Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Nishapiga 240kph nikiwa na GLE.

Nishapiga 250kph nikiwa na X3.

Sijawahi toboa 170kph nikiwa na harrier.

Mission iliobaki ni kuchukua M competition na kupiga above 270kph mpaka 300.
Ni kwamba Harrier hazipo stable mkuu au?
 
Mwaka juzi jamaa yangu alikuwa anapeleka gari yake kwa mteja Moshi BMW 3 series.

Tukaongozana kutoka Arusha kuelekea Moshi ikawa mashindano barabarani BMW 5 Series vs BMW 3 series.

Aisee walioumia barabarani ni wajapan.

Jamaa yangu alikuwa mwoga wa spidi nikiwa nyuma yake namwangalia jinsi Mark X inavyomtoa jasho kuipita.

Nampigia simu namuuliza ni biashara gani unafanya hapo mbele, anajibu namlia timing.

Nikamwambia usimpite tena, angalia mashine inavyopita, niliwakata kwa spidi ya 200kph.
Asee we ni nyokoo [emoji91][emoji91][emoji91]
 
mkuu umenikumbusha mbali sana.
2017 Landrover impala Petroli. nilifika 140. kutoka Marangu mtoni mpaka Himo. hiyo 140 niliipata hapo Marangu sec. ukiwa dereva kuna vitu unafanya halafu unaona haina maana. stage hiyo ukivuka wewe ni dereva mzuri. ila kama unapenda tu kuendelea wewe sio dereva mzuri.
Vipi kurudia tena mkuu? [emoji23]
 
Aah me sio muoga mtu ninayemuamini akiniendesha ila nikiendesha mimi ndio nakua muoga, speed mwisho 80, narudi kwenye 60,
Yanini mieee akaaaaa
Kuna aunt yangu anagonga Vx 1hdt manual hadi speed 160 afu hana hata habari..... wamama wenzake huwa wanaogopa kupanda gari yake. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nikikumbuka kuna Rafiki yangu alikua na volkswagen nilitembea umbali wa Kilomita 120 ilibaki Kilomita 60 nifike safari yangu, Bwana yule akaanza Kilomita kama 10 hivi akaja kunikata njiani Kilomita 60 sijamaliza kwa kweli kuna Watu wanatembea!!!!!......
Mie ningekanyaga engine ipasuke tu [emoji23][emoji23]
 
Nakumbuka kuna siku natoka Arusha kwenda Moshi mjini niko na BMW 5 Series.

Hicho kipande cha Arusha Moshi sipendi kuendesha bila kumkimbiza Prey (kwa tuliosoma Wildlfe Prey animal (mfano Swala) ni wanyama wanaoliwa na predator).

Nimeendesha mpaka maeneo ya KIA sijapata changamoto yoyote ya maana ya kufukuzana, Kuna mjinga wa Land cruiser Hardtop nilimprovoke tukimbizane akanitolea nje.

Nikawa naendesha mdogo mdogo kusubiria prey mwingine, eeh bana ikapita Gx 100 kibati.

Nikamwacha anipoteze kabisa asinione ili ajisifu. Nikatupia kitu kwenye sport mode.

170kph huyu hapa, jamaa anahangaika kucheki kwenye rear mirror, mbele kulikuwa na mteremko fulani, nikasema nikimpita hapa atasingizia mteremko.

Nikashuka naye kitu kinasoma 180, na jamaa alitegemea kwenye mteremko atachanganya zaidi aniache, akicheki niko nyuma yake, tukakamata tambarare, nikawasha indicator nataka kuchomoka.

Jamaa akapaniki zaidi akaniwashia indicator ya kushoto kuniruhusu nipite halafu huku anaendelea kukanyaga kibati kisiri siri 180kph.

Nikampita na lengo jamaa asione kabisa break light baada ya kilometa kadhaa nikasimama nikojoe nimsubirie jamaa apite nimfukuze tena.

Hahaha jamaa alisimama akaniambia kaka nimekubali mziki, naomba niangalie dash board hii mashine inasoma ngapi.

Siku nyingine gari ilifungwa spea pump flani nikasema wacha niende barabara ya ngaramtoni nikatest hiyo pump kama inapiga kazi vizuri.

Eeh bana natiririka na 170kph kurudi town, ghafla kwa mbele naona fuso linatolewa gereji linasukumwa barabarani liwake.

Wale jamaa waliokuwa wanasukuma walivyoona nakuja kwa moto mkali wakaacha gari wakakimbia kunusuru maisha yao.

Nilimwambia Mungu pokea roho yangu.

Usinitanie nikaingiza gari shambani. Nikala shamba la mahindi kama movie vile.

Nyingine natoka Arusha kwenda mto wa mbu mida ya saa 2 usiku. Nakimbia kumtafuta prey huko mbele mara Hilux double cabin yeboyebo hii hapa.

Kwa kweli jamaa alikuwa anafukia sio mchezo, nikasema huyu nisimpite nimchoshe hapo nyuma 170/180/190kph

Jamaa akawasha indicator anaingia kulia kama vile amefika. Nikasema huyu usikute amedhani majambazi ananikataa kijanja.

Kweli baada ya kukata kulia akasimama akawa ananisikilizia. Nikasepa zangu mdogo mdogo namuona anakuja nyuma yangu, nikimsubiria apite hapiti. Nikachimba zangu.
Duh eti unatafuta prey! Ugonjwa mbaya sana huo
 
Siku moja tunatoka mbeya harusini kurudi dar sie tuna crown royal salon 4gr-fse kipande cha kumaliza kitonga hapa kuishusha down fortuner hiyoo apo! Mbele kuna alteza...

