Je, nini kifanyike ili kama Taifa tutoke kwenye mkwamo wa kidiplomasia duniani?

Kumtegemea mtu aliyechanganyiwa anayejiita Rais kupitia uporaji wa uchaguzi ni kupoteza muda.
Imani yangu ni kuwa, Ili tutoke hapa tulipokwama ni sharti WaTanganyika wengi waliolala waamke na kuidai Tanganyika yao.
Tanganyika ikirejea lazima watu watakaa mezani wachore upya ramani ya kushirikiana na Zanzibar.
Tusipofanya hivyo, vizazi vijavyo vitafanya maamuzi ya ajabu kiasi kwamba nchi yetu itakosa amani mithili ya Sudani Kusini, Somalia, Eritrea, DR Congo n.k!
 
ungeeleza yale yako ya maana zaidi na ingependesa sana gentleman,

lakini hi ya kumbwelambwela nonsense jukwaani, imekufanya wadau wa JF wakuone ni wewe mtu useless kabisa
Jamaa kakufafanulia vizuri,kiuchumi,kijamii na kimataifa,we umeshupaza shingo uko kichama zaidi!Badilika gentleman!
 
Jamaa kakufafanulia vizuri,kiuchumi,kijamii na kimataifa,we umeshupaza shingo uko kichama zaidi!Badilika gentleman!
nadhani nimeeleza vizuri zaidi tena kwa kina, kwa maslahi mapana ya wadau wote wa JF na sio wafuata mkumbo pekee, right?
 
Comrade Tlaatlaah, nimekusoma vizuri sana. Naona umejitahidi kutetea dhana ya uzalendo, lakini unazungumzia diplomasia ya nadharia ya miaka ya 1970 badala ya uchumi wa kivitendo wa karne ya 21.

Hebu twende kwenye ukweli kidogo (facts over rhetoric) kwenye maeneo uliyogusa kwa kuwa umeyagusa inanibidi niyaseme kidogo:

1. Kuhusu mfano wako wa Joseph Kabila na DRC:

Mkuu nahisi Uko less Informed, Vikwazo vya Marekani dhidi ya Kabila na mfumo wake vilisababisha DRC itengwe kiuchumi na mataifa ya Magharibi. Benki zote kubwa duniani ziliacha kufanya biashara na DRC (De-risking) kwa hofu ya kupigwa faini na Marekani.
Matokeo yake, uchumi wa DRC ulikwama, sarafu yao ikaporomoka, na ikabidi nchi hiyo iweke rehani madini yake yote ya kimkakati (Cobalt na Lithium) kwa nchi moja tu (Uchina) kwa mikataba mibovu ya unyonyaji ili wapate hela ya haraka ya kuendesha serikali.
Huwezi kumtenganisha kiongozi mkuu wa nchi na uchumi wa nchi hiyo; athari ya vikwazo vya mtu binafsi huwa inaikumba nchi nzima kwa namna moja au nyingine.


2. Kuhusu Hoja yako uliyosema "Mikopo sio Hisani, Tunakopa kwasababu tuna uwezo wa kulipa":

Mkuu ashakumsi Matusi Hapa kuna ujinga fulani wa kiuchumi unatakiwa uufahamu gentleman.
Tanzania haikopi kwenye masoko ya biashara yenye riba kubwa (Commercial markets) kama mataifa yaliyoendelea.
Sisi tunakopa kupitia dirisha la IDA (International Development Association) la Benki ya Dunia. Huu ni mkopo wa masharti nafuu sana (Concessional loans) wenye riba ya 0% hadi 1% na miaka 40 ya kulipa. Unajua hiyo pesa ya IDA inatoka wapi?
Ni RUZUKU NA MISAADA inayochangwa na nchi tajiri, na mchangiaji mkuu (Largest Contributor) ni Marekani. Marekani akizuia au akipiga kura ya Veto (ambayo anayo), dirisha la IDA linafungwa. Hiyo sio biashara ya soko huru, ni hisani iliyofichwa kwenye mkopo nafuu. so nakupa faida hiyo leo Mkuu..
nikutolee mfano leo hata kama unaweza kukopesheka milion 300 ila kama wizara ya fedha na BOT wamekuwekea zuio la kukopa hakuna benki yoyote Tanzania itakukopesha hata kama una sifa zote

