Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Amekosea wapi au kwanini unadhani amekosea, hivi tunavyozungumza Sen. Adam Schiff ameshafanya yake akidai Trump atauza Alaska kwa Canada... it is called freedom of expression...
Msando hajakosea katika kuandika hicho alichoandika. Haki ya kufanya hivyo anayo.

Hakuna tofauti ya alichokifanya Msando na tukifanyacho humu JF.

Alichokosea ni kwenye ‘substance’ katika alichokiandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanahabari Huru,
Msando hana hoja katika barua yake, lakini kama Mtanzania ana haki ya kikatiba ya kujieleza, kuandika barua ubalozi wa Marekani, State Department, White House, New York Times, Washington Post, Jamiiforums etc.

Wamarekani wenyewe tunapenda uhuru wa kujieleza na tunamuona anatumia uhuru wake huo, hata kama hoja zake zina mushkeli mwanzo mwisho.

Natetea haki yake ya kujieleza hata kama sikubaliani na anachoeleza.
Mbona wengine wakitumua uhuru wao kujieleza wakawa,wnasingiziwa kesi hiyo huoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni kama protesting letter, ni sawa kabisa, kuna njia nyingi za kufanya protesting, kuandamana, kubeba mabango, kuandika barua, kusimama mbele ya yule anayekutendea isivyo, kuchoma picha ya yule mlengwa kupinga anachokufanyia, hivyo mwanasheria msomi yuko sahihi kabisa, kupeleka ujumbe kwa njia ya barua kwamba USA wanachofanya siyo sahihi kabisa, mbona Rwanda, Uganda, Saudi Arabia ambako hakuna demokrasis na mauaji ni kila siku hakuna zuio kama hilo, nenda South America, Mexico ambako kila siku zaidi ya watu 100 wanauwawa kila siku hakuna katazo kwa viongozi wake. Kuna tofauti gani kati ya Zitto na Snowden snitch wa kimarekani ambaye kapata amnesty uko Russia, Snowden leo hii akitia mguu USA siku ya pili ni kitanzi tu au life in prison. JPM kukata minyororo ya wizi kwa kushirikiana na hawa wezi weusi ndiyo imeleta shida yote hiyo. Kila siku hawa wezi weusi wanapeleka matako yao uko kwa mabwana zao kuleta tafaruku kwenye jamii. USA hana urafiki wa kudumu yeye ni personal interest tu, hizo interest zikiisha hakuna tena urafiki unakuwa adui. Hivyo akina Zitto, Membe, Nyalandu, Lissu, na wengine ambao wako undercover USA haitawasadia kama ambavyo wanaamini.
Kwahiyo unataka tanzania ifikie mauji ya watu 100 kwa siku kama nchi ulizotaja ndio uone kuna tatizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mitaala ya shule zetu tangu primary hadi chuo Kikuu, tunapaswa tuwe na mtaala wa uzalendo ili Tanzania tuzalishe wasomi wazalendo badala ya kuzalisha wasomi mamluki.
P
Hilo somo litaitwaje bwana Pascal...somo la uzalendo kitabu gani. Au uko njiani kukitunga. Kuna Somo la Civics, ni somo tosha kumfundisha kijana kuitambua nchi, principles za uongozi, mihimili ya nchi, sasa uzalendo upi mnaousema, au kila mtu akosoaye serikali ya JPM sio mzalendo. Mbona akina Kitila Mkumbo na hao akina Bashiri walikosoa sana kabla ya kupata teuzi, walikuwa sio wazalendo halafu wako kwenye ofisi za umma? Acheni fikira ndogo hizo. Ifanyeni shule kuwa kipimo cha Fikra zenu na acheni njaa za asubuhi.
 
Mwanahabari Huru, Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Hawa wanafichua uwakala wao wa mabeberu. Hajui kwamba katika nchi ya demokrasia ya kweli hata yeye anaruhusiwa kuandika anachotaka.

Wanasema awamu hii inazuia uhuru wa kujieleza, Msando akitumia uhuru wake wao wanaupinga uhuru huo!.
 
