Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Nakumbuka kuna siku natoka Arusha kwenda Moshi mjini niko na BMW 5 Series.

Hicho kipande cha Arusha Moshi sipendi kuendesha bila kumkimbiza Prey (kwa tuliosoma Wildlfe Prey animal (mfano Swala) ni wanyama wanaoliwa na predator).

Nimeendesha mpaka maeneo ya KIA sijapata changamoto yoyote ya maana ya kufukuzana, Kuna mjinga wa Land cruiser Hardtop nilimprovoke tukimbizane akanitolea nje.

Nikawa naendesha mdogo mdogo kusubiria prey mwingine, eeh bana ikapita Gx 100 kibati.

Nikamwacha anipoteze kabisa asinione ili ajisifu. Nikatupia kitu kwenye sport mode.

170kph huyu hapa, jamaa anahangaika kucheki kwenye rear mirror, mbele kulikuwa na mteremko fulani, nikasema nikimpita hapa atasingizia mteremko.

Nikashuka naye kitu kinasoma 180, na jamaa alitegemea kwenye mteremko atachanganya zaidi aniache, akicheki niko nyuma yake, tukakamata tambarare, nikawasha indicator nataka kuchomoka.

Jamaa akapaniki zaidi akaniwashia indicator ya kushoto kuniruhusu nipite halafu huku anaendelea kukanyaga kibati kisiri siri 180kph.

Nikampita na lengo jamaa asione kabisa break light baada ya kilometa kadhaa nikasimama nikojoe nimsubirie jamaa apite nimfukuze tena.

Hahaha jamaa alisimama akaniambia kaka nimekubali mziki, naomba niangalie dash board hii mashine inasoma ngapi.

Siku nyingine gari ilifungwa spea pump flani nikasema wacha niende barabara ya ngaramtoni nikatest hiyo pump kama inapiga kazi vizuri.

Eeh bana natiririka na 170kph kurudi town, ghafla kwa mbele naona fuso linatolewa gereji linasukumwa barabarani liwake.

Wale jamaa waliokuwa wanasukuma walivyoona nakuja kwa moto mkali wakaacha gari wakakimbia kunusuru maisha yao.

Nilimwambia Mungu pokea roho yangu.

Usinitanie nikaingiza gari shambani. Nikala shamba la mahindi kama movie vile.

Nyingine natoka Arusha kwenda mto wa mbu mida ya saa 2 usiku. Nakimbia kumtafuta prey huko mbele mara Hilux double cabin yeboyebo hii hapa.

Kwa kweli jamaa alikuwa anafukia sio mchezo, nikasema huyu nisimpite nimchoshe hapo nyuma 170/180/190kph

Jamaa akawasha indicator anaingia kulia kama vile amefika. Nikasema huyu usikute amedhani majambazi ananikataa kijanja.

Kweli baada ya kukata kulia akasimama akawa ananisikilizia. Nikasepa zangu mdogo mdogo namuona anakuja nyuma yangu, nikimsubiria apite hapiti. Nikachimba zangu.
[emoji23] hah huyu anapenda ligi
 
Kwanin mkuu hupendi speed?
Niliwahi kupata ajali kwenye spidi kali!
Ilinisababishia hali ya mshtuko gari inapokua spidi au breki zikifungwa ghafla.
Nmepona hiyo hali ya kushtuka ila nmejikuta spendi 'mabio'.
Ingawa kwenye mishe za kusaka ugali nalazimika kupiga 70-80 km/h kwa baadhi ya maeneo town.
Ila always mjini ni 25, na 45 kutegemea na speed limit husika.
"Nina familia inayonitegemea"
 
Niliwahi kupata ajali kwenye spidi kali!
Ilinisababishia hali ya mshtuko gari inapokua spidi au breki zikifungwa ghafla.
Nmepona hiyo hali ya kushtuka ila nmejikuta spendi 'mabio'.
Ingawa kwenye mishe za kusaka ugali nalazimika kupiga 70-80 km/h kwa baadhi ya maeneo town.
Ila always mjini ni 25, na 45 kutegemea na speed limit husika.
"Nina familia inayonitegemea"
Pole sana kiongozi...... wanasema ukishagongwa na nyoka hata siku ukiguswa na majani ni lazima utasktuka.
 
Back
Top Bottom