Je, ni Siasa za sasa za Tanzania ndizo zinawakwaza IMF na WB hadi hawatujali tena Watanzania au kuna 'Kirusi' Kimewakwaza sana?

Je, ni Siasa za sasa za Tanzania ndizo zinawakwaza IMF na WB hadi hawatujali tena Watanzania au kuna 'Kirusi' Kimewakwaza sana?

Mpaka leo najiuliza hili Swali ni kwanini Taasisi Kubwa na Muhimu kabisa za Masuala ya Fedha Duniani (Ulimwenguni) za WB (Benki ya Dunia) na IMF (Shirika la Fedha Duniani) kwa Siku za karibuni na niweke tu wazi tokea 2016 hadi huu wa 2020 wamekuwa ' Wazito ' mno Kuisaidia Tanzania kwa Pesa (Fedha) tofauti na ilivyokuwa huko nyuma?

Je, ni Siasa za Tanzania labda ndizo ' zimewakwaza ' hivi au labda yawezekana kukawa na ' Kirusi ' kisicho na Jina ambacho kipo Tanzania na labda hata Sisi Watanzania hatukijui ndicho kimewakera na kuwakatisha tamaa hivi ya Kutusaidia tofauti na nchi zingine kadhaa za Afrika kama za Rwanda, Uganda, Ethiopia, Ghana ambazo zinapewa kila wakati?

Tumewakosea nini WB na IMF?

Nawasilisha.
Nkujuze wewe hasa. Mlimchagua mtu aliyekuwa black listed na mashirika makubwa ya fedha ya dunia (hasa WB). Ipo sababu nayo ni kuwa awamu ya tatu tulikuwa wapenzi haya mashirika. Mtu wenu alionyesha waziwazi uimla kwenye fedha zilizotolewa na WB akitaka yeye ndiye aziamulie akiwa waziri. Wataalamu wa ndani ya serikali wakati huo walisimama kidete kuweka mambo sawa kwa kuwa walitambua nafasi yao ya kitaalamu. Sasa hivi wafanyakazi wataalam waliopo wanatekeleza maigizo toka juu kwa mtu ambaye hajaondolewa kwenye black list ya wakubwa zaidi ya kudhihirisha tabia yake kwenye madaraka ya juu kabisa ya nchi ya uimla hata kwenye maamuzi ya kitaalamu.

Tutarajie neema tutakapochagua viongozi wanaoheshimu taratibu za uongozi na siyo unyapara.
 
Mpaka leo najiuliza hili Swali ni kwanini Taasisi Kubwa na Muhimu kabisa za Masuala ya Fedha Duniani (Ulimwenguni) za WB (Benki ya Dunia) na IMF (Shirika la Fedha Duniani) kwa Siku za karibuni na niweke tu wazi tokea 2016 hadi huu wa 2020 wamekuwa ' Wazito ' mno Kuisaidia Tanzania kwa Pesa (Fedha) tofauti na ilivyokuwa huko nyuma?

Je, ni Siasa za Tanzania labda ndizo ' zimewakwaza ' hivi au labda yawezekana kukawa na ' Kirusi ' kisicho na Jina ambacho kipo Tanzania na labda hata Sisi Watanzania hatukijui ndicho kimewakera na kuwakatisha tamaa hivi ya Kutusaidia tofauti na nchi zingine kadhaa za Afrika kama za Rwanda, Uganda, Ethiopia, Ghana ambazo zinapewa kila wakati?

Tumewakosea nini WB na IMF?

Nawasilisha.
Fanya subira, upinzani utakapoiniga Ikulu, viongozi wake wataenda kuwapigia magoti na kuwalamba miguu ili wapewe mikopo na misaada. Kwa Rais Magufuli, wao imebidi waje kumpigia magoti.
 
Kenya na Uganda mbona nao hawajapewa?
Vipi Kagame anayejulikana ni dikteta mbona kapata? Hakuna hoja hapa
 
Uko sahihi ila ni kwanini hizo Hela wanazotupa huwa wanazitoa kwa ' Mbinde ' sana wengine Kwanza twende Vijijini Kwetu tukatambike kwa Mabibi, Mababu na tukeshe Ziwani tukitizama Samaki au Mbugani tukipiga Mbizi katika Mawe makubwa makubwa?

Huko nyuma WB na IMF walikuwa wakiipenda sana Tanzania yetu ila kwa sasa Uhusiano wetu nao umekuwa ni wa ' Kimazabe ' mno. au Wewe hulioni hili? Hebu lifuatilie kwa umakini wako tafadhali.
Ww nawe mshamba kweli hela yoyote ya kukopa haitolewi kirahisi
 
Mkuu ni hivi majuzi tu nilikuwa naperuzi viwango vya IQ duniani nikaona kwa Africa mashariki Taifa lako pendwa Rwanda liko chini sana.

Rwanda wana IQ ndogo Africa Mashariki juu tu ya Burundi.
 
Haya majitu ya ajabu sn hayashiriki mbongo ni mapumbafu.Ukweli ni kwamba hatuna mahusiano mazuri na hiz multilateral financial insts kwa sababu ya upuuzzi wetu wa kutozingatia baadhi ya mikataba ya kimataifa ya haki za binadam pamoja kujitutumua kulikopitiliza,tatizo hawajui kwangu tupo kwenye ulimwengu wa utandawaz hata ukiwatukana mabeberu kisukuma wanajua,mijitu haioni shida kuandaa mswada kwa ajili ya kumkomoa aidha tundu lisu au zitto bila kujali athari na maslahi mapana ya kitaifa.Lakini kubwa zaidi ni kuwa na maviongozi mabinafs zaidi ya shetani,yaani mtu yupo tayari kuonesha ujeuri na misimamo ya kipuuzi huku maelf ya watu wakiangamia.Mathalani tulikua tunapewa ruzuku ya chanjo na US kwa watoto kwa sabab serikali na wananchi wake hawana uwezo wa kumudu,ruzuku hii inamasharti ya kuhamasisha uzaz wa mpango,bwana mkubwa bila kujielewa na kutafuta sifa za kipuuzi akasema hakuna uzaz wa mpango fyatueni serikali ya awamu ya tano ina hela,kutokana na maamuzi ya kipuzi huko mbeleni tutarajie high mortality death rates kwa sababu chanjo hii ni gharama around 80k,wananchi wa kawaida hawawez kumudu.

Mchango wako huu mzuri na wenye Tija na Mantiki kamwe baadhi ya tulionao hawawezi Kuchangia hivi Mkuu. Heko! Huwa napenda mno Kukutana na Watu wenye ' Akili ' nyingi na ' Uelewa ' pamoja na Uchambuzi mahiri wa ' Issues ' kama Wewe hapa Jamvini JamiiForums. Nimekukubali mno na Asante kwa ulichokiwasilisha hapa ambacho nakubaliana nacho kwa 99.99999%.

Cc: Ruttashobolwa
 
Mkuu ni hivi majuzi tu nilikuwa naperuzi viwango vya IQ duniani nikaona kwa Africa mashariki Taifa lako pendwa Rwanda liko chini sana.

Rwanda wana IQ ndogo Africa Mashariki juu tu ya Burundi.

Hoja ya Msingi hapa Mezani ni WB na IMF dhidi ya Tanzania Kimahusiano yake au ni GENTAMYCINE na Rwanda yake?
 
Mpaka leo najiuliza hili Swali ni kwanini Taasisi Kubwa na Muhimu kabisa za Masuala ya Fedha Duniani (Ulimwenguni) za WB (Benki ya Dunia) na IMF (Shirika la Fedha Duniani) kwa Siku za karibuni na niweke tu wazi tokea 2016 hadi huu wa 2020 wamekuwa ' Wazito ' mno Kuisaidia Tanzania kwa Pesa (Fedha) tofauti na ilivyokuwa huko nyuma?

Je, ni Siasa za Tanzania labda ndizo ' zimewakwaza ' hivi au labda yawezekana kukawa na ' Kirusi ' kisicho na Jina ambacho kipo Tanzania na labda hata Sisi Watanzania hatukijui ndicho kimewakera na kuwakatisha tamaa hivi ya Kutusaidia tofauti na nchi zingine kadhaa za Afrika kama za Rwanda, Uganda, Ethiopia, Ghana ambazo zinapewa kila wakati?

Tumewakosea nini WB na IMF?

