Je, nini kifanyike ili kama Taifa tutoke kwenye mkwamo wa kidiplomasia duniani?

Je, nini kifanyike ili kama Taifa tutoke kwenye mkwamo wa kidiplomasia duniani?

Huna akili.Sisi hatuna hiyo nguvu ya kujiamulia mambo.Sisi ni kanchi kadogo tu na masikini hatuwezi kupanga hata bei za bidhaa zinazouzwa soko la dunia.
mwenye akili tuliza mihemko useless bas aise,

acha kuwaza kimaskini hivyo, huenda ndio maana huishi kulalamika na inaonekana ni mvivu haswa, right?

kwani kwenye soko la dunia kuna mtu anapanga bei za soko hilo gentleman?🤣
 
mwenye akili tuliza mihemko useless bas aise,

acha kuwaza kimaskini hivyo, huenda ndio maana huishi kulalamika na inaonekana ni mvivu haswa, right?

kwani kwenye soko la dunia kuna mtu anapanga bei za soko hilo gentleman?🤣
Nani kapanga bei ya dhahabu au bidhaa zingine duniani?Tanzania yenyewe inafuata hizo bei tu.au zinajipanga zenyewe.Tanzania ni nchi masikini hatuwezi kujipangia chochote nchi zenye uhuru kamili labda Marekani tu au Russia kidogo.
 
mwenye akili tuliza mihemko useless bas aise,

acha kuwaza kimaskini hivyo, huenda ndio maana huishi kulalamika na inaonekana ni mvivu haswa, right?

kwani kwenye soko la dunia kuna mtu anapanga bei za soko hilo gentleman?🤣
Hata mifumo mingi ya ndani wametupangia wao mfano mfumo wa vyama vingi au ubinafsishaji tuliambiwa tuufuate ili tupate mikopo ya benki ya dunia Enzi za Mwinyi.kwahiyo ni mtu mjinga tu wa CCM anayeweza kusema sisi tunauwezo wa kujiamulia mambo wakati Tanzania ni nchi masikini.
 
Nani kapanga bei ya dhahabu au bidhaa zingine duniani?Tanzania yenyewe inafuata hizo bei tu.au zinajipanga zenyewe.Tanzania ni nchi masikini hatuwezi kujipangia chochote nchi zenye uhuru kamili labda Marekani tu au Russia kidogo.
unaniuliza mimi tena gentleman?🤣

kwani pale kariakoo, nani anawapangia bei, mathalani za simu?

Kwahiyo kuna nchi inakupangia wew nauli yako ya kutoka mbagala mpaka kawe right?🐒
 
Kama taifa tunapitia matukio magumu. Hayajawahi tokea huko nyuma. Kabla ya Okt29 hakuna aliyeamini kama yangeweza tokea machafuko ya vile, mimi ni mmoja wapo. Kuna wadau nakumbuka niliwakatalia kabisa kwamba baada ya uchaguzi hata kama kutatokea uonevu basi wananchi tutanywea. Kilichotokea baada ya uchaguzi kimebaki kama historia mpya TZ.

Baada ya matukio hayo yote kila kiongozi anakili intelligence ilishindwa ng'amua mambo, labda reaction ingekuwa tofauti, uhalisia uabaki pale pale kwamba watu wengi waliouawa hawakuwa kwenye maandamano.

Sasa hapa issue sio inteligence ilishindwa ng'amua mambo, bali akili zetu kutokukubaliana na uhalisia wa mabadiliko ya kisiasa, ndani ya nchi na nje ya nchi. Hata sasa hali ya kutokukubaliana na ukweli bado ipo, tunaona kabisa kuna muswada unaandaliwa USA ila mioyo ya viongozi wetu inaamini hilo nalo litapita, bila kuchukua hatua stahiki.

Mombo pamoja na ukongwe wake wizara ya mambo ya nje, diplomasia imemshindwa, intelligence na alama za nyakati kashindwa soma. Ni dhahiri tukiendelea na mwendo huu, siku si nyingi tunaenda rudia kauli ile ile ya hatukujua kama rungu la USA litatupiga ki namna hii.

