Gentleman,
kwani diplomasia ya Marekani ni ya lini ikiwa ya Tanzania ni ya miaka ya 1970? kwamba diplomasia ya Tanzania ni old kuliko ya Marekani ya miaka ya 1800?
kwahiyo gentleman,
DRC inapata changamoto fulani katika uchumi wake kwasababu ya vikwazo alivyowekewa Joseph Kabila specifically? halafu, kwani kawekewa hivyo vikwazo lini pamoja na huo mfumo wake unaeleza?

Benki gani hiyo ya marekani iliacha kufanya biashara na DRC na lini lilitokea hilo?
Licha ya changamoto za kiusalama zisizo koma, ni lini uchumi wa DRC ulikwama gentleman?
Ni vizuri kuwapa wasio elewa mambo haya ufahamu wa na uelewa wa kweli kuhusu vikwazo.
Ikiwa vikwazo hivyo ni kwa mtu binafsi, athari zinamuhusu yeye na mali zake tu,
Na ikiwa vikwazo hivyo vimelenga makampuni fulani ya kibaishara, athari za kiuchumi sasa zinanza kupanda kuanzia kwenye kampuni yenyewe, waajiriwa na nchi kwa kiasia fulani kukosa ilichokua inapata kutoka kwenye kampuni hiyo,
Ikiwa sasa vikwazo vinailenga serikali ya taifa fulani kwa ujumla wake, basi hapo athari zinaongezeka ukubwa zaidi na kupiga hadi tosi za wananchi wake kwa ujumla.
DRC inaendelea kua taifa linalofanya vizuri sana kiuchumi katika eneo la maziwa makuu na hakuna athari za zozote za kiuchumi inazopata baada ya Joseh Kabila kuwekewa vikwazo na Marekani. Anainjoy maisha bila mbambamba yoyote Belgium.
Kwenye suala la mikopo naona bado huelezi ukweli, ila wafuata mkumbo wanakuelewa mno

hakuna mtu au taifa linaweza kumkopesha maskini ambae anaonekana kabisa hana vigezo wala uwezo wa kulipa deni la anachotaka kukopa. Uwezo wa taifa kukopa ndio uwezo wa kiuchumi wa taifa hilo.
Mkopo ni mkopo tu, haijalishi umetoka wapi ila wewe unadeal na anae kopesha, ndio maana nimeeleza hapo juu kwa gentleman, unaeleza tuvitu tudogotudogo sana ambavyo hata darasani Lecture hawezi kukufundisha bali utavikuta stationary kwenye hardcopy ukajisomee mwenyewe. Hata hilo sijui la veto ni kitu cha huko chini kabisa na hakituhusu kama Tanzania hata kidogo.
Mwisho kabisa,
Falsafa ya kutokufungana na upande wowote wa dunia kama msingi wa sera ya mambo ya nje ya Tanzania, ndio inatufanya Tanzania kua taifa ambalo halitishishiki wala kutikiswa na vitisho vya upande wowote ule wa dunia kuhusu mambo yake ya ndani kiuchumi, kisiasa au kijamii. Na ndio maana serikali sikivu ya CCM chini ya Dr SAMIA SULUHU HASSAN, ikipata formal and detailed information kutoka serikali ya Marekani, itachukua hatua muafaka ya makusudi sana na kuhakikisha songombingo hii inayopotoshwa na kutiwa chumvi na wafuata mkumbo inakua solved katika meza ya mazungumzo peaceful kwa maslahi mapana ya wanachi wa nchi hizi mbili zenye mahusiano ya kihistoria ya muda mrefu sana. hicho ambacho wafuata mkumbo wanapotoshana ni ndoto za mchana tu,
Naamini,
licha ya kua confused na hali ya mambo mashariki ya kati rais Donald Trump hawezi kushawishika kabisa na porojo nonsense za seneta TED Cruz alizopenyezewa na kupotoshwa kirahisi kabisa na wafuata mkumbo kuihusu Tanzania
Comrade!
Pumzika Kunywa Chai na kahawa kwanza nahisi kama unazidi kujichanganya.!

na hapo ndio ninapojiuliza
Unasoma ili kujibu na kushinda ubishi, au unasoma ili kuelewa uhalisia wa mambo ulivyo kwa sasa?