3.Kuhusu kuita sekta ya Afya na Utalii "Tuvitu tudogotudogo"

Mkuu, hivi Dola Milioni 400 (Zaidi ya Tsh Trilioni 1) kila mwaka kutoka Marekani (PEPFAR) zinazonunua ARVs na kuziweka hai familia za Watanzania zaidi ya Milioni 1.5 ni "kavitu kadogo"? Hivi sekta ya utalii inayotegemea watalii wa Kimarekani na Ulaya, ambayo ndio inaingiza fedha nyingi zaidi ya kigeni (Forex) na kuzuia shilingi yetu isinywee, ni "kavitu kadogo"? Uchumi ukiingia mshtuko wa Forex (Uhaba wa Dola) kwa sababu ya Travel Advisory ya Marekani, bei ya mafuta inapanda, mfumuko wa bei unapaa, na mwananchi wa chini kabisa huko kijijini ndio anaumia. Uchumi mkuu unajengwa na hivyo "tuvitu tudogotudogo" unavyovidharau, kabla ya kuchangia hizi mada za Mustakabali wa Nchi yetu tuhakikishe tuna angalau elimu ya kiuchumi

Kuhusu "Neutrality" yaani "non Align" na Mambo ya Ndani

Ndio maana nikasema namuunga mkono Waziri wa Mambo ya Nje aliyesema kuna haja ya kukaa nao na kuongea vizuri.
Kwenye ulimwengu wa sasa, huwezi kujificha kwenye kivuli cha 'Neutrality' wakati mifumo yetu ya kifedha (kama SWIFT), mifumo ya kiteknolojia ya kiserikali, na hata vipuri vya ndege zetu (Boeing/Bombardier) vinamilikiwa na hakimiliki (patents) za nchi za Magharibi.

Ni vizuri kuwa mzalendo, lakini uzalendo wa kweli ni kuuona ukweli jinsi ulivyo (economic pragmatism) ili kulinda nchi yetu, na sio kuishi kwenye kasumba ya kufikirika kwamba tunaweza kusimama peke yetu bila kuumia. Diplomasia ya sasa ni uchumi na maslahi ya wananchi, si maneno ya jukwaani.

Alamsiki!
 
dhana ya "sovereignty" inategemea unaitumia kwenye mazingira yapi. Dunia ya leo dhana hii imepoteza umuhimu wake zaidi ya interdependance angalia Venezuela, Iran, Palestina, ukraine etc wanavyoingiliwa na wakubwa wa dunia. Internatinal law remains a hoax. Tanzania iliipiga Uganda kwa dhana ya hot pursuit na kumgoa Iddi Amin, Nyerere alikataa wote waliolaumu kwa kuingilia mamlaka ya nchi ya Uganda. Diplomasia ya sasa ni complex. Nadhani ili tushinde hii vita tungeanza kurekebisha mambo yetu ya ndani kumwachia Tundu Lissu na wafungwa wote wa kisiasa,Katiba Mpya seriously, uwajibikaji, reforms za mifumo yetu na maridhiano yatakuja yenyewe na dunia hatimaye itatuelewa.
 
Naungana na wewe kwa 100%
kama tukijifanya tujilembeee kwenye dhana ya Sovereignty na Uhuru basi tusisahau hata sisi tuliwahi kuingilia uhuru wa nchi nyingine yaani Uganda na tukamtoa rais wao ,Hapo hatukuingilia mamlaka ya Nchi?

sikuhizi hakuna Independence kuna Interdependence..
mimi nashauri Busara itumike sio kutunisha Mabavu ambayo kiuhalisia hatuna
 
Maneno tani 900.