Nini Kifanyike Kwa sasa: Kila mmoja atachangia mawazo yake, kila mmoja aheshimu mawazo ya mwenzake.

1. Raisi amrudishe Makamba wizara ya mambo ya nje, apewe jukumu moja tu la kurudisha mahusiano ya kidiplomasia kimataifa. (Nmeongea kikubwa, hata kama sio mbunge anaweza pewa ubunge, najua mpo mtaosema sio mbunge)

2. Raisi awapumzishe kazi mawaziri hawa (Kabudi & Mombo), bado wanaamini kwenye ubabe na sio remorse. watalicost taifa, yani akae mbali nao kabisa.

3. Lissu aachiwe unconditionally, alipwe compasation ya muda aliopotezewa na maumivu familia yake iliyoyapitia. Malipo yafanyike off the books. Pamoja naye zile kesi zilizotokana na uchaguzi, kabla na baada ya uchaguzi zote zifutwe.

4. Raisi ateue jopo la maridhiano ya kweli, litaloongozwa na magwiji wa Africa na Dunia, pia wawepo wazee wetu ambao bado wana nguvu kama Rais Kikwete, Mizengo Pinda, Dr. Slaa, Prof Lipumba, etc. Hawa wazee wet wanajua namna waliituliza Zanzibar baada ya machafuko ya 2001, basi wawe msaada kwenye kuliponya taifa. Wapo wengiunaweza waongezea na wewe.

Rais Samia, pamoja na yote yaliyotokea bado una nafasi ya kuliponya taifa, mwaka sasa umeshakatika, bado big agenda ni okt29, vyema hii agenda ingemalizwa ndani ya miezi 6, tukamove on na development agendas.
Waliofungws kisiasa waachiliwe,walotekwa(ambao hawajulikani waliko)kama wapo waachiliwe, kuwe na uhuru wa habari bila masharti, uhuru wa mahakama, serikali ikubali mchakato wa katiba mpya,na wale wote waliouwa ocktoba 29 wawajibishwe
 
mwenye akili tuliza mihemko useless bas aise,

acha kuwaza kimaskini hivyo, huenda ndio maana huishi kulalamika na inaonekana ni mvivu haswa, right?

kwani kwenye soko la dunia kuna mtu anapanga bei za soko hilo gentleman?🤣
Hapo juzi tu mlipangiwa kuwafungulia chadema wafanye siasa na wamarekani na ulaya.mlitishwa kidogo mkawafungulia chadema. Mnachoweza kujipangia ni kuzalisha machawa tu hapo CCM. ila Tanzania ni kanchi kadogo tu ambacho ni masikini na tutaendelea kupangiwa mambo.
 
Hata mifumo mingi ya ndani wametupangia wao mfano mfumo wa vyama vingi au ubinafsishaji tuliambiwa tuufuate ili tupate mikopo ya benki ya dunia Enzi za Mwinyi.kwahiyo ni mtu mjinga tu wa CCM anayeweza kusema sisi tunauwezo wa kujiamulia mambo wakati Tanzania ni nchi masikini.
kwahiyo gentleman,
ni world Bank au ni nchi gani iliwaambia wapiga kura wa Tanzania wamchague Dr.Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya 98% ya kura zote?🐒
 
Hapo juzi tu mlipangiwa kuwafungulia chadema wafanye siasa na wamarekani na ulaya.mlitishwa kidogo mkawafungulia chadema. Mnachoweza kujipangia ni kuzalisha machawa tu hapo CCM. ila Tanzania ni kanchi kadogo tu ambacho ni masikini na tutaendelea kupangiwa mambo.
hiyo unapotosha kwa makusudi kabisa gentleman 🤣
 
unaniuliza mimi tena gentleman?🤣

kwani pale kariakoo, nani anawapangia bei, mathalani za simu?

Kwahiyo kuna nchi inakupangia wew nauli yako ya kutoka mbagala mpaka kawe right?🐒
Anayetuuzia bidhaa ndo anaifluence bei ziweje hatuwezi kujiamulia.
 
