Je, ninaweza kumtengua msimamizi wa mirathi?

Exactly
 
Na iwe hivyo.
Ni mpuuzi.
 
Hao warithi wenzio wakae kikao wakuue tu ili usiendelee kusumbua wenzio.

Watu kama nyinyi hamfai kabisa kuwa ndugu wa watu.
 
Niliposoma tu kichwa cha habari nikaingiwa na shauku ya kukusaidia Buree. Nilidhani ni Mtu unayeonewa. Sasa nilipoingia na kusoma kisa kamili, ndio nimechoka kabisa.
Kwa ufupi, una matatizo somewhere.

Na Hilo unalolitaka haliwezekani kwa mazingira hayo. In fact hizo Kesi ulipaswa kuamuriwa ulipe gharama.
 
Ukweli seriously!! Katika mahakama mara zote msimamizi amekuwa anatoa Rai Kwa mahakimu kuwa eti Mimi nikapimwe akili, lakini hakimu anasema mahakama inamsikiliza yeyote (si utani ni kweli kabisa)
Wewe kwanini hutaki nyumba iuzwe? Unataka mfanyeje na hiyo nyumba? Una plan yoyote inayoeleweka?
 
Vigezo, moja, nimedai Msimamizi si ndugu yetu.
Pili, nimedai kuwa katika kikao Cha mirathi sikuwepo na walifoji sahihi yangu
Kwakuwa umekuja kuomba ushauri hapa JF,

Basi Fuata ushauri wa walio wengi wa hapa JF,

Lakini pia kesi imekwisha hivi majuzi na nimeshindwa. Na sasa nataka KUMTENGUA msimamizi wa mirathi, je imekaaje hii? Je, nitatoboa?
Huo ndio ukweli kuwa hutotoboa.
 
Wewe una Roho ya Uzurumati!
Nyie ndo mnasababisha Migogoro ya familia kila siku kwa roho zenu mbaya!

Yani unavyoandika utadhani unaandika jambo jembo kumbe ni Ubinafsi, Uchawi na Dhurma!
 
Kimsingi hapo kutoboa ni ngumu ingawa haujatuwekea bayana sababu za ligi ya kukataa kuuzwa kwa hiyo nyumba.

1. Msimamizi wa mirathi sio mwenye matakwa bali ni mtekelezaji wa maamuzi ya ninyi watoto 6. Kumbambikia kesi ya kufoji sahihi yako kiukweli ulimuonea sana sababu hakuuza hiyo nyumba kwa kutaka yeye bali ni maamuzi ambayo nyote mlishiriki kabla haujakengeuka.

2. Katika kugomea nyumba isiuzwe, ulikuja na hoja gani ambayo ina faida kwako kwanza na kwa ndugu zako wote. Inawezekana unagoma nyumba isiuzwe ila ndugu zako wanaona kabisa hakuna namna ya kuiendeleza ninyi kama wanafamilia.

3. Kushindwa kwako kesi katika hizi hatua zote ni matokeo ya kutokuwa na hoja za msingi, mahakama huwa hazimtupi mwenye haki hata iweje akikomaa kama wewe ulivyokomaa hivi. Bado hapa nitakuhoji, wewe ulitaka nyumba isiuzwe, ulikuja na alternative ipi kwa niaba ya wenzako 5 ili kuwepo na faida mara mbili au sawa sawa na kuuza.

Hebu tiwekee bayana shida ni nini kati yako na ndugu zako and why unamlaumu zaidi msimamizi wa mirathi ambaye kimsingi sio mwenye maamuzi ya mwisho ya kuuza mali hata kama alikuwa anakupuuza.
 
Nyumba ilishauzwa miaka 9 imepita. Mi nilikuwa nadhani ninahaki ya kumiliki iyo nyumba maana mi ni mtoto wa kwanza
Vikao na maamuzi ya kuuza vilijadiliwaje ukiwa kama mtoto wa kwanza si ulitakiwa kucoordinate kila kitu na wadogo zako, and how come madogo wanaamua vitu huku wewe kaka yao hauna moja wa mbili unalojua.
 
Vikao na maamuzi ya kuuza vilijadiliwaje ukiwa kama mtoto wa kwanza si ulitakiwa kucoordinate kila kitu na wadogo zako, and how come madogo wanaamua vitu huku wewe kaka yao hauna moja wa mbili unalojua.
Hajitambuii huyooo.. Mtoto wa kwanza kikao cha mirathi haupo alikuwa kuvutaa bhangii sijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…