Je, ninaweza kumtengua msimamizi wa mirathi?

Pole sana kwa changamoto mkuu.

Kuhusu kesi ya kumtengua msimamizi wa mirathi huwezi kutoboa maana kwa sasa msimamizi alishamaliza kazi yake kwa kufunga mirathi, hana anachokisimamia tena. Yaani sio msimamizi wa mirathi yoyote. Ulipaswa kuomba kumtengua kabla hajafunga mirathi, ungeweza kufanikiwa.

Halafu hata ungefanikiwa kumtengua msimamizi wa mirathi kwa sasa na kuomba mwingine ateuliwe (hata wewe mwenyewe) bado mahakama isingeweza kuruhusu hilo maana hakuna kitu cha kusimamia. Mali za marehemu zimeshauzwa, sasa utateuliwa ili kusimamia nini??

Kuhusu nyumba, hata ungefanikiwa kuthibitisha kuwa mirathi ilipatikana kidanganyifu, bado usingeweza kuirejesha kwa kuwa mnunuzi analindwa na sheria. Yaani ungeambiwa umdai fedha muuzaji ila nyumba isingerudi kwenu.

Kuhusu mgao wako, kwa kuwa ulikataa mwenyewe kupokea pesa, pia huwezi kuzidai sasa, labda kama zipo kwenye akaunti ya mahakama. Ila kama zilikuwa kwa aliyekua msimamizi wa mirathi nako itakuwa ngumu kuzidai.
Exactly
 
Na iwe hivyo.
Ni mpuuzi.
 
Naomba msaada kwenu Wabobezi wa Sheria, Tulifungua mirathi 2006 na kumchagua msimamizi wa mirathi.

Marehemu aliacha nyumba moja ambayo sisi warithi wote 6 tulikuwa tunaishi humo kasoro tu msimamizi wa mirathi alikuwa anaishi mbali, Lakini ugomvi wa mara Kwa mara kati yetu na kupelekana Polisi ulikuwa auishi na hatimaye Mimi nilimwita msimamizi wa mirathi aje, alipokuja tulikaa kikao kama ndugu, katika kikao hicho tulikuwa 4 tukakubaliana suluisho ni kuuza nyumba Ili Kila mmoja Apate haki yake aendelee na maisha yake.

Na wale 2 walipojulishwa wakaafiki nyumba kuuzwa, Mimi ni mtoto wa kiume nilipofikiri mara ya pili maamuzi tuliyofikia ya kuuza nyumba nikaamua kugeuka na kukataa. Msimamizi wa mirathi akaamua kwenda mahakamani na warithi wote tuliitwa, wenzangu 5 waliafiki kuuzwa nyumba ila Mimi pekee nilikataa na kutamka mahakamani kuwa ata wakiuza sitopokea hizo pesa. Mahakama ikakubaliana na warithi hao nyumba iuzwe.

Mimi nikazuia kuuzwa Kwa nyumba Kwani nilifungua kesi mahakamani kudai nyumba ni Mali yangu, kesi nikashindwa. Baadae nikafungua kesi nyingine kuwa Mirathi ni batili, nayo nikashindwa, na nikapewa muda wa kukata rufaa, sikukata rufaa ndani ya muda niliopewa.

Kwa kuwa sikukata rufaa na hakukuwa na kesi mahakamani, Msimamizi aliendelea na Zoezi akatangaza kuuzwa Kwa nyumba na ikauzwa kupitia Kwa mwanasheria mwaka 2014 nilikataa mgawo wangu na nikagomea kutoka katika nyumba, Kwa kuwa Mimi ni bouncer walikuwa wananiogopa kunigusa, hatimae msimamizi 2015 akarudi mahakamani kufunga usimamizi wa mirathi na tuliitwa wote na Mimi nilikataa pesa wananiona Mimi kama punguani.

Baada ya nyumba kuuzwa Nikarudi mahakamani kuomba kukata rufaa nje ya muda kuhusu kesi yangu ya Mirathi ni batili, mahakama ya wilaya nikashindwa, nikakata rufaa mahakama kuu Nako nikashindwa Mwaka 2020. Baada ya kushindwa mahakama kuu 2020 hiyo hiyo nikaenda Polisi kulalamika kuwa katika kile kikao cha mirathi 2006 mi sikuwepo na wameiga sahihi yangu. Polisi walifanya uchunguzi wao na wakamkata msimamizi na kumfungulia kesi ya forgery.

Lakini pia kesi imekwisha hivi majuzi na nimeshindwa. Na sasa nataka KUMTENGUA msimamizi wa mirathi, je imekaaje hii? Je, nitatoboa?
Hao warithi wenzio wakae kikao wakuue tu ili usiendelee kusumbua wenzio.

Watu kama nyinyi hamfai kabisa kuwa ndugu wa watu.
 
Niliposoma tu kichwa cha habari nikaingiwa na shauku ya kukusaidia Buree. Nilidhani ni Mtu unayeonewa. Sasa nilipoingia na kusoma kisa kamili, ndio nimechoka kabisa.
Kwa ufupi, una matatizo somewhere.

Na Hilo unalolitaka haliwezekani kwa mazingira hayo. In fact hizo Kesi ulipaswa kuamuriwa ulipe gharama.
 
Vigezo, moja, nimedai Msimamizi si ndugu yetu.
Pili, nimedai kuwa katika kikao Cha mirathi sikuwepo na walifoji sahihi yangu
Kwakuwa umekuja kuomba ushauri hapa JF,

Basi Fuata ushauri wa walio wengi wa hapa JF,

Lakini pia kesi imekwisha hivi majuzi na nimeshindwa. Na sasa nataka KUMTENGUA msimamizi wa mirathi, je imekaaje hii? Je, nitatoboa?
Huo ndio ukweli kuwa hutotoboa.
 
Naomba msaada kwenu Wabobezi wa Sheria, Tulifungua mirathi 2006 na kumchagua msimamizi wa mirathi.

Marehemu aliacha nyumba moja ambayo sisi warithi wote 6 tulikuwa tunaishi humo kasoro tu msimamizi wa mirathi alikuwa anaishi mbali, Lakini ugomvi wa mara Kwa mara kati yetu na kupelekana Polisi ulikuwa auishi na hatimaye Mimi nilimwita msimamizi wa mirathi aje, alipokuja tulikaa kikao kama ndugu, katika kikao hicho tulikuwa 4 tukakubaliana suluisho ni kuuza nyumba Ili Kila mmoja Apate haki yake aendelee na maisha yake.

Na wale 2 walipojulishwa wakaafiki nyumba kuuzwa, Mimi ni mtoto wa kiume nilipofikiri mara ya pili maamuzi tuliyofikia ya kuuza nyumba nikaamua kugeuka na kukataa. Msimamizi wa mirathi akaamua kwenda mahakamani na warithi wote tuliitwa, wenzangu 5 waliafiki kuuzwa nyumba ila Mimi pekee nilikataa na kutamka mahakamani kuwa ata wakiuza sitopokea hizo pesa. Mahakama ikakubaliana na warithi hao nyumba iuzwe.

Mimi nikazuia kuuzwa Kwa nyumba Kwani nilifungua kesi mahakamani kudai nyumba ni Mali yangu, kesi nikashindwa. Baadae nikafungua kesi nyingine kuwa Mirathi ni batili, nayo nikashindwa, na nikapewa muda wa kukata rufaa, sikukata rufaa ndani ya muda niliopewa.

Kwa kuwa sikukata rufaa na hakukuwa na kesi mahakamani, Msimamizi aliendelea na Zoezi akatangaza kuuzwa Kwa nyumba na ikauzwa kupitia Kwa mwanasheria mwaka 2014 nilikataa mgawo wangu na nikagomea kutoka katika nyumba, Kwa kuwa Mimi ni bouncer walikuwa wananiogopa kunigusa, hatimae msimamizi 2015 akarudi mahakamani kufunga usimamizi wa mirathi na tuliitwa wote na Mimi nilikataa pesa wananiona Mimi kama punguani.

Baada ya nyumba kuuzwa Nikarudi mahakamani kuomba kukata rufaa nje ya muda kuhusu kesi yangu ya Mirathi ni batili, mahakama ya wilaya nikashindwa, nikakata rufaa mahakama kuu Nako nikashindwa Mwaka 2020. Baada ya kushindwa mahakama kuu 2020 hiyo hiyo nikaenda Polisi kulalamika kuwa katika kile kikao cha mirathi 2006 mi sikuwepo na wameiga sahihi yangu. Polisi walifanya uchunguzi wao na wakamkata msimamizi na kumfungulia kesi ya forgery.

Lakini pia kesi imekwisha hivi majuzi na nimeshindwa. Na sasa nataka KUMTENGUA msimamizi wa mirathi, je imekaaje hii? Je, nitatoboa?
Wewe una Roho ya Uzurumati!
Nyie ndo mnasababisha Migogoro ya familia kila siku kwa roho zenu mbaya!

Yani unavyoandika utadhani unaandika jambo jembo kumbe ni Ubinafsi, Uchawi na Dhurma!
 
Kimsingi hapo kutoboa ni ngumu ingawa haujatuwekea bayana sababu za ligi ya kukataa kuuzwa kwa hiyo nyumba.

1. Msimamizi wa mirathi sio mwenye matakwa bali ni mtekelezaji wa maamuzi ya ninyi watoto 6. Kumbambikia kesi ya kufoji sahihi yako kiukweli ulimuonea sana sababu hakuuza hiyo nyumba kwa kutaka yeye bali ni maamuzi ambayo nyote mlishiriki kabla haujakengeuka.

2. Katika kugomea nyumba isiuzwe, ulikuja na hoja gani ambayo ina faida kwako kwanza na kwa ndugu zako wote. Inawezekana unagoma nyumba isiuzwe ila ndugu zako wanaona kabisa hakuna namna ya kuiendeleza ninyi kama wanafamilia.

3. Kushindwa kwako kesi katika hizi hatua zote ni matokeo ya kutokuwa na hoja za msingi, mahakama huwa hazimtupi mwenye haki hata iweje akikomaa kama wewe ulivyokomaa hivi. Bado hapa nitakuhoji, wewe ulitaka nyumba isiuzwe, ulikuja na alternative ipi kwa niaba ya wenzako 5 ili kuwepo na faida mara mbili au sawa sawa na kuuza.

Hebu tiwekee bayana shida ni nini kati yako na ndugu zako and why unamlaumu zaidi msimamizi wa mirathi ambaye kimsingi sio mwenye maamuzi ya mwisho ya kuuza mali hata kama alikuwa anakupuuza.
 
Nyumba ilishauzwa miaka 9 imepita. Mi nilikuwa nadhani ninahaki ya kumiliki iyo nyumba maana mi ni mtoto wa kwanza
Vikao na maamuzi ya kuuza vilijadiliwaje ukiwa kama mtoto wa kwanza si ulitakiwa kucoordinate kila kitu na wadogo zako, and how come madogo wanaamua vitu huku wewe kaka yao hauna moja wa mbili unalojua.
 
Back
Top Bottom