Je, ninaweza kumtengua msimamizi wa mirathi?

Je, ninaweza kumtengua msimamizi wa mirathi?

Naomba msaada kwenu Wabobezi wa Sheria, Tulifungua mirathi 2006 na kumchagua msimamizi wa mirathi.

Marehemu aliacha nyumba moja ambayo sisi warithi wote 6 tulikuwa tunaishi humo kasoro tu msimamizi wa mirathi alikuwa anaishi mbali, Lakini ugomvi wa mara Kwa mara kati yetu na kupelekana Polisi ulikuwa auishi na hatimaye Mimi nilimwita msimamizi wa mirathi aje, alipokuja tulikaa kikao kama ndugu, katika kikao hicho tulikuwa 4 tukakubaliana suluisho ni kuuza nyumba Ili Kila mmoja Apate haki yake aendelee na maisha yake.

Na wale 2 walipojulishwa wakaafiki nyumba kuuzwa, Mimi ni mtoto wa kiume nilipofikiri mara ya pili maamuzi tuliyofikia ya kuuza nyumba nikaamua kugeuka na kukataa. Msimamizi wa mirathi akaamua kwenda mahakamani na warithi wote tuliitwa, wenzangu 5 waliafiki kuuzwa nyumba ila Mimi pekee nilikataa na kutamka mahakamani kuwa ata wakiuza sitopokea hizo pesa. Mahakama ikakubaliana na warithi hao nyumba iuzwe.

Mimi nikazuia kuuzwa Kwa nyumba Kwani nilifungua kesi mahakamani kudai nyumba ni Mali yangu, kesi nikashindwa. Baadae nikafungua kesi nyingine kuwa Mirathi ni batili, nayo nikashindwa, na nikapewa muda wa kukata rufaa, sikukata rufaa ndani ya muda niliopewa.

Kwa kuwa sikukata rufaa na hakukuwa na kesi mahakamani, Msimamizi aliendelea na Zoezi akatangaza kuuzwa Kwa nyumba na ikauzwa kupitia Kwa mwanasheria mwaka 2014 nilikataa mgawo wangu na nikagomea kutoka katika nyumba, Kwa kuwa Mimi ni bouncer walikuwa wananiogopa kunigusa, hatimae msimamizi 2015 akarudi mahakamani kufunga usimamizi wa mirathi na tuliitwa wote na Mimi nilikataa pesa wananiona Mimi kama punguani.

Baada ya nyumba kuuzwa Nikarudi mahakamani kuomba kukata rufaa nje ya muda kuhusu kesi yangu ya Mirathi ni batili, mahakama ya wilaya nikashindwa, nikakata rufaa mahakama kuu Nako nikashindwa Mwaka 2020. Baada ya kushindwa mahakama kuu 2020 hiyo hiyo nikaenda Polisi kulalamika kuwa katika kile kikao cha mirathi 2006 mi sikuwepo na wameiga sahihi yangu. Polisi walifanya uchunguzi wao na wakamkata msimamizi na kumfungulia kesi ya forgery.

Lakini pia kesi imekwisha hivi majuzi na nimeshindwa. Na sasa nataka KUMTENGUA msimamizi wa mirathi, je imekaaje hii? Je, nitatoboa?
Umeandika upuuzi wa kutosha.
Umeshindwa kuficha uzwazwa wa mdai mirathi.

Kimsingi hata ukienda kushtaki mbinguni utashindwa.

Hiyo nyumba uliijenga wewe?
Una hati ya umiliki?
Wewe una haki gani zaidi ya warithi wengine?

Usituchoshe akili hapa
 
Vigezo, moja, nimedai Msimamizi si ndugu yetu.
Pili, nimedai kuwa katika kikao Cha mirathi sikuwepo na walifoji sahihi yangu
Wewe mbona swali la msingi unaloulizwa na kila mtu haulijibu?

Unaulizwa swali, KWANINI HAUTAKI NYUMBA IUZWE, WEWE UNAMPANGO GANI NA HIYO NYUMBA AMBAO UTAKUWA NA FAIDA KWAKO NA KWA NDUGU ZAKO?
 
Mtoto wa kwanza anaacga kutafuta mali zako ujisimamie unagombania mali za urithiii...!! Kenge maji... wadogo zako warithi nin sasa???
Hadi sasa hajasema sababu ya msingi, pengine anayosababu ya msingi ya kugomea nyumba ya familia kuuzwa labda alikuwa na mkakati ambao ungesaidia kila mwanafamilia ila shida sasa hasemi tatizo ni nini kuuzwa nyumba na alitaka ibakie kwaajiri ipi nadhani swala la kuhoji hapa ni wewe kama kaka wa familia unatoa maamuzi gani ya mwisho kwa faida ya wanafamilia wenzako na kwako pia.
 