Ila wakianza kukushona, hakuna atayejali.
 
Huna hoja kabisa we jamaa zaidi ya uchawa tu.
 
Sovereignty na NAM siyo kuua watu wako na kuchukua wengine kuwasweka jela.

TZ ilivunja uhusiano na Israel na Morocco pamoja na kuwa NAM


Kwasaaa hao wanasema NAM, hawajui hata maana yake nini?

Tuna kundi la viazi ambao wanachojua ni kukaza fuvu tu.
 
Kwa maoni yangu hata dhana na kanuni ya sovereighty ina hitaji kuwa re defined kwa vile ilibuniwa karne ya 17 rejea westfalia/ vienna conventions ni muda mrefu sana mazingira ya jamii,kiuchumi,teknolojia na kisiasa na diplomasia yamebadilika. wataalam wa diplomasia na uhusiano wa kimataifa duniani wafanye utafiti waje na kanuni mpya inayoendana na kisasa, UN iweze kua adopt.
 
Sovereignty imeshakuwa redifined intoa complex reality of global interdependence...
watu hawajielimishi tu
 
Gentleman,
kwani diplomasia ya Marekani ni ya lini ikiwa ya Tanzania ni ya miaka ya 1970? kwamba diplomasia ya Tanzania ni old kuliko ya Marekani ya miaka ya 1800?

kwahiyo gentleman,
DRC inapata changamoto fulani katika uchumi wake kwasababu ya vikwazo alivyowekewa Joseph Kabila specifically? halafu, kwani kawekewa hivyo vikwazo lini pamoja na huo mfumo wake unaeleza?
Benki gani hiyo ya marekani iliacha kufanya biashara na DRC na lini lilitokea hilo?
Licha ya changamoto za kiusalama zisizo koma, ni lini uchumi wa DRC ulikwama gentleman?

Ni vizuri kuwapa wasio elewa mambo haya ufahamu wa na uelewa wa kweli kuhusu vikwazo.
Ikiwa vikwazo hivyo ni kwa mtu binafsi, athari zinamuhusu yeye na mali zake tu,
Na ikiwa vikwazo hivyo vimelenga makampuni fulani ya kibaishara, athari za kiuchumi sasa zinanza kupanda kuanzia kwenye kampuni yenyewe, waajiriwa na nchi kwa kiasia fulani kukosa ilichokua inapata kutoka kwenye kampuni hiyo,
Ikiwa sasa vikwazo vinailenga serikali ya taifa fulani kwa ujumla wake, basi hapo athari zinaongezeka ukubwa zaidi na kupiga hadi tosi za wananchi wake kwa ujumla.
DRC inaendelea kua taifa linalofanya vizuri sana kiuchumi katika eneo la maziwa makuu na hakuna athari za zozote za kiuchumi inazopata baada ya Joseh Kabila kuwekewa vikwazo na Marekani. Anainjoy maisha bila mbambamba yoyote Belgium.

Kwenye suala la mikopo naona bado huelezi ukweli, ila wafuata mkumbo wanakuelewa mno
hakuna mtu au taifa linaweza kumkopesha maskini ambae anaonekana kabisa hana vigezo wala uwezo wa kulipa deni la anachotaka kukopa. Uwezo wa taifa kukopa ndio uwezo wa kiuchumi wa taifa hilo.
Mkopo ni mkopo tu, haijalishi umetoka wapi ila wewe unadeal na anae kopesha, ndio maana nimeeleza hapo juu kwa gentleman, unaeleza tuvitu tudogotudogo sana ambavyo hata darasani Lecture hawezi kukufundisha bali utavikuta stationary kwenye hardcopy ukajisomee mwenyewe. Hata hilo sijui la veto ni kitu cha huko chini kabisa na hakituhusu kama Tanzania hata kidogo.

