Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Amekosea wapi au kwanini unadhani amekosea, hivi tunavyozungumza Sen. Adam Schiff ameshafanya yake akidai Trump atauza Alaska kwa Canada... it is called freedom of expression...
Msando hajakosea katika kuandika hicho alichoandika. Haki ya kufanya hivyo anayo.

Hakuna tofauti ya alichokifanya Msando na tukifanyacho humu JF.

Alichokosea ni kwenye ‘substance’ katika alichokiandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wengine wakitumua uhuru wao kujieleza wakawa,wnasingiziwa kesi hiyo huoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo unataka tanzania ifikie mauji ya watu 100 kwa siku kama nchi ulizotaja ndio uone kuna tatizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mitaala ya shule zetu tangu primary hadi chuo Kikuu, tunapaswa tuwe na mtaala wa uzalendo ili Tanzania tuzalishe wasomi wazalendo badala ya kuzalisha wasomi mamluki.
P
Hilo somo litaitwaje bwana Pascal...somo la uzalendo kitabu gani. Au uko njiani kukitunga. Kuna Somo la Civics, ni somo tosha kumfundisha kijana kuitambua nchi, principles za uongozi, mihimili ya nchi, sasa uzalendo upi mnaousema, au kila mtu akosoaye serikali ya JPM sio mzalendo. Mbona akina Kitila Mkumbo na hao akina Bashiri walikosoa sana kabla ya kupata teuzi, walikuwa sio wazalendo halafu wako kwenye ofisi za umma? Acheni fikira ndogo hizo. Ifanyeni shule kuwa kipimo cha Fikra zenu na acheni njaa za asubuhi.
 
Mwanahabari Huru, Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Hawa wanafichua uwakala wao wa mabeberu. Hajui kwamba katika nchi ya demokrasia ya kweli hata yeye anaruhusiwa kuandika anachotaka.

Wanasema awamu hii inazuia uhuru wa kujieleza, Msando akitumia uhuru wake wao wanaupinga uhuru huo!.
 
Msando kaandika ukweli mtupu. Marekani wana ubaguzi wa kimfumo wenye kuwatesa watu weusi.

Wamarekani wamewafanyia unyama usioelezeka raia wa Iraq, Afghanistan na Pakistan lakini wao hawastahili kuambiwa ukweli!.

Wameivuruga Libya mpaka kesho inashindwa kurudi katika hali bora ya zamani.
 
Mabeberu ni nani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mabeberu wanatokana na ubeberu.
Ubeberu ni imperialism.
Imperialism is the highest stages of capitalism.
Nchi mabeberu ni nchi tajiri, zinatumia utajiri wao kuendeleza ukoloni mambo leo na ubeberu.

Hatua ya kwanza ni kuja kwa kujifanya wanakuja kusaidia, misaada, fedha, FDI, mikopo, mitaji etc, hivyo tunawaita, nchi rafiki, nchi wafadhili, nchi washirika wa maendeleo, hivyo faida yote ya uwezaji wao, inarudi kwao,hivyo kuendelea kutunyonya. Kwa kawaida fedha zao huwa zinaandamama na masharti fulani, kama good governance, respect to human rights, transparency etc.

Sasa wanapoanza kutukosoa ndipo sasa tunaanza kupiga kelele za mabeberu. Hivyo hawa mabeberu ndio wale wale wahisani, marafiki na wafadhili.
P
 
Reactions: Lee
Wanamaanisha uzalendo wa kuvaa mabendera/scarf kama nchemba ambaye sasa habari tena sijui wanamwitaje huko lumumbav
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Actually niliisoma ile barua haifanani na kuandikwa na learned brother. Haina mvuto wa kimalkia.
 
CHA MSINGI TUJITAFAKARI YOTE YALIYOAINISHWA NA USA YAMETENDEKA NCHINI KWETU? NA JE KAMA YAMEFANYWA KINA NANI WAPO NYUMA YA YOTE HAYO? KISHA TUNAJISAFISHAJE?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanahabari Huru, Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Tamaa ya madaraka itakuponza kaka njaa, inakuwaje tunalilia pesa za mabeberu?
Kilichochafuliwa ni serikali ya ccm na wala si nchi.
Nchi imehusika vipi kuua raia wake na kuwaweka katika viroba?
KUTETEA SERIKALI NA CCM SI UZALENDO!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani Kama Msando kamuwskilisha kiongozi yeyote Wala kaiwakilisha serikali

Itakua alikua kaboreka na ana hamu ya cheo... Kwahiyo akaamua kutype

Hard to put it any other way
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…