Je, ni sawa kwa Wanajeshi kurekodi video kama hizi na kuzisambaza mtandaoni?

VHayo ni mafunzo? Au unacomment tu mradi tubishane Mkuu?.... Rudia vizuri kusoma nilichoandika bwana Daktari, sheria ilikuwa signed Dec, kutumika imeanza May 2023, kairejee na uweke rekodi zako sawa
 
Mkuu; unauhakika gani kama hilo sio igizo?
Mbona hatumuoni afande anayetoa Amri ila wewe unamtaja afande Sese wa Oljoro. Hatuwaoni wanaocheka (JKT huwezi kucheka hovyo-hovyo namna ile)
Uniform za JKT sio hiyo alovaa huyo muigizaji. T-shirt Kijani ya Jeshi na Bukta ya blue vinaeleweka hata jinsi vilivyoshonwa. Uwekaji wa nywele na usimamaji wa aliyerekodiwa umekaa kimtaani / kiraia sana. Hakuna kitu kama hiko JKT.
  • Je, ww unabifu na huyo afande?
  • Je ww umewahi kupitia JKT au ulitoroka JKT? au basi walau mafunzo ya mgambo? Mbona inaonekana kama unakitu fulani dhidi ya JKT? Huipendi JKT?
Mkuu elewa kabisa JKT ni Chuo cha mafunzo kama zilivyo shule zingine.Mtu unaingia shuleni hujui 1+1 = 2 lakini baada ya mafunzo unajua hata zaidi ya hapo. JKT inaamini kwamba Kuruta hajui hata kutembea. Ndo mana kuna smart area ambapo kuruta hupita hapo kwa kukimbia.
Kuruta (Kuruta One)hufunga mguu kwa kuruka na kutamka"MOJA".
Je, mbona huyo chalii hapo hana ivo vigezo?
Hiyo ni Chai -bila sukari wala maandazi -TUPA KULEE.
 
Hakuna Kosa hapo..
Hakuna Mtu anayejua Lengo la mchukuaji Video zaidi ya mchukuaji mwenyewe..

HIsia za Muonaji Sio hisia za mchukuaji..
Kwahyo Hakuna kosa hata kidogo..

Kisheria Na wala Ethically labda kama una Mada nyingine
Kosa lipo. Ni utovu wa heshima ya faragha.

Mitandao ya kijamii imeleta MASS PSYCHOSIS, ugonjwa wa akili unaosababisha binadamu kubehave kama kundi la nyumbu!

Kuna haja gani ya kurekodi? ili iweje?

Huu ni udhihirisho tosha kwamba hawa migambo ni wahitimu wa MADIVISHENI FOO.

Hawa ndio wanaopewa mamlaka ya kutulazimisha tubugie MACHANJO yenye MERCURY kwa kutucharaza mijeledi endapo tukigoma.

Mie nehii, hayo masumu mdungane wenyewe kwa kweRi.
 
Kwanza kabla ya kuchangia is it Unethical au Crime..
Hapo kwanza nataka kujua..

Ni kosa la Kinidhamu/Kitaaluma/maadili (Ethics)..
Au ni kosa la Uhalifu (Breaking the law)..

Tuwekane sawa kwanza.. hapo..

Kama ni Kosa la Kimaadili Tutajadili
Kama ni kosa la uhalifu "Kuvunja sheria" ningependa sheria zilizovunjwa Ziwekwe tuzione..

Na kingine uko sawa kabisa kuhusu Paragraph ya Pili na ndicho nilichokisema..

Kuchukua Video kwa matumizi ya kijeshi hakuna kosa lolote shida aliyesambaza video hizo anapatikana na kosa la Kimaadili na wala sio kuvunja sheria..

usisahau kwamba anaweza akawa amechukua Video ila aliyesambaza akawa ni mwingine..
 
Afadhali kuna mtu anayeelewa kilichofanyika hapa! DR Mambo Jambo take notes
 
Mhhhhhhhhhhhh! Urongo!
 
Hakuna Kosa hapo..
Hakuna Mtu anayejua Lengo la mchukuaji Video zaidi ya mchukuaji mwenyewe..

HIsia za Muonaji Sio hisia za mchukuaji..
Kwahyo Hakuna kosa hata kidogo..

Kisheria Na wala Ethically labda kama una Mada nyingine
Hakuna kosa eti ? Kulikuwa na uhalali gani hiyo video kupanda mitandaoni ? Idhini katoa nani ?
Mlengwa ameridhia maudhui ya yeye kufanyiwa kebehi kupanda mtandaoni ?

Anza na hayo kwanza
 
Asante Mkuu. Tunataka kuhalalisha hili sababu aliyefanya ni mwanajeshi
 
VHayo ni mafunzo? Au unacomment tu mradi tubishane Mkuu?.... Rudia vizuri kusoma nilichoandika bwana Daktari, sheria ilikuwa signed Dec, kutumika imeanza May 2023, kairejee na uweke rekodi zako sawa
Mkuu sitaki Kujua elimu yako Kwenye swala la sheria ila inanifanya nipate Wasiwasi wa kuanza kuihoji..

Unajua Sheria ikichapishwa kwenye Gazeti la serikali maana yake?
 
Hakuna Aliyedhalilishwa hapo.Naomba unionyeshe Sheria iliyovunjwa
Una uhakika hakuna aliye dhalilishwa ? Kwamba aliye tendewa kafurahishwa na hicho kitendo na karidhia kuwekwa kwenye mitandao umma wote waone ?
 
Wametenda makosa yote, ya kimaadili na uhalifu pia.
 
Kasome vizuri nilichondika, sijasema namjua, nimesema kwa mujibu wa comments kutoka kwenye video hiyo mtandaoni. Mkuu, mpaka unatafuta visababu vyote hivyo kutetea hili naamini umeona kabisa kosa hili. Ingekuwa igizo tungeona kwenye official page zao, wakitaja tukio pamoja na taarifa nyingine. Kama upo kwenye kada hiyo saidia kuelimisha wenzako kuliko kutetea ujinga
 
Hakuna kosa eti ? Kulikuwa na uhalali gani hiyo video kupanda mitandaoni ? Idhini katoa nani ?
Mlengwa ameridhia maudhui ya yeye kufanyiwa kebehi kupanda mtandaoni ?

Anza na hayo kwanza
Umeongea Mlengwa?
Mlengwa amekulalamikia?
Kuhusu kupanda Video mtandaoni Ni kosa la Mchukuaji au la mpandishaji?

Unakua Sheria ya JKT, Mbona za mafunzo mengine zikivuja mtandaoni hamlalamiki?

Kukosea ni moja ya Njia ya kujifunza Huenda Mchukuliwaji alitaka ili Akihitimu aone alivyoingia na alivyotoka..

Ukiona umeingia Jeshini na unalalamika kuhusu Kuchukuliwa Video rudi kijijini Video zinachukuliwa mpaka Vitani seuze kwenye mafunzo..
By the way sheria ga mafunzo ya Jkt inaruhusu Kuchukua Picha mjongeo.wakati wa mafunzo
 
Unakua Sheria ya JKT, Mbona za mafunzo mengine zikivuja mtandaoni hamlalamiki?
Yaani una nipangia kipi cha kulalamikia na kipi cha mimi kuto kulalamikia kama vile wanifahamu na una uhakika gani kuwa silalamiki kwa mengine kuhusu jeshi ?

Au unaandika tu kujifurahisha?
 
Huenda, huenda, huenda tuliza kichwa chako vizuri na soma unachoandika hauongei na wendawazimu hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…