Mwisho kabisa,
Falsafa ya kutokufungana na upande wowote wa dunia kama msingi wa sera ya mambo ya nje ya Tanzania, ndio inatufanya Tanzania kua taifa ambalo halitishishiki wala kutikiswa na vitisho vya upande wowote ule wa dunia kuhusu mambo yake ya ndani kiuchumi, kisiasa au kijamii. Na ndio maana serikali sikivu ya CCM chini ya Dr SAMIA SULUHU HASSAN, ikipata formal and detailed information kutoka serikali ya Marekani, itachukua hatua muafaka ya makusudi sana na kuhakikisha songombingo hii inayopotoshwa na kutiwa chumvi na wafuata mkumbo inakua solved katika meza ya mazungumzo peaceful kwa maslahi mapana ya wanachi wa nchi hizi mbili zenye mahusiano ya kihistoria ya muda mrefu sana. hicho ambacho wafuata mkumbo wanapotoshana ni ndoto za mchana tu,

Naamini,
licha ya kua confused na hali ya mambo mashariki ya kati rais Donald Trump hawezi kushawishika kabisa na porojo nonsense za seneta TED Cruz alizopenyezewa na kupotoshwa kirahisi kabisa na wafuata mkumbo kuihusu Tanzania
 
Ulizia habari za Nicolas Maduro, ukizipata akili itakukaa sawa.
 
Maneno tani 900.

Ila wakianza kukushona, hakuna atayejali.
hebu jieleze kiufasaha kwa hiyo tani moja yako ya maneono gentleman,
nadhani itapedeza zaid,

badilikeni wafuata mkumbo jamani
 
Ulizia habari za Nicolas Maduro, ukizipata akili itakukaa sawa.
kwanini usizieleze kwa faida ya wadau wa JF gentleman?

au kama kawaida ulipotoshwa nawe kwa kufuata mkumbo ukajibeba kama ulivyo, right?
 
Tiba ni moja tu kuitishwa uchaguzi mwingine huru chini ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi [sio hii ya wateule wa mwenyekiti wa CCM] .

Kinyume na hapo njia ya Rwanda naiona tukiielekea miaka michache ijayo ndipo heshima na maridhiano ya kweli yatafanyika.

Huwezi kupiga risasi watoto, wajawazito, waru wakiwa majumbani mwao useme ulikua unatuliza ghasia , bado unamaliza unaichukua miili unaenda kuizika katika kaburi la halaiki ukiamini umeficha ushahidi.

Watu wakizika viatu, picha, na nguo za ndugu zao huo ni msiba wa kudumu ambao hautoisha.

Balozi anatekwa na kupotea nyumbani kwake, watu wanatekwa mitaani , ofisini, majumbaji kwao wewe unasema shauri ya mapenzi, ushirikina, kukwepa madeni.

Watu wakiona wa juu hawafikiki kirahisi huwa wanaanza na wa chini .

Hizi propaganda mara ni vijana wa nchi jirani, mara walilipwa, mara walifuata mkumbo, mara walichochewa ipo siku zitaunganishwa na itakua kweli na itakaua zaidi ya October 29.

Watu wanaolipwa kupigania kitu hawawezi kuingia kupigana na watu wenye mabunduki na wao wakiwa mikono mitupu.
Your browser is not able to display this video.
 
Comrade!
Pumzika Kunywa Chai na kahawa kwanza nahisi kama unazidi kujichanganya.! na hapo ndio ninapojiuliza Unasoma ili kujibu na kushinda ubishi, au unasoma ili kuelewa uhalisia wa mambo ulivyo kwa sasa?