Kuna kale kamchezo njia nzima mkiwa road za mikoani mnakutana mko watatu mnaongozana na hamtaki kuachana tukamkata fortuner na alteza hiyo tukaila..
Heee![emoji16] fortuner hajakubali katuacha tukamtuliza alteza maana yeye Ana 3sGE tukamwambia kiishara tulia ligi huwezi..

Jamaa wa fortuner tulinyoosha nae hadi msamvu maana yeye alikua anaenda dom tukaachana hapo lakini najua jamaa alikubali mziki.[emoji16]

Nyingine tulikuwa tunatoka msibani saa 8 ivi mchana tunaludi zetu dar tukiwa ndani ya lc j200... watu kama 6 hivi.Tupo katikati ya swanga na tunduma discovery 5 na range
Rover evoque zikatupita shwaaaaah! Wanao ijua barabara ilivyo saii from tunduma mpaka swanga wananielewa road inashawishi ukanyage! Dah tuliwatamani sema nikwavile tumetoka mazikoni tukaona isiwe tabu acha wapite
Tusije kuludisha msiba kwa mara nyingine..

Saa 10 tunafika uyole pale tumemaliza kula tunasepa wale jamaa kumbe nao walipitia mahali tunawaona hao tukavutiwa kuwafata sema tulikuwa na wamama kama wawili waoga aah! Tukawaacha waende tena alafu zile gari zilikuwa za ubalozi zimekula tinted tiiii! Ligi ni tamu bana![emoji16]
Haswa uwe na chuma yenye pulling.
 
Nyie ndio mnatufanya tufikishe 200+ maanake tukiishia 160 mkapita mnaona tumeshindwa!
Narudia maneno ya trafiki baada ya kunikamata..."huyu alikua spidi 170 mbugani...enhee ikamate na hio range rover ilikua spidi 160" aisee hio ilikua ligi kali sana siwezi hama Toyota aisee... 😂😂😂😂 sema range rover naikubali kwenye milima aisee jamaa aliikanyagia alinipita kama nimesimama vile...😂😂😂
 
Nakumbuka kuna siku natoka Arusha kwenda Moshi mjini niko na BMW 5 Series.

Hicho kipande cha Arusha Moshi sipendi kuendesha bila kumkimbiza Prey (kwa tuliosoma Wildlfe Prey animal (mfano Swala) ni wanyama wanaoliwa na predator).

Nimeendesha mpaka maeneo ya KIA sijapata changamoto yoyote ya maana ya kufukuzana, Kuna mjinga wa Land cruiser Hardtop nilimprovoke tukimbizane akanitolea nje.

Nikawa naendesha mdogo mdogo kusubiria prey mwingine, eeh bana ikapita Gx 100 kibati.

Nikamwacha anipoteze kabisa asinione ili ajisifu. Nikatupia kitu kwenye sport mode.

170kph huyu hapa, jamaa anahangaika kucheki kwenye rear mirror, mbele kulikuwa na mteremko fulani, nikasema nikimpita hapa atasingizia mteremko.

Nikashuka naye kitu kinasoma 180, na jamaa alitegemea kwenye mteremko atachanganya zaidi aniache, akicheki niko nyuma yake, tukakamata tambarare, nikawasha indicator nataka kuchomoka.

Jamaa akapaniki zaidi akaniwashia indicator ya kushoto kuniruhusu nipite halafu huku anaendelea kukanyaga kibati kisiri siri 180kph.

Nikampita na lengo jamaa asione kabisa break light baada ya kilometa kadhaa nikasimama nikojoe nimsubirie jamaa apite nimfukuze tena.

Hahaha jamaa alisimama akaniambia kaka nimekubali mziki, naomba niangalie dash board hii mashine inasoma ngapi.

Siku nyingine gari ilifungwa spea pump flani nikasema wacha niende barabara ya ngaramtoni nikatest hiyo pump kama inapiga kazi vizuri.

Eeh bana natiririka na 170kph kurudi town, ghafla kwa mbele naona fuso linatolewa gereji linasukumwa barabarani liwake.

Wale jamaa waliokuwa wanasukuma walivyoona nakuja kwa moto mkali wakaacha gari wakakimbia kunusuru maisha yao.

Nilimwambia Mungu pokea roho yangu.

Usinitanie nikaingiza gari shambani. Nikala shamba la mahindi kama movie vile.

Nyingine natoka Arusha kwenda mto wa mbu mida ya saa 2 usiku. Nakimbia kumtafuta prey huko mbele mara Hilux double cabin yeboyebo hii hapa.

Kwa kweli jamaa alikuwa anafukia sio mchezo, nikasema huyu nisimpite nimchoshe hapo nyuma 170/180/190kph

Jamaa akawasha indicator anaingia kulia kama vile amefika. Nikasema huyu usikute amedhani majambazi ananikataa kijanja.

Kweli baada ya kukata kulia akasimama akawa ananisikilizia. Nikasepa zangu mdogo mdogo namuona anakuja nyuma yangu, nikimsubiria apite hapiti. Nikachimba zangu.
Itabidi siku nikutafute kama bado hio 5 series upo nayo tuipimishe na GRS200 iliotolewa speed limit...😂😂😂😂
 
Siku moja nilikuwa najikongoja sehemu za mbarara uganda kuna barabara moja iko njema sana kuanglia dash board yangu niko 230 nyuma yangu ikaja chuma moja kuangalia ni Jaguar jamaa alipita kama upepo dk moja hata haikufika jamaa kaishapote
 
Back
Top Bottom