Je, ni sawa kwa Wanajeshi kurekodi video kama hizi na kuzisambaza mtandaoni?

Habari Precious Diamond..
Ni hakika Sheria uitajayo Haupo aware nayo kabisa.
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ni sheria Namba 11 ya Mwaka 2022 (2nd December)..
Na sio may 2023..(Tuanze na hapo)

Imeanza Kutumika Tarehe 2 Mwezi December mwaka 2022 na Ilitangazwa Katika gazzete la serikali La Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Gazeti la serkali Namba 45 Toleo la 103 la Tarehe 2" December, 2022 (Gazette of the United Republic of Tanzania No. 45 Vol. 103 Dated 2" December, 2022)...

Tafsiri ya "Taarifa Binafsi.."Hakuna Umbo wala sura Wala Picha jongeo,.hiyo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 3 Cha sheria hiyo ya Ulinzi wa Taarifa binafsi..

Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa No 16 ya mwaka 1964 Sura 193 [R.E 2002] Inaruhusu Kuchukua Picha Jongeo katika mafunzo ili kuweka kumbukumbu Ya maendeleo ya mafunzo..

Karibu Mkuu
VHayo ni mafunzo? Au unacomment tu mradi tubishane Mkuu?.... Rudia vizuri kusoma nilichoandika bwana Daktari, sheria ilikuwa signed Dec, kutumika imeanza May 2023, kairejee na uweke rekodi zako sawa
 
Wakuu kwema?

Nimekutana na video hii mtandaoni, ambako huyu 'kuruta' (kama sijakosea) anapewa amri ya kugeuka kulia na kushoto, kijana huyo anafata maagizo aliyopewa huku anayetoa maagizo na wengine wakisikika wakicheka.

Nini dhumuni la kurekodi video hizi mpaka kufikia hatua ya kuzirusha mtandaoni? Anayerekodiwa ameridhia? Na hii sio mara ya kwanza kukutana na video kama hizi mtandaoni, za hawa wanafunzi wanaokwenda jeshi kwa mujibu wa sheria kurekodiwa katika matukio mbalimbali.

Huu ni udhalilishaji wa utu wake, tayari watu washaanza kutoa maoni mbalimbali juu ya muonekano wake, maumbile na kadhalika, kwa hali tu ya kawaida hakuna mtu angependa kurekodiwa katika hali hiyo na video hiyo irushwe kwa kila mtu kuona.

Hii sio sawa, kwanza ukipewa amri hapo lazima ufate, usipofata ni kukaidi na udhabu unapewa. Kwanini tunahalalisha udhalilishaji huu uendelee kutokea na kuonekana na kawaida? Wanajeshi wapo juu ya Sheria? Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wao haiwahusu?

Aliyechukua video hii awajibishwe, Jeshi kama chombo cha ulinzi wanatakiwa kuwa mfano kwenye kufata sheria na sio kuwa wa kwanza kwenda kinyume na kudhalilisha utu wa watu.

Kutoka kwenye comments za video hiyo anayesikika akitoa amri ni Afande Sese, JKT Oljoro.

Sheria iwe msumeno, sio ikate kwetu tu halafu kwao kuwe butu.

Mkuu; unauhakika gani kama hilo sio igizo?
Mbona hatumuoni afande anayetoa Amri ila wewe unamtaja afande Sese wa Oljoro. Hatuwaoni wanaocheka (JKT huwezi kucheka hovyo-hovyo namna ile)
Uniform za JKT sio hiyo alovaa huyo muigizaji. T-shirt Kijani ya Jeshi na Bukta ya blue vinaeleweka hata jinsi vilivyoshonwa. Uwekaji wa nywele na usimamaji wa aliyerekodiwa umekaa kimtaani / kiraia sana. Hakuna kitu kama hiko JKT.
  • Je, ww unabifu na huyo afande?
  • Je ww umewahi kupitia JKT au ulitoroka JKT? au basi walau mafunzo ya mgambo? Mbona inaonekana kama unakitu fulani dhidi ya JKT? Huipendi JKT?
Mkuu elewa kabisa JKT ni Chuo cha mafunzo kama zilivyo shule zingine.Mtu unaingia shuleni hujui 1+1 = 2 lakini baada ya mafunzo unajua hata zaidi ya hapo. JKT inaamini kwamba Kuruta hajui hata kutembea. Ndo mana kuna smart area ambapo kuruta hupita hapo kwa kukimbia.
Kuruta (Kuruta One)hufunga mguu kwa kuruka na kutamka"MOJA".
Je, mbona huyo chalii hapo hana ivo vigezo?
Hiyo ni Chai -bila sukari wala maandazi -TUPA KULEE.
 