Umeandika maelezo marefu, lakini umejichanganya kwenye mambo ya msingi sana ya kiuchumi na kihistoria. Ngoja nikufungue macho kwenye maeneo uliyopotoka:
Kuhusu Mimi kusema wewe unatumia Diplomasia ya Miaka ya 1970 Niliposema unazungumzia diplomasia ya miaka ya 1970, sikuwa namaanisha umri wa nchi ya Marekani.
Nilimaanisha unatumia fikra za kipindi cha
Cold War (Vita Baridi) ambapo nchi masikini zilikuwa zinajificha kwenye kivuli cha
"Neutrality/Non-Aligned Movement" na kufikiri haziwezi kuguswa. Dunia ya sasa ya 2026 inaendeshwa na
Economic Interdependence (Utegemezi wa Kiuchumi). Hakuna nchi inayojifungia ndani ikasema haitishiki na mifumo ya kimataifa.
Pili umeuliza kuhusu DRC,vikwazo na benki haya sikiliza,Umeuliza ni benki gani iliyoacha kufanya biashara na DRC na lini uchumi wao ulikwama? Twende kwenye ripoti za kifedha:
- Kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, Marekani ilipoweka vikwazo kwa watu wa karibu wa Kabila na mfanyabiashara Dan Gertler, benki kubwa za kimataifa kama Deutsche Bank, Citibank, na Barclays zilisitisha kutoa huduma za clearing za sarafu ya Dola (USD clearing) kwa benki za DRC kwa hofu ya kupigwa faini na Wizara ya Fedha ya Marekani (OFAC). Jambo hili kitaalamu tunaita De-risking.(najaribu kukuonyesha maneno ili ukayasome na kuyaelewa)
- kingine nimeshangaa umesema DRC ipo vizuri kiuchumi Hiyo DRC unayosema inaendelea vizuri, ripoti za IMF na Benki ya Dunia zinaonyesha ina viwango vya juu zaidi vya mfumuko wa bei (inflation), na sarafu yao (Congolese Franc) imepoteza thamani kwa kiasi kikubwa sana. Kabila anaweza akawa anaponda raha Ubelgiji kwa mabilioni aliyojilundikia, lakini wananchi wa DRC ndio wanaoteseka na mfumo mbovu wa kiuchumi uliosababishwa na nchi yao kutengwa. Vikwazo vya mtu binafsi vilivyowekwa viongozi wa serikali huwa vinazuia Foreign Direct Investment (FDI) kutoka mataifa makubwa kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayetaka kuweka pesa kwenye nchi yenye migogoro ya vikwazo. Pengine hii elimu inapaswa uijue au ukaisome na ukajue Vikwazo vya vioungozi huzuia Foreign Direct Investment (FDI)
Kuna vitu nahisi Elimu yako sio kubwa sana kuvijua kwahyo nisamehe kwa kuongea vitu vikubwa vilivyokuzidi samahani sana,, yaani Mkuu, hivi kweli unaita kura ya turufu (Veto Power) ya Marekani ndani ya Benki ya Dunia na IMF kuwa ni
"tuvitu twa chini kabisa" visivyotuhusu? Hapa ndio unathibitisha kuwa husomi kuelewa.
Tanzania tunapata mikopo kupitia dirisha la
IDA. Hili dirisha halikopeshi kibiashara; linatoa mikopo ya hisani (Concessional loans) kwa nchi masikini kwa kutumia pesa za ruzuku zinazochangwa na mataifa tajiri. Marekani ndio mchangiaji mkubwa zaidi wa fedha hizo. Kusema jambo hili halituhusu wakati tunajenga reli, barabara, na shule kwa fedha hizo za IDA ni kujidanganya mchana kweupe. Huwezi kwenda kukopa kwenye taasisi ambayo mdhamini mkuu amekuwekea vikwazo.
narudia Tena kukufundisha kuhusu Mikopo..
maana kwenye hoja yako ya mikopo, umeandika vitu ambavyo kiuchumi vinaonyesha unachanganya kati ya
"Mkopo wa Biashara" (Commercial Loan) na
"Mkopo wa Maendeleo/Msaada" (Concessional Loan). Ngoja nikupe mfano rahisi sana wa maisha ya kawaida ili uelewe kwanini hiyo unayoita "mambo ya stationary" ndiyo inayoendesha bajeti ya Tanzania:..