Umeandika maelezo marefu, lakini umejichanganya kwenye mambo ya msingi sana ya kiuchumi na kihistoria. Ngoja nikufungue macho kwenye maeneo uliyopotoka:

Kuhusu Mimi kusema wewe unatumia Diplomasia ya Miaka ya 1970 Niliposema unazungumzia diplomasia ya miaka ya 1970, sikuwa namaanisha umri wa nchi ya Marekani.
Nilimaanisha unatumia fikra za kipindi cha Cold War (Vita Baridi) ambapo nchi masikini zilikuwa zinajificha kwenye kivuli cha "Neutrality/Non-Aligned Movement" na kufikiri haziwezi kuguswa. Dunia ya sasa ya 2026 inaendeshwa na Economic Interdependence (Utegemezi wa Kiuchumi). Hakuna nchi inayojifungia ndani ikasema haitishiki na mifumo ya kimataifa.
Pili umeuliza kuhusu DRC,vikwazo na benki haya sikiliza,Umeuliza ni benki gani iliyoacha kufanya biashara na DRC na lini uchumi wao ulikwama? Twende kwenye ripoti za kifedha:
  • Kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, Marekani ilipoweka vikwazo kwa watu wa karibu wa Kabila na mfanyabiashara Dan Gertler, benki kubwa za kimataifa kama Deutsche Bank, Citibank, na Barclays zilisitisha kutoa huduma za clearing za sarafu ya Dola (USD clearing) kwa benki za DRC kwa hofu ya kupigwa faini na Wizara ya Fedha ya Marekani (OFAC). Jambo hili kitaalamu tunaita De-risking.(najaribu kukuonyesha maneno ili ukayasome na kuyaelewa)
  • kingine nimeshangaa umesema DRC ipo vizuri kiuchumi Hiyo DRC unayosema inaendelea vizuri, ripoti za IMF na Benki ya Dunia zinaonyesha ina viwango vya juu zaidi vya mfumuko wa bei (inflation), na sarafu yao (Congolese Franc) imepoteza thamani kwa kiasi kikubwa sana. Kabila anaweza akawa anaponda raha Ubelgiji kwa mabilioni aliyojilundikia, lakini wananchi wa DRC ndio wanaoteseka na mfumo mbovu wa kiuchumi uliosababishwa na nchi yao kutengwa. Vikwazo vya mtu binafsi vilivyowekwa viongozi wa serikali huwa vinazuia Foreign Direct Investment (FDI) kutoka mataifa makubwa kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayetaka kuweka pesa kwenye nchi yenye migogoro ya vikwazo. Pengine hii elimu inapaswa uijue au ukaisome na ukajue Vikwazo vya vioungozi huzuia Foreign Direct Investment (FDI)

Kuna vitu nahisi Elimu yako sio kubwa sana kuvijua kwahyo nisamehe kwa kuongea vitu vikubwa vilivyokuzidi samahani sana,, yaani Mkuu, hivi kweli unaita kura ya turufu (Veto Power) ya Marekani ndani ya Benki ya Dunia na IMF kuwa ni "tuvitu twa chini kabisa" visivyotuhusu? Hapa ndio unathibitisha kuwa husomi kuelewa.

Tanzania tunapata mikopo kupitia dirisha la IDA. Hili dirisha halikopeshi kibiashara; linatoa mikopo ya hisani (Concessional loans) kwa nchi masikini kwa kutumia pesa za ruzuku zinazochangwa na mataifa tajiri. Marekani ndio mchangiaji mkubwa zaidi wa fedha hizo. Kusema jambo hili halituhusu wakati tunajenga reli, barabara, na shule kwa fedha hizo za IDA ni kujidanganya mchana kweupe. Huwezi kwenda kukopa kwenye taasisi ambayo mdhamini mkuu amekuwekea vikwazo.