Anayetuuzia bidhaa ndo anaifluence bei ziweje hatuwezi kujiamulia.
labda wewe ndie huwezi kujiamulia mambo yako gentleman, na ni huenda ni kwasababu ya unyonge wa kiuchumi ulionao au vinginevyo,

but kama taifa, tunafanya mambo yetu kwa uhuru, bila kushurutishwa na taifa lolote lile duniani 🐒
 
Upotoshaji upo wapi hapo?CCM hadharani mnasema kama mngekuwa na nguvu mngeiua chadema kabisa lakini juzi baada influence kutoka nje mkaifungulia chadema.hamna hiyo nguvu ya kujiamulia mambo
bado unapotosha gentleman,
anaeweza kuelewa upotoshaji wako ni mfuata mkumbo mwenzako tu 🐒
 
bado unapotosha gentleman,
anaeweza kuelewa upotoshaji wako ni mfuata mkumbo mwenzako tu 🐒
Onesha upotoshaji upo wapi hapo?ukisikia nchi inapewa mikopo kutoka mfano ulaya au Marekani au benki ya dunia au IMF maana yake kuna masharti umepewa na umekubali.moja ya masharti ni kuimarish democracy
 
Onesha upotoshaji upo wapi hapo?ukisikia nchi inapewa mikopo kutoka mfano ulaya au Marekani au benki ya dunia au IMF maana yake kuna masharti umepewa na umekubali.moja ya masharti ni kuimarish democracy
naimarisha demokrasia ya nani kama sio ya kwangu na nchi yangu?

hiyo porojo haina maana yoyote kwenye uhuru wa mambo ya ndani Tanzania gentleman 🐒
 
Gentleman,
ni muhimu uwe bize kidogo kutafuta videtails kwenye mambo madogomadogo yasiyo muhimu sana but yanasaidia kuongeza uelewa na ufahamu wa watu walio serious kujifunza ndani ya jukwaa,

najua nakuchosha but, nivumilie tu na ifahamike tu kwa wadau wote wa JF, kama vile ambavyo pato la taifa letu huongezaka sambamba na pato la mTanzania moja moja mwaka hadi mwaka kutokana na jitihada za makusudi zinazofanywa na serikali sikivu ya CCM kwenye uchumi, wafuata mkumbo wengi huwa wanapinga na kuchanganywa sana na ukweli huo.

Na ndio maana ninasisitiza hapa kwamba, taifa letu Tanzania ni huru kisiasa, kijamii na kiuchumi. Halipo taifa lolote lile duniani linaweza kuishurutisha au kuipangia Tanzania namna ya kufanya mambo yake ya ndani. Hakuna taifa kama hilo duniani na halitawahi kutokea.

Tulipambania uhuru wa taifa letu kwa jasho na damu ya waTanzania pekeyao, bila msaada wa yeyote yule, na hizo World Bank, IMF, IDA na taasisi zingine za fedha unazozijua wewe na wanazozisimamia hawakua sehemu ya mapambano hayo. So, hakuna namna taasisi hizo zinaweza kuingilia uhuru wa taifa letu hata kama zitashinikizwa na na nchi wanazozipa fedha taasisi hizo. Tanzania hawezi kitishwa hivyo gentleman.

Kwamba tutishwe na Marekani halafu tuwaachie uhuru wa taifa letu tulioupigania kwa jasho na damu? halafu waje kutupangia na kutuamilia mambo ya nchi yetu, kwasababu tu wanatukopesha au kutupa misaada kwa hiyari yao?🤣

huenda huo utakua umaskini wa aina mpya, na huenda ukawa ndio umaskini mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.

Diplomasia ya Tanzania, inakwenda kubadili kabisa hali ya mahusiano baina ya Tanzania na Marekani, na kufanya mahusiano hayo ya kihistoria, kua bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote, na yenye maslahi zaidi kwa wananchi wa pande zote husika.

