Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
Aiseeh hizi TDI ni noma mkuu.Speed 240 na golf 5 tdi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aiseeh hizi TDI ni noma mkuu.Speed 240 na golf 5 tdi
Upo kama baba chanja wangu anapenda sana kuweka ligi barabarani basi na mie hua nampampu "aah sio kweli huyu anatupitaje kwa mfano" anachochea moto,Nakumbuka kuna siku natoka Arusha kwenda Moshi mjini niko na BMW 5 Series.
Hicho kipande cha Arusha Moshi sipendi kuendesha bila kumkimbiza Prey (kwa tuliosoma Wildlfe Prey animal (mfano Swala) ni wanyama wanaoliwa na predator).
Nimeendesha mpaka maeneo ya KIA sijapata changamoto yoyote ya maana ya kufukuzana, Kuna mjinga wa Land cruiser Hardtop nilimprovoke tukimbizane akanitolea nje.
Nikawa naendesha mdogo mdogo kusubiria prey mwingine, eeh bana ikapita Gx 100 kibati.
Nikamwacha anipoteze kabisa asinione ili ajisifu. Nikatupia kitu kwenye sport mode.
170 huyu hapa, jamaa anahangaika kucheki kwenye rear mirror, mbele kulikuwa na mteremko fulani, nikasema nikimpita hapa atasingizia mteremko.
Nikashuka naye kitu kinasoma 180, na jamaa alitegemea kwenye mteremko atachanganya zaidi aniache, akicheki niko nyuma yake, tukakamata tambarare, nikawasha indicator nataka kuchomoka.
Jamaa akapaniki zaidi akaniwashia indicator ya kushoto kuniruhusu nipite halafu huku anaendelea kukanyaga kibati kisiri siri 180.
Nikampita na lengo jamaa asione kabisa break light baada ya kilometa kadhaa nikasimama nikojoe nimsubirie jamaa apite nimfukuze tena.
Hahaha jamaa alisimama akaniambia kaka nimekubali mziki, naomba niangalie dash board hii mashine inasoma ngapi.
Siku nyingine gari ilifungwa spea pump flani nikasema wacha niende barabara ya ngaramtoni nikatest hiyo pump kama inapiga kazi vizuri.
Eeh bana natiririka na 170 kurudi town, ghafla kwa mbele naona fuso linatolewa gereji linasukumwa barabarani liwake.
Wale jamaa waliokuwa wanasukuma walivyoona nakuja kwa moto mkali wakaacha gari wakakimbia kunusuru maisha yao.
Nilimwambia Mungu pokea roho yangu.
Usinitanie nikaingiza gari shambani. Nikala shamba la mahindi kama movie vile.
Nyingine natoka Arusha kwenda mto wa mbu mida ya saa 2 usiku. Nakimbia kumtafuta prey huko mbele mara Hilux double cabin yeboyebo hii hapa.
Kwa kweli jamaa alikuwa anafukia sio mchezo, nikasema huyu nisimpite nimchoshe hapo nyuma 170/180/190
Jamaa akawasha indicator anaingia kulia kama vile amefika. Nikasema huyu usikute amedhani majambazi ananikataa kijanja.
Kweli baada ya kukata kulia akasimama akawa ananisikilizia. Nikasepa zangu mdogo mdogo namuona anakuja nyuma yangu, nikimsubiria apite hapiti. Nikachimba zangu.
Tabora - Nzega ni barabara tamu sana.... maana unajiachia uwezavyo.Speed kubwa kabisa ni 250kmh.. 180kmh ya kawaida kabisa kwangu [emoji38][emoji38][emoji38] hizi nazikata sana Barbara ya tabora nzega, au tabora manyoni.. au dodoma to singida Kuna vipande mafuta hii
Kwa kipande hicho halaliLC 200 GXR
Niligonga 200KPH lakini kuna muda niligusa hadi 240KPH ambayo ndiyo mwisho wa kisahani
Ilikuwa Mafinga to Makambako tulikuwa tunatoka Dar kuenda Mbeya na tulikuwa tunapokezana kuendesha
[emoji23][emoji23][emoji23]Upo kama baba chanja wangu anapenda sana kuweka ligi barabarani basi na mie hua nampampu "aah sio kweli huyu anatupitaje kwa mfano" anachochea moto,
Kuna siku ujinga wa Bara tukaupeleka Zenji barabara kule bado sana halafu traffic wapo macho balaa, tukapigwa fine tukatulia.
Ni kweli kabisaaTutafute pesa tu mkuu Mjerumani ndo magari
Cc990 tena manualIna engine gani mkuu?
Mhhhh!!!! Acha tuwaachie wenyewe akina crown wamalize kisahaniU
ngekaza kamba hadi 18Okph
Sema umasikini ndo unatufanya tuone toyota ndo magari mazuriNi kweli kabisaa
Ligi kufanya na mjerumani ni kujichosha Tu mwiliMwaka juzi jamaa yangu alikuwa anapeleka gari yake kwa mteja Moshi BMW 3 series.
Tukaongozana kutoka Arusha kuelekea Moshi ikawa mashindano barabarani BMW 5 Series vs BMW 3 series.
Aisee walioumia barabarani ni wajapan.
Jamaa yangu alikuwa mwoga wa spidi nikiwa nyuma yake namwangalia jinsi Mark X inavyomtoa jasho kuipita.
Nampigia simu namuuliza ni biashara gani unafanya hapo mbele, anajibu namlia timing.
Nikamwambia usimpite tena, angalia mashine inavyopita, niliwakata kwa spidi ya 200kph.
Hii barabara ina humps tatu tu180km/h ...Dodoma to Kondoa