- Thread starter
-
- #81
Unaposema kifo hakiendeshwi kwa dhana, unajua hiyo ni dhana?
Kifo cha nani?
Unaelew kwamba si dhana zote ziko tofauti na uhakisia?
Unaelewa kwamba juna dhana zilizo mzizi wa uhalisia?
Nikikwambia jua litaonekana kuchomoza kesho, hiyo ni dhana au uhalisia?
Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua nilipokuuliza unajua nini maana ya dhana ,sababu niliona udhaifu juu ya tamko hili.
Tamko dhana kilugha ina maana moja ila kiistilahi ina maana kutokana na matumizi. Na maana ya kilugha ndio hua inakuwa pana zaidi.
Almuhimu dhana ni kutokuwa na uhakika wa jambo fulani,aidha kuwepo kwake,kutokea kwake,maana yake,uhalisia wake yaani kwa ufupi shaka.
Sasa unaposema kifo ni dhana ,itabiti utithibitishie ya kuwa kivipi kifo ni dhana. Kwa mtazamo wako kutokana na mtiririko hoja zako unakurubisha maana ya dhana kama wazo au kanuni fulani iliyojengeka kutokana na misingi fulani sasa uelewa huu si sahihi.
Mjengeko wa sentensi yako ya mwisho haujakaa sawa kwa mujibu wa sarufi ya au kanuni za sarufi ya kiswahili,sasa iweke vyema kisha nikupe maelezo yake.