Kinachokufanya ukatae kuuzwa kwa nyumba ni Nini mkuu?
The grounds for revoking the grant are listed under Section 49 (1) of Probate and Administration of Estates Act, Cap 352 R.E 20023which stipulates that the grant of probate and letters of administration may be revoked or annulled for any of the following reasons:"
(a) that the proceedings to obtain the grant were defective in substance;
(b) that the grant was obtained fraudulently by making a false suggestion, or by concealing from the court something material to the case;
(c) that the grant was obtained by means of an untrue allegation of a fact essential in point of law to justify the grant, though such the allegation was made in ignorance or inadvertently;
(d) that the grant has become useless and inoperative;
(e) that the person to whom the grant was made has wilfully and without reasonable cause omitted to exhibit an inventory or account in accordance with the provisions of Part XI or has exhibited under that Part an inventory or account which is untrue in a material respect."
 
Sasa Ngoja nikujibu swali lako na wapi ulipofanya makosa....

Kwenye Dunia ya Sasa nashangaa unassma "Nyumba ilikuwa ya kwangu" Hiki ni tatizo kubwa...

Sasa sikiliza Mwwnye matatizo makubwa ni Wewe na sio msimamizi..
Msimamizi anafata miongozo na ikiwa mojawapo ni kutoamua Kitu cha familia bila kuhusisha Wanafamilia...

Kwa Hadidu Rejea Ulikataa kuhudhuria vikao vyotr alivyoitisha (sasa hapa kosa ni la nani?)
Kwa sheria wakitimia asilimia 75 ya wahusika kikao ni halali kama wenzako wote walikuwepo na wewe hukuwepo kikao kilikuwa halali na maamuzi yalikuwa halali...

Na ndio maana umeshindwa kesi zote kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka mahakama kuu!

Kiufupi malalamiko yako hayana mashiko wala hayana Umaana kwa sasa...
Ingekuwa kama ungefanya hivyo mwka 2006 ukapinga uteuzi wake pengine ungekuwa sawa....

Naweza nikajenga picha moja hivi...

Mwaka 2006 ulikuwa na Pesa za kutosha na ulikuwa na kibuli sana kwa wenzako ulijiona wewe ni bora kuliko wengine,Hata walipokuambia tunauza nyumba uliwaambia iuzeni tu kwa jeuri yako ya fedha.....

Sasa fedha zimekata unaanza kujutia kwa sababu huna sehemu ya kukaa na pesa ya kodi imekuwa ngumu....
Sasa unatafuta mtu wa kumpa Lawama kwa makosa yako uliyofanya miaka kumi saba iliyopita...
Hakuna Rufaa unaweza kukata ambayo ni ys miaka 17 ambayo sio jinai eti kwa ajili ya madai
Msimamizi alikuwa ni mtu wangu wa karibu na Mimi ndie niliyemuita aje asuluishe mgogoro wetu, na siku ya kikao Cha usuluishi tukaamua tuuze nyumba, katika kikao hicho tulikuwa 4 na hatukuandika popote, Kwa iyo baada ya siku chache kupita Mimi nilihitaji msimamizi anipatie hati ya nyumba lakini hakunipa na ndipo nikamwambia Mimi sipo katika mpango wa kuuza nyumba nimejitoa. Hapo ndipo Msimamizi akaona aende mahakamani kutuita warithi wote na Mimi niliitikia Wito wa mahakama na mahakamani warithi wote waliafiki kuuzwa nyumba isipokuwa Mimi pekee nilikataa.
 
The grounds for revoking the grant are listed under Section 49 (1) of Probate and Administration of Estates Act, Cap 352 R.E 20023which stipulates that the grant of probate and letters of administration may be revoked or annulled for any of the following reasons:"
(a) that the proceedings to obtain the grant were defective in substance;
(b) that the grant was obtained fraudulently by making a false suggestion, or by concealing from the court something material to the case;
(c) that the grant was obtained by means of an untrue allegation of a fact essential in point of law to justify the grant, though such the allegation was made in ignorance or inadvertently;
(d) that the grant has become useless and inoperative;
(e) that the person to whom the grant was made has wilfully and without reasonable cause omitted to exhibit an inventory or account in accordance with the provisions of Part XI or has exhibited under that Part an inventory or account which is untrue in a material respect."
Mkuu tafsiri hapa inahitajika lugha ya kisheria hiyo
 