Hakuna Kosa hapo..
Hakuna Mtu anayejua Lengo la mchukuaji Video zaidi ya mchukuaji mwenyewe..

HIsia za Muonaji Sio hisia za mchukuaji..
Kwahyo Hakuna kosa hata kidogo..

Kisheria Na wala Ethically labda kama una Mada nyingine
Kosa lipo. Ni utovu wa heshima ya faragha.

Mitandao ya kijamii imeleta MASS PSYCHOSIS, ugonjwa wa akili unaosababisha binadamu kubehave kama kundi la nyumbu!

Kuna haja gani ya kurekodi? ili iweje?

Huu ni udhihirisho tosha kwamba hawa migambo ni wahitimu wa MADIVISHENI FOO.

Hawa ndio wanaopewa mamlaka ya kutulazimisha tubugie MACHANJO yenye MERCURY kwa kutucharaza mijeledi endapo tukigoma.

Mie nehii, hayo masumu mdungane wenyewe kwa kweRi.
 
It's unethical.
Kitendo alichofanya huyu Mwanajeshi ni Ni kosa kisheria. Anapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sana aliotendewa huyu kijana.

Kama kurekodi video kwa ajili ya matumizi ya Jeshi ilikuwa sahihi, lakini video hizo zilizorekodiwa na Jeshi ni lazima zitumike kwa matumizi ya Jeshi tu, wala siyo vinginevyo. Kamwe video hizo hazipaswi kuwekwa publicly, ni mwiko kabisa tena ni kosa kubwa, unless kuwepo na ridhaa ya anayerekodiwa au kutokana na sababu maalumu kabisa za lazima ambazo hazizuiliki.
Kwanza kabla ya kuchangia is it Unethical au Crime..
Hapo kwanza nataka kujua..

Ni kosa la Kinidhamu/Kitaaluma/maadili (Ethics)..
Au ni kosa la Uhalifu (Breaking the law)..

Tuwekane sawa kwanza.. hapo..

Kama ni Kosa la Kimaadili Tutajadili
Kama ni kosa la uhalifu "Kuvunja sheria" ningependa sheria zilizovunjwa Ziwekwe tuzione..

Na kingine uko sawa kabisa kuhusu Paragraph ya Pili na ndicho nilichokisema..

Kuchukua Video kwa matumizi ya kijeshi hakuna kosa lolote shida aliyesambaza video hizo anapatikana na kosa la Kimaadili na wala sio kuvunja sheria..

usisahau kwamba anaweza akawa amechukua Video ila aliyesambaza akawa ni mwingine..
 
Afadhali kuna mtu anayeelewa kilichofanyika hapa! DR Mambo Jambo take notes
 
Habari Precious Diamond..
Ni hakika Sheria uitajayo Haupo aware nayo kabisa.
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Ni sheria Namba 11 ya Mwaka 2022 (2nd December)..
Na sio may 2023..(Tuanze na hapo)

Imeanza Kutumika Tarehe 2 Mwezi December mwaka 2022 na Ilitangazwa Katika gazzete la serikali La Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Gazeti la serkali Namba 45 Toleo la 103 la Tarehe 2" December, 2022 (Gazette of the United Republic of Tanzania No. 45 Vol. 103 Dated 2" December, 2022)...