narudia Tena kukufundisha kuhusu Mikopo..
maana kwenye hoja yako ya mikopo, umeandika vitu ambavyo kiuchumi vinaonyesha unachanganya kati ya "Mkopo wa Biashara" (Commercial Loan) na "Mkopo wa Maendeleo/Msaada" (Concessional Loan). Ngoja nikupe mfano rahisi sana wa maisha ya kawaida ili uelewe kwanini hiyo unayoita "mambo ya stationary" ndiyo inayoendesha bajeti ya Tanzania:..
  • Mkopo wa Biashara (Msimamo wako): Ukweli ni kwamba, ukienda benki ya biashara (kama CRDB au NMB) kukopa shilingi milioni 500 kujenga nyumba, watakuomba dhamana (hati ya nyumba/kiwanja) na watakuwekea riba kubwa ya 14% hadi 18% kwa sababu wanajua una biashara inayozalisha. Hapo ndipo unakuwa na haki ya kusema "mimi nina uwezo wa kulipa ndio maana wamenikopesha."
  • Mkopo wa Hisani/Maendeleo (Uhalisia wa Tanzania mikopo tulionayo): ikitokea huna biashara kubwa, unaenda kuomba mkopo kwa tajiri wa ukoo wenu akujengee nyumba ya kuishi, akakuambia "Nenda kachukue milioni 500, utanirudishia baada ya miaka 40, na riba ni 0.5% tu." Mkuu, hapo tajiri hakukopesha kwa sababu una biashara au vigezo vya kibiashara; amekukopesha kwa sababu ya uhusiano wenu mzuri na hisani. Ukimtukana huyo tajiri na kumwambia "huna uwezo wa kunipangia maisha yangu," akasitisha huo mkopo, hutaweza kwenda kukopa benki ya biashara kwa masharti yale yale nafuu.
Tanzania haikopi fedha za kujenga reli (SGR), barabara, au miradi ya maji ya vijijini kwenye masoko ya biashara ya kimataifa yenye riba kubwa (kama Eurobonds) kwa kiwango kikubwa kwa sababu hatuna uwezo huo wa kulipa riba kubwa.Sisi tunakopa kupitia dirisha la IDA (International Development Association) la Benki ya Dunia.
  • Huu ni mkopo wenye riba ya chini ya 1% na muda wa kulipa ni hadi miaka 30 hadi 40.
  • Hizo pesa za IDA unajua zinatoka wapi? Hazitokani na faida ya Benki ya Dunia; ni ruzuku na misaada (donations) inayochangwa na nchi tajiri ili kuzisaidia nchi masikini na zinazoendelea.
  • Marekani ndiye mchangiaji mkubwa zaidi (Largest Contributor) wa fedha hizo za IDA zinazokuja kutujengea shule na zahanati huku kwetu.
Sasa unaposema "Suala la Veto ya Marekani ni la chini kabisa halituhusu," unaonyesha jinsi usivyojua mfumo wa kifedha duniani unavyofanya kazi. Ndani ya Benki ya Dunia, nguvu ya kura (Voting Power) inategemea kiasi cha fedha nchi inachochangia. Marekani ana takriban 15.5% ya kura zote. Sheria za Benki ya Dunia zinasema maamuzi makubwa yanahitaji 85% ya kura. Hii ina maana kwamba Marekani peke yake akisema HAPANA, hakuna mkopo au msaada wowote unaweza kupitishwa na Benki ya Dunia kwenda nchi yoyote. Hiyo ndiyo inaitwa Veto Power.

Nimecheka sana na Inaonyesha Hujui hata mifumo ya Kisenate na kibunge Ya marekani inafanyaje kazi..
basi atleast kasome hata ya Kenya inakaribiana na marekani.

Eti unasema kuwa Rais Donald Trump hawezi kushawishiwa na Seneta Ted Cruz. Unasahau kuwa mifumo ya sera ya mambo ya nje ya Marekani haiendeshwi kwa mihemko ya mtu mmoja. Seneta Cruz akipeleka mswada (bill) Senate na ukapitishwa kuwa sheria, Rais wa Marekani analazimika kuutekeleza kisheria, iwe anataka au hataki.

comrade itoshe kusema tunahitaji kusoma sana, Kuhusu Mada tunazochangia kabla ya kuingia kwenye Hoja..
Mimi ni CCM damu kabisa na ni Kada mzuri tu ila kwenye swala la kushupaza shingo kwenye hili swala nakataa ,kwa sababu najua Hasara zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…