Hayo mengine yabaki kama darasa kwa wanaopenda kujifunza zaidi na kujua mambo, lakini muhimu zaidi ni hayo niliyoyaeleza hapo juu.

Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania hana sababu hata moja ya kubadili serikali yake kwa sasa, nadhani ni muhimu sana akafanya hivyo ikimpendeza baada ya tume ya jinai kumaliza jukumu lake.

Mungu Ibariki Tanzania 🐒
Nachokipenda na nachokifurahia Ni ujibuji wako wa HOja bila matusi wala kejeli,
huenda utakuwa ni Kijana hasa uliyepikwa na UVCCM ya zamani kama Mimi,..

ukiwa unasoma mabandiko yako kuna kosa la kiUchumi linaitwa Impossibility of True Autarky!
umekuwa Ukikirudia mpaka sasa naona Kero kukijibu kila mara..
narudia Hakuna nchi duniani ambayo ni Absolute Autarky.
yaani namaanisha hakuna nchi duniani ambayo iko huru kwa kujitegemea kila kitu yenyewe hapo ndo zana ya Sovereignty inakuwa redifined into Interdependence na hili nimeliongelea sana..

nadhani niishie hapo..

kuhusu Tanganyika kupata uhuru pengine Historia Haukuisoma naelewa maana Hata mimi nilianza kuisoma historia rasmi miaka ya 2006 juzi tu hapa kabla sijaenda kwenye fellowship...

Ngoja nikupe Faida kidogo ya Historia ...
Tanganyika imepata Uhuru kwa kusaidiwa, nikukumbushe tu Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Tanganyika haikuwa "Koloni" la uingereza rasmi, bali ilikuwa Dola ya Udhamini (UNO Trust Territory) chini ya Umoja wa Mataifa, huku Uingereza akiwa msimamizi tu,wakati huo katibu mkuu akiwa Dag Hammarskjöld Kutoka nchini Sweden..Usisahau Kuwa makao makuu ya UNO Kipindi hicho yalikuwa ni Marekani..(ambayo unaibeza sasa hivi)
Mwalimu Julius Nyerere alisafiri mara tatu kwenda New York Marekani (mwaka 1955, 1956, na 1957) kuhutubia Baraza la Udhamini la UNO (UNO Trusteeship Council), mwalimu alitumia sheria na mikataba ya UN kuishinikiza Uingereza itupe uhuru wetu. Bila jukwaa hilo la kimataifa na msaada wa nchi wanachama wa UN waliokuwa wanapinga ukoloni (kama nchi za kisoshalisti na zile za Kiarabu/Asia), harakati za TANU zingechukua muda mrefu sana au kutoswa.

Wakati wa harakati, TANU na Nyerere walipata msaada mkubwa wa hali na mali kutoka nje baadhi ni kama kutoka kwa Kwame Nkrumah (Ghana) Ghana walipopata uhuru 1957, ilitoa msaada wa kisaikolojia, kisiasa, na mbinu kwa vyama vya ukombozi Afrika, ikiwemo TANU, kuna wafadhili binafsi wa ndani na nje mimi nitataja mmoja tu Watu kama Archibald Montgomery walisaidia kufadhili safari za Nyerere kwenda UNO wakati TANU haina pesa.

sasa tuachane na hayo..

nakupeleka mpaka muda tayari tuna Uhuru wetu na Unakumbuka Ujamaa ULiposhindwa Tanzania na Mwaka 1980 nchi ilipofilisika nani alituokoa na kutufanya tubadilishe miundo na sera?

Katika miaka ya 1980 na 1990, Tanzania ilifilisika kiuchumi. IMF na World Bank zilitulazimisha kufuata Marekebisho ya Miundo ya Kiuchumi (Structural Adjustment Programmes - SAPs).
  • Tulilazimika kubadili sera zetu za kijamaa na kuingia kwenye ubepari.
  • Tulilazimika kubinafsisha mashirika yetu ya umma (kama viwanda na benki).
  • Tulilazimika kuanza kutoza ada kwenye shule na hospitali (kitu ambacho Nyerere alikataa mwanzoni).
Kama taasisi hizi hazina nguvu ya kutupangia kitu, mbona tulibadili mfumo wetu wa uchumi ili utakae wao ndio watupe mikopo? Huko sio kuingiliwa?