Tafsiri ya "Taarifa Binafsi.."Hakuna Umbo wala sura Wala Picha jongeo,.hiyo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 3 Cha sheria hiyo ya Ulinzi wa Taarifa binafsi..

Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa No 16 ya mwaka 1964 Sura 193 [R.E 2002] Inaruhusu Kuchukua Picha Jongeo katika mafunzo ili kuweka kumbukumbu Ya maendeleo ya mafunzo..

Karibu Mkuu
Mhhhhhhhhhhhh! Urongo!
 
Hakuna Kosa hapo..
Hakuna Mtu anayejua Lengo la mchukuaji Video zaidi ya mchukuaji mwenyewe..

HIsia za Muonaji Sio hisia za mchukuaji..
Kwahyo Hakuna kosa hata kidogo..

Kisheria Na wala Ethically labda kama una Mada nyingine
Hakuna kosa eti ? Kulikuwa na uhalali gani hiyo video kupanda mitandaoni ? Idhini katoa nani ?
Mlengwa ameridhia maudhui ya yeye kufanyiwa kebehi kupanda mtandaoni ?

Anza na hayo kwanza
 
Kosa lipo. Ni utovu wa heshima ya faragha.

Mitandao ya kijamii imeleta MASS PSYCHOSIS, ugonjwa wa akili unaosababisha binadamu kubehave kama kundi la nyumbu!

Kuna haja gani ya kurekodi? ili iweje?

Huu ni udhihirisho tosha kwamba hawa migambo ni wahitimu wa MADIVESHENI FOO.

Hawa ndio wanaopewa mamlaka ya kutulazimisha tubugie MACHANJO yenye MERCURY kwa kutucharaza mijeledi endapo tukigoma.

Mie nehii, hayo masumu mdungane wenyewe kwa kweRi.
Asante Mkuu. Tunataka kuhalalisha hili sababu aliyefanya ni mwanajeshi
 
VHayo ni mafunzo? Au unacomment tu mradi tubishane Mkuu?.... Rudia vizuri kusoma nilichoandika bwana Daktari, sheria ilikuwa signed Dec, kutumika imeanza May 2023, kairejee na uweke rekodi zako sawa
Mkuu sitaki Kujua elimu yako Kwenye swala la sheria ila inanifanya nipate Wasiwasi wa kuanza kuihoji..

Unajua Sheria ikichapishwa kwenye Gazeti la serikali maana yake?
 
Hakuna Aliyedhalilishwa hapo.Naomba unionyeshe Sheria iliyovunjwa
Una uhakika hakuna aliye dhalilishwa ? Kwamba aliye tendewa kafurahishwa na hicho kitendo na karidhia kuwekwa kwenye mitandao umma wote waone ?
 
Kwanza kabla ya kuchangia is it Unethical au Crime..
Hapo kwanza nataka kujua..

Ni kosa la Kinidhamu/Kitaaluma/maadili (Ethics)..
Au ni kosa la Uhalifu (Breaking the law)..

Tuwekane sawa kwanza.. hapo..

Kama ni Kosa la Kimaadili Tutajadili
Kama ni kosa la uhalifu "Kuvunja sheria" ningependa sheria zilizovunjwa Ziwekwe tuzione..

Na kingine uko sawa kabisa kuhusu Paragraph ya Pili na ndicho nilichokisema..

Kuchukua Video kwa matumizi ya kijeshi hakuna kosa lolote shida aliyesambaza video hizo anapatikana na kosa la Kimaadili na wala sio kuvunja sheria..

usisahau kwamba anaweza akawa amechukua Video ila aliyesambaza akawa ni mwingine..
Wametenda makosa yote, ya kimaadili na uhalifu pia.
 
