- Thread starter
- #201
Asante sana ushauri wako nimeupokea kwa mikono miwiliPole sana kwa changamoto hiyo. Lakin siku zote binadamu tunapaswa kusimamia maamuzi yenye kutufanya tuwe na furaha na amani kwani ndo kila kitu kwenye maisha.
Unaweza ukatenga muda wa kuongea nae lakin akakuahidi atabadilika labda mkishaona. Swali je mmeshaoana na asibadilike what's next?
Kuna watu au watoto wanadhani kufanya hivyo au kujitoa kupitiliza ni kumfanya mzazi afurahi lakin kumbe sio hivyo.
Tunapaswa kujitoa kwa vitu vya msingi. Wazazi ni Mungu wetu wa pili tunapaswa kuwajibika kwao lakn si kwa utaratibu huo.
Nitakupa mfano nina rafiki angu mmoja alikuwa na mahusiano na jamaa yake. Yule bwana alikuwa haambiwi kitu kuhusu familia yake. Hata kama hana hela bora alale njaa lkn familia yake ile that's good hata rafiki angu aliapreciate hilo.Yule bwana alikuwa na dada ake alifariki akaacha watoto 2 wadogo yeye akabeba jukumu la kusomesha wakati huo kaka yake mkubwa alikuwa ameoa mwanamke aliyekuwa na watoto 3 kabla.
Yule bwana akawa anashauriwa sasa na best angu watoto walee kulingana na uwezo wako. Akawa anajibu ni kweli ili wajifunze. Aliwapeleka boarding wa kike alikuwa yuko darasa la saba .Watoto walienda shule wananunuliwa maji ya katoni Mazagazaga wakati bwana uwezo hana anaunga unga.Na alipokuja anakwama basi best angu kumfurahisha akawa anajitoa kukusupport jamaaa. Bado yule kaka ake mkubwa akikwama jamaa yake atoe support. Basi best angu akawa anamshauri kwa mwendo huu hutakuja kufanikiwa sababu hujifikirii hata wewe halafu pia unajitoa hata kwa vitu ambavyo sio vya msingi.
Kwani hiyo hela yenyewe ya kuwapeleka bording anakopa wakati hana uhakika wa kipato,,akamshauri hiyo bora uweke kwenye biashara japo kwa mwaka mmoja ukishapata uhakika ndo watoto uwapeleke bording jamaa akagoma. Basi bwana maisha Yao yakaenda binti kufika kidato Cha tatu kaacha shule kaenda kuishi kwa mwanaume.
Baada ya kila kitu kuharibika ndo akamwambia best asieee najua ningesikiliza ushauri wako. Best angu kuona mwanaume ambaye hashauriki aliamua kufanya maamuzi magumu .
Ushauri wangu; Simamia msimamo utaoona kwako unafaa kamwe usiishi kwa kumfurahisha mtu. Kama Leo anamsikiliza mama yake hivyo basi hata mkiingia kwenye ndoa bado ataendelea kufanya hivyo.
Japokuwa sheria haisemi kuwa mtoto anawajibu wa kumelea mzazi ila kutokana na tamaduni ni wajibu wetu kuwasaidia ila kwa mambo ya msingi.Hata kama ni bia basi isiwe kuendekeza.