NAMALIZA MWISHO KABISA KUKUAMBIA KUWA..
TUPO huru "Kisheria" (De jure) ni tofauti na kuwa huru "Kiuchumi" (De facto).
Kama bajeti yetu ya maendeleo bado inategemea mikopo na misaada kutoka World Bank, IMF, na wafadhili wa nje, maana yake uhuru wetu wa kujiamulia mambo unaishia pale mifuko yetu inapokauka. Nchi inayokukopesha kila siku ina sauti kwenye maamuzi yakohata kama haisemi hadharani.

Nikutakie Siku njema sana Comred na hongera kwa kuwa mzalendo kwa kuipambania nchi maana inatka moyo sana kufanya hivyo hasa kwenye kipindi hichi
 
naimarisha demokrasia ya nani kama sio ya kwangu na nchi yangu?

hiyo porojo haina maana yoyote kwenye uhuru wa mambo ya ndani Tanzania gentleman 🐒
naimarisha demokrasia ya nani kama sio ya kwangu na nchi yangu?

hiyo porojo haina maana yoyote kwenye uhuru wa mambo ya ndani Tanzania gentleman 🐒
Si umeambiwa ufanye hivyo baada ya kuona mambo mnayofanya kama kutesa wapinzani Nk.mfano nyie hamuwataki chadema na kama mngekuwa na uwezo mngekifungia milele lakin wenye nguvu wanawawapangia chakufanya.
 
labda wewe ndie huwezi kujiamulia mambo yako gentleman, na ni huenda ni kwasababu ya unyonge wa kiuchumi ulionao au vinginevyo,

but kama taifa, tunafanya mambo yetu kwa uhuru, bila kushurutishwa na taifa lolote lile duniani 🐒
Hivi wewe unaakili timamu kweli?mifumo yetu yote ya uchumi,utawala Nk na niwao wameamua iwe hivi.nitajie jambo tunalolifanya sisi bila kufuata miongozo au mifumo yao?
 
labda wewe ndie huwezi kujiamulia mambo yako gentleman, na ni huenda ni kwasababu ya unyonge wa kiuchumi ulionao au vinginevyo,

but kama taifa, tunafanya mambo yetu kwa uhuru, bila kushurutishwa na taifa lolote lile duniani 🐒
Ngoja nikupe mfano kama Tanzania tungekuwa tunafanya mambo yetu kwa uhuru tungekuwa mbali sana.nakupa mfano kwenye Engo ya uchumi.nchi za kiafrika zime wekewa mfumo ziwe wazalishaji wa raw materials za viwanda vya ulaya,Marekani na nchi kama china.huo mfumo ndo unaosababisha tuwe tunasuasua kwenye kuwa na maendeleo ya kweli ya viwanda.tunatakiwa kuwa na viongozi wenye akili sana kama wa kiasia sio hawa vilaza kama Samuya ili kuzishinda mifumo kandamizi.Ndo maana utakuta tunamadini mengi za kuzalisha vifaa vya umeme lakini ukienda Dukani kila kitu ni made in china.
 
COMRED TLAATLAAH!
Habari? Kazi na Utu!
mimi nataka kusema machache kwenye hoja yako ya kidiplomasia na nitaomba kutofautiana na wewe!
kwanza kabisa Katika ulimwengu wa sasa, hakuna nchi inayojitegemea kwa 100% (absolute autarky), na utegemezi wa kibajeti na kiuchumi sio utumwa, bali ni uhalisia wa nchi zinazoendelea.
Huwezi kusema nchi "inajitegemea kiuchumi" wakati sehemu kubwa ya miradi ya maendeleo inafadhiliwa na mikopo ya masharti nafuu na misaada kutoka nje.

