Je, ni zipi faida na hasara za Diapers kwa watoto?

mkuu hiki ndicho ninachokiamini na mimi kuhusu pampasi.
Atavaa tu Kwenye matukio maalumu ambayo kubadilibadili nepi inakuwa kwazo.
Lkn Mkuu kaswali kameniijia, mbona wazungu wanavaa tu na bado wanajitambua kuliko sisi wasomeshwaji namba?
 

Mkuu, moto una madhara au hauna?

Gari lina madhara au halina?

Pombe je?

Chakula je?

Hewa unayoivuta ina madhara au haina?

Dunia ya leo mtu kuwa mhanga wa imani potofu ni suala la kujitakia tu.

Sioni kabisa uhusiano wa hizo nepi na uhanithi.

Kama upo, tuonyeshe/ tueleze kinagaubaga namna hizo nepi zinavyosababisha hiyo hali.
 
mkuu hiki ndicho ninachokiamini na mimi kuhusu pampasi.
Atavaa tu Kwenye matukio maalumu ambayo kubadilibadili nepi inakuwa kwazo.
Lkn Mkuu kaswali kameniijia, mbona wazungu wanavaa tu na bado wanajitambua kuliko sisi wasomeshwaji namba?

Na hao hao Wazungu wanazizidi nchi nyingi tu za Kiafrika kwa idadi ya watu!
 
Na hao hao Wazungu wanazizidi nchi nyingi tu za Kiafrika kwa idadi ya watu!
mkuu comment zako huwa zinafungua mipaka ya tanzania na kitutaka tuwe na uwanja mpana zaidi kifikiri.
tutofautishe ''myth'' na ''facts'' na '' Maoni au maamuzi au misimamo binasfi''
Mungu akubariki
 
Nyie wa kwenu wavalishe hayo madude! Mi wa kwangu HATATHUBUTU! Ni heri meoga aliyepona kuliko shujaa aliyekufa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Una uthibitisho gani kuwa pampers zina madhara kwa watoto? Kama Una scientific evidence basi share na Sisi ili tuweke kwenye mizani. Hakuna mzazi anayependa mwanawe aharibikiwe.
 
mkuu sio msimamo wangu huu, ni msimamo wa mshauri mtaani.
mawazo yako yatasaidia kutoa elimu ikiwa kunamaarifa ya zaida tutapeana.
 
Tatizo ni TBS ni butu au niseme dhaifu sana.i Vitu tunavyotumia vipo chini kabisa ya viwango na tuna TBS.

Tanzania hii hawabadiliki hao mpaka Rais aende akawatumbue.

Namuonea huruma sana yeyote anae kuwa Rais wa Tanzania.
 
Tatizo ni TBS uko butu.

Vitu tunavyotumia vipo chini kabisa ya viwango na tuna TBS.

Tanzania hii hawabadiliki hao mpaka Rais aende akawatumbue.

Namuonea huruma sana yeyote anae kuwa Rais wa Tanzania.
mkuu sio wewe tu Hata Nyerere aliwaonea huruma.
mchina anaweza kubana tabata matumbi akaanza kufyatua softkea pampas wakati kiwanda halisi kipo mfano.

Karibu kwa Maoni, Ikiwa ni product ambayo imethibitishwa na TBS yenye makali (assumption) bado tuziogope kwa sababu hizohizo?. Maana wengi sababu zao hazina uhusiano na TBS.
 
mkuu hiki ndicho ninachokiamini na mimi kuhusu pampasi.
Atavaa tu Kwenye matukio maalumu ambayo kubadilibadili nepi inakuwa kwazo.
Lkn Mkuu kaswali kameniijia, mbona wazungu wanavaa tu na bado wanajitambua kuliko sisi wasomeshwaji namba?
Kwa kuongelea kujitambua sina maana ya kuwa wataishia kutojitambua, bali namaanisha huenda wakachelewa badala ya kuhisi tofauti katika mwaka 1.8 anaweza akaanza kuhisi tofauti katika umri miaka 2.5 hadi 3. Nguo ya kawaida itamfanya ahisi kero kuwa na kinyesi au mikojo, hivyo ataanza mapema kuhisi hali inayopelekea kero hiyo na hivyo kutoa ishara/taarifa mapema. Lakini ukimvalisha Pampas sababu ya protection na comfortability hatahisi kero hivyo ataendelea tu kujikojolea na hivyo kuchelewa ku control urine kila inapokuja.
 
mkuu mimi na wewe katika hili tuko pamoja.
asante kwa maelezo shibishi.
 
Kwa kidogo ninachoelewa ni kuwa pampers zimetengenezwa kwa pamba + super absorbent materials zenye uwezo mkubwa Sana wa kuabsorb mkojo na kumuacha mtoto akiwa mkavu. Kwa maana nyingine, mtoto akijikojolea mara moja au mbili na asitokee mtu wa kumbadilisha hata kwa masaa mawili matatu, basi mtoto ataendelea kuwa mkavu. Madhara yanatofautiana kama frequency ya kumbadilisha haizingatiwi plus Hali ya hewa. Sehemu za joto kama Dar ni kweli pampers zinaweza zisiwe rafiki wa mtoto, hasa kama frequency ya kumbadilisha haizingatiwi. Kuna suala la brand pia, zipo zinazouzwa elfu 40 pieces 66 ( kwa Mbeya) na nyingine kwa idadi ya pieces hizo hizo zinauzwa 18,000 na difference yake utaiona kwenye matumizi. Mwisho, hata simu na laptop tunazotumia inasadikika zina madhara, ila kwa sasa hutosikia mtu anasema watoto wake hawatotumia electronic gadgets. TBS nao????
 

Magari kila siku yanapinduka na kugongana na kuua watu na wengine kuwaacha na vilema vya maisha!

Na kutwa kucha hakuna anayefungua mdomo na kusema magari yana madhara kwa maisha ya binadamu!
 
Watoto wangu wawili 8yrs na 3 yrs walivaa pampas tangu siku waliyozaliwa hadi wakatoka stage hiyo.
Sijawahi kuwa na nepi wala kununua nepi.
Mnaenda dunia gani jamani?
Mnaokataa pampas nawashauri hata pedi za dukani msitumie bali mtumie vitambaa.
Ebo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hata vitambaa wasitumie maana navyo vimetengenezwa viwandani huko.

Watumie majani ya miti na nyasi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…