- Mkopo wa Biashara (Msimamo wako): Ukweli ni kwamba, ukienda benki ya biashara (kama CRDB au NMB) kukopa shilingi milioni 500 kujenga nyumba, watakuomba dhamana (hati ya nyumba/kiwanja) na watakuwekea riba kubwa ya 14% hadi 18% kwa sababu wanajua una biashara inayozalisha. Hapo ndipo unakuwa na haki ya kusema "mimi nina uwezo wa kulipa ndio maana wamenikopesha."
- Mkopo wa Hisani/Maendeleo (Uhalisia wa Tanzania mikopo tulionayo): ikitokea huna biashara kubwa, unaenda kuomba mkopo kwa tajiri wa ukoo wenu akujengee nyumba ya kuishi, akakuambia "Nenda kachukue milioni 500, utanirudishia baada ya miaka 40, na riba ni 0.5% tu." Mkuu, hapo tajiri hakukopesha kwa sababu una biashara au vigezo vya kibiashara; amekukopesha kwa sababu ya uhusiano wenu mzuri na hisani. Ukimtukana huyo tajiri na kumwambia "huna uwezo wa kunipangia maisha yangu," akasitisha huo mkopo, hutaweza kwenda kukopa benki ya biashara kwa masharti yale yale nafuu.
Tanzania haikopi fedha za kujenga reli (SGR), barabara, au miradi ya maji ya vijijini kwenye masoko ya biashara ya kimataifa yenye riba kubwa (kama Eurobonds) kwa kiwango kikubwa kwa sababu hatuna uwezo huo wa kulipa riba kubwa.Sisi tunakopa kupitia dirisha la
IDA (International Development Association) la Benki ya Dunia.
- Huu ni mkopo wenye riba ya chini ya 1% na muda wa kulipa ni hadi miaka 30 hadi 40.
- Hizo pesa za IDA unajua zinatoka wapi? Hazitokani na faida ya Benki ya Dunia; ni ruzuku na misaada (donations) inayochangwa na nchi tajiri ili kuzisaidia nchi masikini na zinazoendelea.
- Marekani ndiye mchangiaji mkubwa zaidi (Largest Contributor) wa fedha hizo za IDA zinazokuja kutujengea shule na zahanati huku kwetu.
Sasa unaposema
"Suala la Veto ya Marekani ni la chini kabisa halituhusu," unaonyesha jinsi usivyojua mfumo wa kifedha duniani unavyofanya kazi. Ndani ya Benki ya Dunia, nguvu ya kura (Voting Power) inategemea kiasi cha fedha nchi inachochangia. Marekani ana takriban
15.5% ya kura zote. Sheria za Benki ya Dunia zinasema maamuzi makubwa yanahitaji
85% ya kura. Hii ina maana kwamba Marekani peke yake akisema
HAPANA, hakuna mkopo au msaada wowote unaweza kupitishwa na Benki ya Dunia kwenda nchi yoyote. Hiyo ndiyo inaitwa
Veto Power.
Nimecheka sana na Inaonyesha Hujui hata mifumo ya Kisenate na kibunge Ya marekani inafanyaje kazi..
basi atleast kasome hata ya Kenya inakaribiana na marekani.
Eti unasema kuwa Rais Donald Trump hawezi kushawishiwa na Seneta Ted Cruz. Unasahau kuwa mifumo ya sera ya mambo ya nje ya Marekani haiendeshwi kwa mihemko ya mtu mmoja. Seneta Cruz akipeleka mswada (bill) Senate na ukapitishwa kuwa sheria, Rais wa Marekani analazimika kuutekeleza kisheria, iwe anataka au hataki.
comrade itoshe kusema tunahitaji kusoma sana, Kuhusu Mada tunazochangia kabla ya kuingia kwenye Hoja..
Mimi ni CCM damu kabisa na ni Kada mzuri tu ila kwenye swala la kushupaza shingo kwenye hili swala nakataa ,kwa sababu najua Hasara zake