Katika bajeti kuu za kila mwaka za Tanzania, takriban 30% hadi 40% ya bajeti ya maendeleo (miradi ya maji, barabara, afya, na elimu) inategemea fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo (Development Partners) ikiwemo Benki ya Dunia (World Bank), IMF, na nchi wahisani (ikiwemo USA kupitia USAID).

tusisahau kuwa Marekani ina kura ya turufu (veto power) au ushawishi mkubwa sana ndani ya IMF na World Bank. Wakiamua kuweka "rungu" la vikwazo vya kiuchumi, wanaweza kuzuia idhini ya mikopo mipya na misaada, jambo ambalo litaleta mshtuko mkubwa kwenye fedha za kigeni na utekelezaji wa miradi ya ndani.

Mkuu unaposema "hakuna taifa lenye uwezo wa kuipangia Tanzania," unasahau kuwa biashara ya kimataifa inaendeshwa kwa mikataba. Marekani ikitupa vikwazo, haituhumu kwa maneno, inakata agreements zote na mikataba.
Unaifahamu kuhusu Hii mikataba?>
  • AGOA (African Growth and Opportunity Act): Huu ni mkataba unaoruhusu nchi za Afrika kuuza bidhaa zake (kama nguo na mazao) nchini Marekani bila ushuru. Marekani ikiondoa Tanzania kwenye AGOA (kama walivyofanya kwa mataifa mengine yaliyokiuka misingi ya kidemokrasia au haki za binadamu huko nyuma), viwanda vyetu vya ndani vinavyotegemea soko hilo vitafungwa, na maelfu ya Watanzania watapoteza kazi.
  • Misaada ya Sekta ya Afya (PEPFAR & Global Fund): Marekani ndio mfadhili mkuu wa mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, na Malaria nchini kupitia PEPFAR. Mabilioni ya shilingi yanayoingia kwenye sekta ya afya kuokoa maisha ya Watanzania yanatoka huko. Kusema "tumejipatia uhuru na tunajitegemea" huku wagonjwa wetu wanategemea ARVs za bure kutoka kwa walipa kodi wa Marekani ni kujidanganya.
Sera ya mambo ya nje ya Tanzania kwa sasa imejikita kwenye Diplomasia ya Kiuchumi kutafuta masoko, wawekezaji, na watalii. Uhusiano mbaya wa kidiplomasia unaharibu "Country Risk Rating index" (Kielelezo cha hatari ya nchi). Marekani ikitoa tahadhari ya kiusalama au kisiasa (Travel Advisory), inaua sekta ya utalii papo hapo kwa sababu watalii wengi wa kiwango cha juu (high-spending tourists) wanaoingia Zanzibar na Serengeti wanatoka Marekani na Ulaya.Wawekezaji wakubwa wa kigeni (FDI) hawawezi kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo inagombana na mataifa makubwa yanayodhibiti mifumo ya kifedha duniani (kama SWIFT).

Ndugu yangu, uzalendo sio kufumba macho na kukataa ukweli wa kiuchumi (economic reality). Ndio, Tanzania ni taifa huru kisheria (sovereign state), lakini kiuchumi tuko kwenye ulimwengu unaotegemeana (interdependent world).
Kushindwa kwa diplomasia yetu kumesababisha mataifa makubwa kuanza kuandaa miswada ya kutuwekea vikwazo. Tukileta ubabe wa 'sisi ni taifa huru' bila kuangalia ukweli wa takwimu za kibajeti, tutakwama. Uhuru wa bendera hauwezi kulisha wananchi kama uchumi na mifumo ya fedha ikivurugika kwa sababu ya diplomasia mbovu. Ni vyema tukajadili mambo kwa ukweli wa takwimu (facts) na sio kwa hisia za kijasusi za kufikirika.

nimeandika maelezo mengi sana ila ninaunga mkono Uamuzi wa Waziri wa mambo ya nje, Aliposema kuna haja ya kukaa na wamarekani na kuongea nao vizuri kabla mambo hayajaharibika..

nikutakie Asubuhi njema
Asante kwa madini mkuu. Lakini uliyemshauri ni kama unapaka rangi upepo.
 
Back
Top Bottom