Msando kaandika ukweli mtupu. Marekani wana ubaguzi wa kimfumo wenye kuwatesa watu weusi.

Wamarekani wamewafanyia unyama usioelezeka raia wa Iraq, Afghanistan na Pakistan lakini wao hawastahili kuambiwa ukweli!.

Wameivuruga Libya mpaka kesho inashindwa kurudi katika hali bora ya zamani.
 
Mabeberu ni nani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mabeberu wanatokana na ubeberu.
Ubeberu ni imperialism.
Imperialism is the highest stages of capitalism.
Nchi mabeberu ni nchi tajiri, zinatumia utajiri wao kuendeleza ukoloni mambo leo na ubeberu.

Hatua ya kwanza ni kuja kwa kujifanya wanakuja kusaidia, misaada, fedha, FDI, mikopo, mitaji etc, hivyo tunawaita, nchi rafiki, nchi wafadhili, nchi washirika wa maendeleo, hivyo faida yote ya uwezaji wao, inarudi kwao,hivyo kuendelea kutunyonya. Kwa kawaida fedha zao huwa zinaandamama na masharti fulani, kama good governance, respect to human rights, transparency etc.

Sasa wanapoanza kutukosoa ndipo sasa tunaanza kupiga kelele za mabeberu. Hivyo hawa mabeberu ndio wale wale wahisani, marafiki na wafadhili.
P
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Wanamaanisha uzalendo wa kuvaa mabendera/scarf kama nchemba ambaye sasa habari tena sijui wanamwitaje huko lumumbav
Hilo somo litaitwaje bwana Pascal...somo la uzalendo kitabu gani. Au uko njiani kukitunga. Kuna Somo la Civics, ni somo tosha kumfundisha kijana kuitambua nchi, principles za uongozi, mihimili ya nchi, sasa uzalendo upi mnaousema, au kila mtu akosoaye serikali ya JPM sio mzalendo. Mbona akina Kitila Mkumbo na hao akina Bashiri walikosoa sana kabla ya kupata teuzi, walikuwa sio wazalendo halafu wako kwenye ofisi za umma? Acheni fikira ndogo hizo. Ifanyeni shule kuwa kipimo cha Fikra zenu na acheni njaa za asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diplomacy ina respond to official government statement and position; sio barua za individuals.

If anything UDSM waanze kuandaa proffesional skills modules; kama wenzao wanavyofanya kwenye first degree.

Unakuta mtu ni prominent figure kwa viwango vyetu vya Tanzania awezi ata kuandika proffesionally; formal letter gani ndefu vile you just summarize staff mtu akifungua tu barua refu vile anaona mwandishi sio mtu makini.

Awawezi ichukulia hiyo barua kama mtazamo wa serikari it’s just Msando viewpoint.

Actually niliisoma ile barua haifanani na kuandikwa na learned brother. Haina mvuto wa kimalkia.
 
CHA MSINGI TUJITAFAKARI YOTE YALIYOAINISHWA NA USA YAMETENDEKA NCHINI KWETU? NA JE KAMA YAMEFANYWA KINA NANI WAPO NYUMA YA YOTE HAYO? KISHA TUNAJISAFISHAJE?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanahabari Huru, Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Tamaa ya madaraka itakuponza kaka njaa, inakuwaje tunalilia pesa za mabeberu?
Kilichochafuliwa ni serikali ya ccm na wala si nchi.
Nchi imehusika vipi kuua raia wake na kuwaweka katika viroba?
KUTETEA SERIKALI NA CCM SI UZALENDO!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ktk makosa ambayo kama taifa tutakuwa tumefanya ni kuruhusu hiyo barua kwenda kwa taifa kubwa kama USA, kwani badala ya kuponyesha kidonda ndiyo itazidi kukitia bakteria na kukifanya kuoza kabisa.

Msando ni nani kwenye uongozi wa kitaifa wa nchi hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani Kama Msando kamuwskilisha kiongozi yeyote Wala kaiwakilisha serikali

Itakua alikua kaboreka na ana hamu ya cheo... Kwahiyo akaamua kutype

Hard to put it any other way
 
Back
Top Bottom