Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Siku moja nilikuwa najikongoja sehemu za mbarara uganda kuna barabara moja iko njema sana kuanglia dash board yangu niko 230 nyuma yangu ikaja chuma moja kuangalia ni Jaguar jamaa alipita kama upepo dk moja hata haikufika jamaa kaishapote
Ww ulikuwa na chuma gani mkuu?
 
Hiii wanayoiita mishangingi wakuu iacheni.
Tu siku nyingine tunatoka bagamoyo kuna ile sehemu pana roundabout tupo na crown nyeusi mbele mbele kidogo tumefika LC amazon hiyo nikasema huyu nanyooka nae mda huo ni saa 12 tochi zishaaanza kupungua nikamuacha atakuangulie kidogo..

Nikaanza sasa kukanyaga jamaa nilipo mfikia karibu nikampigia pasi kumuomba..
Tunyooshe mguu kidogo aka-respond...
Jamaa akawa kila akijitahidi wapi![emoji16] tukafika maeneo ya tegeta kuna kafoleni akatanua nikaungaa nikawasha hazad nae kawasha mwenge ndo tulikuja kuachana!

Yeye anaelekea ubungo mimi nanyoosha.
Nikiwa barabarani njia nyeupe namuona mtu kanipita alafu namuweza huwa sikubali[emoji16] lazima nipiane nae kidogo.
Watu pekee naowaheshimu ni watu wenye
Benz,Bmw,LC, na mjerumani yeyote.
 
Kuna siku naenda Manyara mida ya saa 4 usiku, nipo 170kph aisee nilikutana na kona kali haishi, nililala nayo tairi zinalalamika hatare.

Naimaliza nakutana na nyingine kushoto ina daraja, nimevuka daraja nikapaki gari pembeni siamini kilichotokea.

Wakati nashusha pumzi, Mwenyeji wangu akanipigia simu "ukifika maeneo flani kuna kona kali sana, kuwa makini". Ananijua mi ni mtu wa spidi kali

Bimmer - Germany Machine
Hii 5 series nilikuwa nayo E39 520i tu straight six, aisee nilikuwa nafanya kazi kama 80km kutoka ninapokaa, around 60km natumia Motorway. Kipindi niliinjoi gari ni hiki. Kila unavyokanyaga ndivyo inavyozidi kushika barabara. BMW ni Ultimate Driving Machine.
 
Watu mna underestimate sana diesel vehicles. Siku hizi diesel engines zinawasha moto vizuri tu.

200Kph kwa XC90 D5 ni kugusa tu
Kuna diesel zinakamua mpaka 400hp.

Si mchezo, kibongobongo wanaokutisha ni wachache sana bongo.
 
Kitu nachojilaumu ni kutokua na dash cam + rear view cam aisee ile ligi ilikua tamu sana range rover haina mbio kabisa
Kweli, inategemea range ipo hapo.. Kuna range zilizopoa sana, na Kuna range za moto hasaa
 
Mleta mada mimi naomba niulize kitu..hio GX100 uliifanyia modification na kuweka hio turbo? Maana JZX100 ndo ina 1JZGTE...nirudi kwenye point mimi speed kubwa ni 170KPH Altezza 3SGE sehemu mbili moja ukiwa unaitafuta kitonga baada ya kuimaliza iringa sehemu ya pili ni mikumi mbugani hii siku niliiacha Range Rover..ya 2014..na sehemu ingine ukishamaliza mikumi kutafuta vijiji vya mangae/mangai😀😀😀

Hiyo Range haikuamua tu kutengeneza ligi na wewe mkuu 😂😂😂
 
Hivi ukiendesha kwa "spidi kali sana" unapata faida gani?

Mimi nilijua wavuta bangi ndiyo hufanya hivyo, kumbe mpaka majitu mazima?
Kwan speed ndogo kuna faida gani? Speed kali ni ipi kwa uelewa wako....maana kuna nchi mfano Germany kuna njia ni free tembea vile unaweza kule ndo unakuta bike ya 1000cc 4cyl inaaibishwa ...tena bike ambayo 1st gear inaenda hadi 140 gia ya pili 200kph kule unaaibishwa japo kwa bongo bike ya hata cc 400 unasumbua gari nyingi sana
 
Itabidi siku nikutafute kama bado hio 5 series upo nayo tuipimishe na GRS200 iliotolewa speed limit...😂😂😂😂
Grs200 na 5 series ipi hapo ? Kuhusu balance vipi .. nazielewa sana grs 200 ila kuziweka kwenye mchakato na BMW 5 series kuitesa.. maana Kwa balance grs200 inaktwa na Lexus GS 450
 
Back
Top Bottom