzania kwa ujumla..

Nijia hizo ndio zinaweka utaratibu rasmi wa kuhakiki kama mtuhumiwa ana hatia na hizo tuhuma au hana hatia.
Kujisemea tu sisi nchi flani tunazo taarifa za uhakika kwamba huyu kafanya au anafanya hivi bila kupitia hizo taratibu sio sahihi, maana hata sasa tunakumbuka Marekani alisema ana taarifa za kuaminika Sadam Hussein anatengeneza silaha za maangamizi.

Kilichotokea sote tunakijua, na baadae wanarudi kusema taarifa hazikuwa sahihi. Nani analipia au anarudisha maisha na malizi za watu zilizo angamia kutokana na taarifa hizo zisizo sahihi ambazo walisema taarifa za uhakika (reliable info/intel)?

Ole Mushi anakubaliana na Marekani kusambaza tuhuma na zuio lile kwenye mitandao kabla ya hizo njia za kidiplomasia anazo taka Msando au Tanzania wafuate. Huu ni unafiki na double standard!
Basi aseme tu Marekani ana haki ya kufanya chochote na sisi watanzania tuna baadhi tu ya haki za kufanya mambo fulani na sio yote.

Mnachofanya ni kumkana Msando sasa?

Well
 
Lini mwananchi akaijibia barua serikali, kwenda nchi nyingine?
Pascal think twicely before you over took.

Sent using Jamii Forums mobile app
Freedom of expression ni uhuru wa kusema lolote kwa yeyote. Hata wewe uko huru kuandika barua kwa Trump, kwa Papa, kwa Magufuli, kwa mpenzi wako au kwa yeyote expressing your opinion on anything alimradi hujavunja sheria yoyote.
P
 
Mwanahabari Huru, Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Inaonekana awamu hii imezalisha wazalendo wengi sana kama ilivyojenga viwanda vingi tangu nchi hii ipate uhuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri kinachotusumbua 'na kinakachoendelea kutusumbua si suala la uzalendo bali tafsiri ya hilo neno uzalendo. Likitafsriwa kiimani au kiitikadi basi maana yake itapotea, lakini likimaanishwa kama linavyomaanisha maana yake itakamilika.
Tupe tafsiri yako ya neno uzalendo ambayo wewe unaona inafaa kwa vipimo vyote.
 
Mwanahabari Huru, Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Basi Bora angejibu Makonda mwenyewe..Kaka mbona munatetea ujinga?Kuna muda tuwe tunafikiria,kwahiyo kila mmoja akiandika barua ya utetezi kupeleka Marekani itakuwaje?na je anayo andika kila mmoja ni yepi?na yataleta taswira gani?Hii sio yakujibiwa na individual

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You're right, Keyword is "Official Communication". Those official communication zinatakiwa kuwa ni mambo yanayohususiana kwa namna fulani na jimbo lako. Unapoandika barua tena to the international organization, talking about national issues, your actiong at what capacity, an MP, a Leader of opposition, or concern citizen? Maana kila moja hapo inatakaiwa utumie karatasi inayohusina na nafasi yake kama leader of opposition then use party head paper, Kama ni mwananchi wa kawaida then you do as what Msando did. On top of that, your using parliament papers kuongea na foreign organization bila kibali cha foreign office, kama sio kuvunja kanuni kwa makusudi ndio uanzishe zogo ni nini?
Kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali, Mbunge yoyote yuko huru kutumia nembo ya Bunge kuandika barua popote, kama ilivyo japo Mbunge ni Mbunge wa jimbo Tanzania na ni Mbunge wa Bunge la Tanzania, akienda popote nje ya nchi anakwenda kama Mbunge wa Bunge la JMT.

Kufuatia Bunge letu Kujipendekeza kwa serikali
Hadi kupindukia, tumefikia kiwango cha Bunge as Bunge haliwezi tena kuisimamia serikali, hivyo Mbunge as an individual, anaweza kubeba jukumu hilo kama Zitto alivyofanya na kutumia nembo ya Bunge sio favours sio hisani ni haki yake, its his right.
P
 
Diplomacy ina respond to official government statement and position; sio barua za individuals.

If anything UDSM waanze kuandaa proffesional skills modules; kama wenzao wanavyofanya kwenye first degree.

Unakuta mtu ni prominent figure kwa viwango vyetu vya Tanzania awezi ata kuandika proffesionally; formal letter gani ndefu vile you just summarize staff mtu akifungua tu barua refu vile anaona mwandishi sio mtu makini.

Awawezi ichukulia hiyo barua kama mtazamo wa serikari it’s just Msando viewpoint.
 
Ole Mushi Msando hajaandika kwa niaba ya serikali au chama chochote au kikundi chochote kilicho sajiriwa.
Kuna hoja ya msingi ya Msando kwamba kuna mikataba tuliyo tia sahini ambayo imeweka utaratibu wa jumuiya za kimatifa kuichukulia nchi flani hatua nchi au mtu mmoja anapotuhumiwa mambo ya uhalifu na uvunjanji haki aliotuhumiwa Makonda na serikali ya Tanzania kwa ujumla..

Nijia hizo ndio zinaweka utaratibu rasmi wa kuhakiki kama mtuhumiwa ana hatia na hizo tuhuma au hana hatia.
Kujisemea tu sisi nchi flani tunazo taarifa za uhakika kwamba huyu kafanya au anafanya hivi bila kupitia hizo taratibu sio sahihi, maana hata sasa tunakumbuka Marekani alisema ana taarifa za kuaminika Sadam Hussein anatengeneza silaha za maangamizi.

Kilichotokea sote tunakijua, na baadae wanarudi kusema taarifa hazikuwa sahihi. Nani analipia au anarudisha maisha na malizi za watu zilizo angamia kutokana na taarifa hizo zisizo sahihi ambazo walisema taarifa za uhakika (reliable info/intel)?

Ole Mushi anakubaliana na Marekani kusambaza tuhuma na zuio lile kwenye mitandao kabla ya hizo njia za kidiplomasia anazo taka Msando au Tanzania wafuate. Huu ni unafiki na double standard!
Basi aseme tu Marekani ana haki ya kufanya chochote na sisi watanzania tuna baadhi tu ya haki za kufanya mambo fulani na sio yote.
Inabidi uwe kichaa kutetea mauaji na kupotea watu watu wasiona hatia. Ama kweli mkuki kwa ngurue ila kwa inadamu ni mchungu. Siku zote uovu unapoinuka lazima ukenewe na kulaaniwa kwa nguvu zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom