MAGALEMWA
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 6,413
- 4,885
Nkujuze wewe hasa. Mlimchagua mtu aliyekuwa black listed na mashirika makubwa ya fedha ya dunia (hasa WB). Ipo sababu nayo ni kuwa awamu ya tatu tulikuwa wapenzi haya mashirika. Mtu wenu alionyesha waziwazi uimla kwenye fedha zilizotolewa na WB akitaka yeye ndiye aziamulie akiwa waziri. Wataalamu wa ndani ya serikali wakati huo walisimama kidete kuweka mambo sawa kwa kuwa walitambua nafasi yao ya kitaalamu. Sasa hivi wafanyakazi wataalam waliopo wanatekeleza maigizo toka juu kwa mtu ambaye hajaondolewa kwenye black list ya wakubwa zaidi ya kudhihirisha tabia yake kwenye madaraka ya juu kabisa ya nchi ya uimla hata kwenye maamuzi ya kitaalamu.Mpaka leo najiuliza hili Swali ni kwanini Taasisi Kubwa na Muhimu kabisa za Masuala ya Fedha Duniani (Ulimwenguni) za WB (Benki ya Dunia) na IMF (Shirika la Fedha Duniani) kwa Siku za karibuni na niweke tu wazi tokea 2016 hadi huu wa 2020 wamekuwa ' Wazito ' mno Kuisaidia Tanzania kwa Pesa (Fedha) tofauti na ilivyokuwa huko nyuma?
Je, ni Siasa za Tanzania labda ndizo ' zimewakwaza ' hivi au labda yawezekana kukawa na ' Kirusi ' kisicho na Jina ambacho kipo Tanzania na labda hata Sisi Watanzania hatukijui ndicho kimewakera na kuwakatisha tamaa hivi ya Kutusaidia tofauti na nchi zingine kadhaa za Afrika kama za Rwanda, Uganda, Ethiopia, Ghana ambazo zinapewa kila wakati?
Tumewakosea nini WB na IMF?
Nawasilisha.
Tutarajie neema tutakapochagua viongozi wanaoheshimu taratibu za uongozi na siyo unyapara.