Nawasilisha.
1:Hatubembelezi. Hence Siasa zetu za Sasa ni tofauti na kabla ya 2016.
Kama enzi za Kambarage. Tunakopa popote hatufungwi na yeyote
2: Sio Berger's Tena,we are donners.
 
Mkuu Gentamycine, sina hakika kama umemsikiliza Mhe. Zitto hivi majuzi alivyoichambua ripoti ya CAG. Moja ya tatizo kubwa la serikali hii Ni matumizi holela yasiyofuata sheria. Yaani mtu anaamua kutumia fedha bila kuingiza kwenye mfuko mkuu wa hazina.
Zaidi ya hapo kuna matumizi mabaya kwenye miradi isiyoidhinishwa wala kupitishwa na Bunge. Mbaya zaidi ni ufichaji wa hasara inayotokana na matumizi hayo mabaya. Mfano wa kuchukua fedha benki kuu kwenda kununua korosho, na baada ya kupata hasara, ukaguzi huru ukazuiwa ili hasara isidhihirike kwa umma.
Hii ni miongoni mwa mifano inayoifanya IMF na WB watuone tunanuka.
 
Mkuu WB wameshaidhinisha USD 500 million mkuu juzi tu au umesahau tena zile Zitto na Wanaharakati walishindwa kuzizuia pamoja na kufunga safari kwenda US!

Je umesoma na kuelewa kuwa zimeidhinishwa kwa utaratibu upi na vigezo vipi??
 
Je umesoma na kuelewa kuwa zimeidhinishwa kwa utaratibu upi na vigezo vipi??

Kiingereza hicho cha Kuisoma hiyo Ripoti kakijulia wapi na lini Mkuu? Ukitaka kujua kuwa ni ' Mtupu ' angalia hata tu ' arguments ' zake hapa zilivyo ' very shallow ' ndipo utanielewa ninachosema au kukimaanisha dhidi yake. Na wapo wengi kweli katika Uzi wangu waangalie tu taratibu utawaona.
 
Wanatufundisha kujitegemea, it's a good move.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikia ndugu... Hizo pesa tunazihitaji sana., Na si ajabu serikali yako ikatuma ombi ijumuishwe kwenye "second round"...
Binafsi nilipenda utaratibu wa Big Ben na Kikwete kuzunguka huko na huko kuanzisha "urafiki wa mashaka/kinafiki na kuchukua vya Wazungu ili kujenga na kuboresha maendeleo ya vitu na watu nchini Tanzania.
Ukweli ni kuwa Wazungu walitupora na kutunyonya kwa miaka mingi sana... Harakati zozote za kutumia akili kurejesha rasilimali zetu ni muhimu sana...
Hoja hapa ilikuwa kuimarisha nidhamu ya makusanyo, misaada na matumizi yetu!!
Utaratibu wa kujimwambafy na kuhisi kuwa tunaweza kujitegemea kwa kila kitu ni sera nzuri lakini Ni ya kishamba sana...
Tunapaswa kutumia akili na kuwa very strategic kujikita katika kuchukua vya Wazungu ili kusaidia kuboresha maendeleo hapa nchini... Utaratibu huu utarahisisha maendeleo ya watu na ukuaji wa uchumi endelevu bila kuwakamua wananchi wetu!!
In the end GOT needs money probably more than its citizens!!
 
mkuu @gentamycin ushasema kuanzia 2016-2020 mpaka hapo dhahiri tatizo ni viongozi wa awamu hii wakiongozwa na jiwe kuu
 
Mkuu WB wameshaidhinisha USD 500 million mkuu juzi tu au umesahau tena zile Zitto na Wanaharakati walishindwa kuzizuia pamoja na kufunga safari kwenda US!
Swali limeulizwa kwanini ni wazito?
Hata hii 500 yenyewe imeletwa na mashrti kibao,,, ni kama imeidhinishwa na Zito mwenyewe maana masharti yote aliyotoa Zito wameyaweka mle.

Mi nadhani hawa wazungu wanapenda mtu ambaye wanaweza kumwendesha wanavyotaka lakini akitoke mtu mwenye msimamo usioyumba kama rsis wetu Tz wanakuwa na chuki naye hivyo kuwa wazito pindi tunapohitaji msaada wao.

Lakini mi naona si mbaya sana,,,, inatubidi tujitegemee siyo tuwategemee ,,la sivyo uhuru wetu na utu wetu utachezewa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom