Je, ninaweza kumtengua msimamizi wa mirathi?

Milembe inakuhusu
 
Watu wa aina hii huwa ni wakorofi na wala hawana sababu za msingi bali wanataka wenzao wasipate haki yao.

Huyu yupo kama kaka yetu sisi, alijirithisha mali zote, akauza nyumba moja kati ya mbili alizojenga baba yetu na moja akawa anaishi yeye. Kila tukimuambia habari ya mirathi alikuwa anatukana watu. Baada ya kifo ndiyo tulitambua kumbe alimwambia mwanawe kuwa ile nyumba sio yake bali ni ya ndugu zake (sisi).
 
Kwenye hiyo nyumba umeshaondoka au bado umeng'ang'ania kwasababu we ni baunsa? Alafu We tangu 2006 hadi leo imepita miaka 17 bado unapambana na migogoro ya urithi tu au ndo umeshaamua maisha yako yote yaliyobaki kazi yako iwe ni kufungua kesi na kushindwa?
 
Na huenda yeye ndiye aliyekuwa akiongoza mgomo wa kwenda shule,kujishughurisha badala yake akawa anaenda kwenye vijiwe vya kuvutia bangi na kutanua kifua eti ili awe baunsa akitegemea vya urithi.
 
Mkuu hii case kwa ninavyoiona imeshatoka kwenye probate..

Hapa nahisi tuizungumie kwenye Contract Breach..

Mlalamikaji anamtuhumu Msimamizi wa mirathi kwa Statute of Frauds wakati yeye mwenyew alikuwepo kwenye kikao na aliridhia na yeye ndo alipresent hiyo mada...

Japo angeweza Kubebwa legally na kipengele cha doctrine of promissory estoppel japo yeye mwenyewe alichelewa mpaka upande mmoja ukaanza kufanya process so hata kama angeshinda Kipindi cha mwaka Nyumba inauzwa ilipaswa alipe promisory Demage of contract..

Kama wangeweka kikao mapema wangekuabliana na ndugu zake kwanza kabla ya kumuhusisha Msimamizi na wangekuwa bora..
Ila hapa atakuwa anapiga kelele tu maana yeye ndo kasababisha demage
 
Vigezo, moja, nimedai Msimamizi si ndugu yetu.
Pili, nimedai kuwa katika kikao Cha mirathi sikuwepo na walifoji sahihi yangu
Mkuu Hoja zako na mapingamizi yako hayana mashiko kabisa..

KWa mujibu wa Sheria tulizo adapt za mirathi..
Msimamizi sio lazma awe ndugu wa karibu..
Tena ni vizuri kwa sababu hakuwa ndugu kwahyo hana Interest kwenye hiyo mirathi (Na hicho ndo kinambeba kuonekana katenda haki)
 
Niling'ang'ania na kupangisha watu na Kodi nilikuwa napata hadi 2019 nikatolewa Kwa amri ya mahakama, msimamizi aliomba mahakama nikatolewa na nyumba akakabidhiwa mnunuzi na akaibomoa.
 
Kwani mkuu wewe unataka nini hasa maana kote umeshindwa, nyumba ishauzwa sasa shida yako nini hasa? Unapoteza muda na kujenga uadui baina yenu na unapoteza ela pia.
 
Anza kufuatilia mgawo wa kuuzwa nyumba ya wazazi wenu(pesa haipo) waliohangaika sanaa kuijenga wakati wewe unajifunza kula ndumu na sasa umekuwa mbobezi.

Nunua kiwanja chako kwa pesa yako kisha jenga,kenge wewe.
 
hutoboi, hauna hoja
 
Kiufupi ukiona mpaka mawazo yako kama kaka mkubwa wa familia yanapuuzwa jua una changamoto kubwa mahaliii... huyu alikuwa anaishi kwenye nyumba ya urithi na wadogo zake kama ndo nyumba pekee walikuwa wanaishi sidhani kama wangeuzaa ila kuna kitu jamaa hasemii...!!
 
Na huenda yeye ndiye aliyekuwa akiongoza mgomo wa kwenda shule,kujishughurisha badala yake akawa anaenda kwenye vijiwe vya kuvutia bangi na kutanua kifua eti ili awe baunsa akitegemea vya urithi.
Wakati huo nyumba ilipangwa kuuzwa kutokana na migogoro isiyoisha wakaamua wauze wagawane. Mleta migogoro alikuwa ni huyu baunsa. Ukiona ndugu ameanza kubeba vyuma huku ni jobless ujue kuna hatari, kadri mwili unavyotanuka ndivyo utahahira unajaa kichwani.

Jambo lingine. Tumpe sifa msimamizi wa mirathi, ni mtu mwaminifu sana na mwenye hekima.
 
Hakika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…