Mkuu; unauhakika gani kama hilo sio igizo?
Mbona hatumuoni afande anayetoa Amri ila wewe unamtaja afande Sese wa Oljoro. Hatuwaoni wanaocheka (JKT huwezi kucheka hovyo-hovyo namna ile)
Uniform za JKT sio hiyo alovaa huyo muigizaji. T-shirt Kijani ya Jeshi na Bukta ya blue vinaeleweka hata jinsi vilivyoshonwa. Uwekaji wa nywele na usimamaji wa aliyerekodiwa umekaa kimtaani / kiraia sana. Hakuna kitu kama hiko JKT.
  • Je, ww unabifu na huyo afande?
  • Je ww umewahi kupitia JKT au ulitoroka JKT? au basi walau mafunzo ya mgambo? Mbona inaonekana kama unakitu fulani dhidi ya JKT? Huipendi JKT?
Mkuu elewa kabisa JKT ni Chuo cha mafunzo kama zilivyo shule zingine.Mtu unaingia shuleni hujui 1+1 = 2 lakini baada ya mafunzo unajua hata zaidi ya hapo. JKT inaamini kwamba Kuruta hajui hata kutembea. Ndo mana kuna smart area ambapo kuruta hupita hapo kwa kukimbia.
Kuruta (Kuruta One)hufunga mguu kwa kuruka na kutamka"MOJA".
Je, mbona huyo chalii hapo hana ivo vigezo?
Hiyo ni Chai -bila sukari wala maandazi -TUPA KULEE.
Kasome vizuri nilichondika, sijasema namjua, nimesema kwa mujibu wa comments kutoka kwenye video hiyo mtandaoni. Mkuu, mpaka unatafuta visababu vyote hivyo kutetea hili naamini umeona kabisa kosa hili. Ingekuwa igizo tungeona kwenye official page zao, wakitaja tukio pamoja na taarifa nyingine. Kama upo kwenye kada hiyo saidia kuelimisha wenzako kuliko kutetea ujinga
 
Hakuna kosa eti ? Kulikuwa na uhalali gani hiyo video kupanda mitandaoni ? Idhini katoa nani ?
Mlengwa ameridhia maudhui ya yeye kufanyiwa kebehi kupanda mtandaoni ?

Anza na hayo kwanza
Umeongea Mlengwa?
Mlengwa amekulalamikia?
Kuhusu kupanda Video mtandaoni Ni kosa la Mchukuaji au la mpandishaji?

Unakua Sheria ya JKT, Mbona za mafunzo mengine zikivuja mtandaoni hamlalamiki?

Kukosea ni moja ya Njia ya kujifunza Huenda Mchukuliwaji alitaka ili Akihitimu aone alivyoingia na alivyotoka..

Ukiona umeingia Jeshini na unalalamika kuhusu Kuchukuliwa Video rudi kijijini Video zinachukuliwa mpaka Vitani seuze kwenye mafunzo..
By the way sheria ga mafunzo ya Jkt inaruhusu Kuchukua Picha mjongeo.wakati wa mafunzo
 
Yaani una nipangia kipi cha kulalamikia na kipi cha mimi kuto kulalamikia kama vile wanifahamu na una uhakika gani kuwa silalamiki kwa mengine kuhusu jeshi ?

Au unaandika tu kujifurahisha?
 
Umeongea Mlengwa?
Mlengwa amekulalamikia?
Kuhusu kupanda Video mtandaoni Ni kosa la Mchukuaji au la mpandishaji?

Unakua Sheria ya JKT, Mbona za mafunzo mengine zikivuja mtandaoni hamlalamiki?

Kukosea ni moja ya Njia ya kujifunza Huenda Mchukuliwaji alitaka ili Akihitimu aone alivyoingia na alivyotoka..

Ukiona umeingia Jeshini na unalalamika kuhusu Kuchukuliwa Video rudi kijijini Video zinachukuliwa mpaka Vitani seuze kwenye mafunzo..
By the way sheria ga mafunzo ya Jkt inaruhusu Kuchukua Picha mjongeo.wakati wa mafunzo
Huenda, huenda, huenda tuliza kichwa chako vizuri na soma unachoandika hauongei na wendawazimu hapa.
 
Back
Top Bottom