Msimamizi alikuwa ni mtu wangu wa karibu na Mimi ndie niliyemuita aje asuluishe mgogoro wetu, na siku ya kikao Cha usuluishi tukaamua tuuze nyumba, katika kikao hicho tulikuwa 4 na hatukuandika popote, Kwa iyo baada ya siku chache kupita Mimi nilihitaji msimamizi anipatie hati ya nyumba lakini hakunipa na ndipo nikamwambia Mimi sipo katika mpango wa kuuza nyumba nimejitoa. Hapo ndipo Msimamizi akaona aende mahakamani kutuita warithi wote na Mimi niliitikia Wito wa mahakama na mahakamani warithi wote waliafiki kuuzwa nyumba isipokuwa Mimi pekee nilikataa.
Sijajua unachangamoto gani ila kwa haraka haraka unashida sana juu ya eneo la uelewa au ufahamu wa mambo.

Huyo msimamizi wa mirathi wewe si ndie ulimleta why sasa aende against na wewe halafu ashikamane na ndugu zako huoni kuwa wewe ni shida hapo?

Umekubaliana wewe mwenyewe kwa ridhaa yako kuwa huyo jamaa yako wa karibu ashike nafasi ya kusimamia mirathi halafu unataka akatie hati ya nyumba, hivi upo sawa sawa kichwani?

Akikupatia hati ya nyumba halafu jambo lolote likatokea kama kupoteza hiyo hati, kuharibika, au nyumba ikachukuliwa mkopo benki bila yeye kujua au ndugu zako ni yeye kwa mujibu wa sheria anatakiwa kudaiwa sio wewe, so kukukatalia si kwasababu ametaka bali ni utaratibu.

Muwe mnajipa nafasi ya kupata elimu kwanza ya vitu kabla hamjaanza kulamu watu.
 
Msimamizi alikuwa ni mtu wangu wa karibu na Mimi ndie niliyemuita aje asuluishe mgogoro wetu, na siku ya kikao Cha usuluishi tukaamua tuuze nyumba, katika kikao hicho tulikuwa 4 na hatukuandika popote, Kwa iyo baada ya siku chache kupita Mimi nilihitaji msimamizi anipatie hati ya nyumba lakini hakunipa na ndipo nikamwambia Mimi sipo katika mpango wa kuuza nyumba nimejitoa. Hapo ndipo Msimamizi akaona aende mahakamani kutuita warithi wote na Mimi niliitikia Wito wa mahakama na mahakamani warithi wote waliafiki kuuzwa nyumba isipokuwa Mimi pekee nilikataa.
Mkuu mbona unajichanganya mwenyewe....
No wonder Mahakamani unashindwa..
Mwanzozni unasema mlikubaliana wote kuwa muuze nyumba...

Mlivokubaliana Nini kilikufanya wewe uombe tena hati ya nyumba?
Msimamizi anachukua makubaliano yoyote yanayowekwa na familia na kuyafanyia kazi!..

Unajua aina za contract (Makubaliano) sio lazima iwe kwenye maandishi hata makubaliano ya Maongezi kama Sehemu zote zikikubaliana huwa ni Legally Binded..

Kwahyo unaposema Wewe hukukubaki nyumba iuzwe Huoni kama unajichangnya ulishakubali nyumba iuzwe mwanzoni na wote mkakubaliana..

sasa msimamizi ana kosa gani?
 
Swali la msingi haujibu, tunakuuliza hapa, kwann uligomea nyumba kuuzwa, wewe ulikuwa na mipango nayo gani ambayo ndugu zako wameshindwa kukuelewa wakagomea? [emoji848]
2 soma
Alifungua kesi na kudai nyumba n yake aisee wamekusitiri ndugu wangeanza na wewe hapa hata usingekujahuku
 
Acha kusumbua wenzio,kesho ni kubwa kuliko jana na leo.
Nashangaa hivi alitaka wenzake wasipate urithi wao na yeye aendelee kuishi kwenye nyumba?

Kwa nini asingeinunua mambo yakaisha?

Huko ni kuhangaishana tu na roho mbaya aliyonayo. Achukuwe hizo pesa za urithi wake asonge mbele au akizikataa zipelekwe wakfu zifanye mambo mengine.

Atakuja kujuta umri umeshapita. Kuna siku atakuja kuondolewa na polisi bila huruma.
 
Back
Top Bottom