Nakumbuka kuna siku natoka Arusha kwenda Moshi mjini niko na BMW 5 Series.
Hicho kipande cha Arusha Moshi sipendi kuendesha bila kumkimbiza Prey (kwa tuliosoma Wildlfe Prey animal (mfano Swala) ni wanyama wanaoliwa na predator).
Nimeendesha mpaka maeneo ya KIA sijapata changamoto yoyote ya maana ya kufukuzana, Kuna mjinga wa Land cruiser Hardtop nilimprovoke tukimbizane akanitolea nje.
Nikawa naendesha mdogo mdogo kusubiria prey mwingine, eeh bana ikapita Gx 100 kibati.
Nikamwacha anipoteze kabisa asinione ili ajisifu. Nikatupia kitu kwenye sport mode.
170 huyu hapa, jamaa anahangaika kucheki kwenye rear mirror, mbele kulikuwa na mteremko fulani, nikasema nikimpita hapa atasingizia mteremko.
Nikashuka naye kitu kinasoma 180, na jamaa alitegemea kwenye mteremko atachanganya zaidi aniache, akicheki niko nyuma yake, tukakamata tambarare, nikawasha indicator nataka kuchomoka.
Jamaa akapaniki zaidi akaniwashia indicator ya kushoto kuniruhusu nipite halafu huku anaendelea kukanyaga kibati kisiri siri 180.
Nikampita na lengo jamaa asione kabisa break light baada ya kilometa kadhaa nikasimama nikojoe nimsubirie jamaa apite nimfukuze tena.
Hahaha jamaa alisimama akaniambia kaka nimekubali mziki, naomba niangalie dash board hii mashine inasoma ngapi.
Siku nyingine gari ilifungwa spea pump flani nikasema wacha niende barabara ya ngaramtoni nikatest hiyo pump kama inapiga kazi vizuri.
Eeh bana natiririka na 170 kurudi town, ghafla kwa mbele naona fuso linatolewa gereji linasukumwa barabarani liwake.
Wale jamaa waliokuwa wanasukuma walivyoona nakuja kwa moto mkali wakaacha gari wakakimbia kunusuru maisha yao.
Nilimwambia Mungu pokea roho yangu.
Usinitanie nikaingiza gari shambani. Nikala shamba la mahindi kama movie vile.
Nyingine natoka Arusha kwenda mto wa mbu mida ya saa 2 usiku. Nakimbia kumtafuta prey huko mbele mara Hilux double cabin yeboyebo hii hapa.
Kwa kweli jamaa alikuwa anafukia sio mchezo, nikasema huyu nisimpite nimchoshe hapo nyuma 170/180/190
Jamaa akawasha indicator anaingia kulia kama vile amefika. Nikasema huyu usikute amedhani majambazi ananikataa kijanja.
Kweli baada ya kukata kulia akasimama akawa ananisikilizia. Nikasepa zangu mdogo mdogo namuona anakuja nyuma yangu, nikimsubiria apite hapiti. Nikachimba zangu.