Je, nini kifanyike ili kama Taifa tutoke kwenye mkwamo wa kidiplomasia duniani?

Duuh kaka Asante Kwa elimu
 
Gentleman,
huenda mtoa hoja mwenyewe anashangaa sana na kwakweli huenda wafuata mkumbo wamepotemo kabsaaaa

umeeleza mambo mengi madogomadogo in details mno, lakini nadhani hayana umuhimu kabisa ukilinganisha na mtiririko wa maelezo yangu dhidi ya mtoa hoja, hususan kuhusu muswada wa haki za binadamu wa Ted Cruz.
Umejiexpose vyema kama mwalimu wa historia ingawa si muhimu sana kwa kinachoendelea katika ulimwengu wa kimataifa kwa sasa.

Nachelea kuamini na kuwahakikishia wadau wote wa jf na taifa kwa ujumla kwamba,
kama mtumishi mchapakazi wa wananchi na raia mwema wa Tanzania, vikwazo binafsi alivyowekewa Mafwele havitakua na athari zozote zile kijamii, kisiasa wala kiuchumi kwa taifa letu, ispokua yeye binafsi, labda na familia yake. Istokea mtu anapotosha hili ili apate kiki. Hata hivyo waziri shupavu wa mambo ya nje nchini Balozi Kombo, akizungumza na chombo kimoja cha habari cha kimataifa hivi kariabuni, alikiri kuona taarifa za Mafwele kuwekewa vikwazo na Marekani, lakini hakua na taarifa rasmi kutoka serikali ya Marekani. Aliongeza kua atakapokea taarifa rasmi na kujua kilichofikiwa na serikali ya Marekani, diplomasia ya Tanzania itachukua mkondo wake haraka iwezekanavyo kudhibiti wengine kuonewa.

Gentleman,
nimeuliza ikiwa vikwazo alivyowekewa Josep Kabila binafsi, kama vina athari yoyote kwenye uchumi wa DRC.
unaelezea masuala ya 2016. Kwani kabila kawekewa vikwazo 2016?
nimeuliza ni benki gani imeacha kufanya biashara na DRC, baada ya J.Kabila kuwekewa vikwazo, unaendelea kueleza masuala yale yale ya kale na tuvitu tudogotudogo. Sasa veto ya Marekani ina athari gani kwa Tanzania wakati, mshirika wa kihistoria wa Tanzania, China pia anayo pia? Hata hivyo kuna jambo gani muhimu hivyo hata Marekani itumie veto dhidi ya Tanzania?

halafu usipotoshe wadau,
mkopo si hisani ni uwezo wako wa kiuchumi, na kujitegemea kiuchumi.
Kwani masharti magumu na mashari nafuu yamewekwa kwasababu gani?

Yaani kwavile unanipa mkopo kwa masharti nafuu ndio uwe na haki au nguvu ya kunishinikiza au kunielekeza jinsi ya kuendesha nchi yangu? Huo si utumwa gentleman?

Kwani hao wanaokopa kwenye masharti magumu, walichochewa na nini kufanya hivyo na kuachana na mikopo ya masharti nafuu?.
Aise, ukiwa mnyonge wa kiuchumi utawaza kimaskini na utakua maskini tu, na unaweza kupewa ratiba hata ya kushiriki tendo la ndoa na mke wako, kisa tu wanakupa mkopo wa masharti nafuu, right?.

la mwisho gentleman,
kwanza,
you can name or call me as you wish.
pili, regadless wewe ni wa chama gani cha siasa humu nchini, kwangu mim sio issue ya maan sana, kwasababu hiyo ni haki na uhuru wako, leo unaweza kua kwa chama hii au ile bila mim kuhusika na uamuzi wako.
Na mwisho, suala la kushupaza shingo, kufuata mkumbo au vinginevyo, naona kama bado ni uhuru na haki yako binafsi, na halihusiani kabisa na mtazamo, maoni au msimamo wangu kuhusu mambo mbalimbali humu jukwaani na hata nje ya jukwaa.

daima ninapo kua najadiliana na yeyote yule popote, napendelea sana hitimisho la majadiliano hayo liwe amani, kama watoto na wanafamilia wa mama Tanzania.

kwa msisitizo mkubwa na wa kipekee sana ni kwamba Dr Samia Suluhu Hassan hatafanya mabadiliko yoyote kwenye serikali sikivu ya CCM kwa sasa, mpaka pale tume ya jinai aliyoiunda itakapokamilisha jukumu ililopewa. Lakini pia serikali ya Marekani kupitia porojo za wafuata mkumbo haitaifanya chochote Tanzania kidiplomasia, kwakua hapatakua na athari zozote zile kijamii, kisiasa na kiuchumi, na zaidi sana, hatua yoyote ya Marekani dhidi ya Tanzania, itakua ni fursa muhimu kwa taifa letu kujipanga upya na kufanya vizuri zaidi kukabiliana na ambao watapotoshwa kama Marekani kupitia seneta Ted Cruz i
 
CCM iondolewe madarakani kwanza.
 
Unanipa wakati mgumu sana kukuelewesha maana nahisi ilipaswa usome elimu hii Darasani kabisa na notisi uchukue kwa ajili ya marejeo maana Kiukweli...Kwnye geopolitics wewe ni mweupe sana acha swala la uchumi mbalo ni basic kwa mwanasiasa, Swala la diplomasia pia Mlipishana kabis..

ulisema uliwahi kugombea ubunge?
Mimi niliwahi kugombea Ubunge ila nahisi niko well Informed kuliko wewe..

Umeandika maelezo marefu sana, lakini unazidi kujieka wazi kuwa hufuatilii mifumo ya sheria, siasa,uchumi, na diplomasia ya sasa,ambayo bado unataka kuchangia kitu ambacho huna elimu nacho bali unakariri maneno ya kisiasa. Ngoja nikufundishe vizuri jinsi mambo yanavyofanya kazi, kuanzia huo mswada wa Ted Cruz uliouita "porojo" hadi kwenye jinsi unavyochanganya maana ya mikopo ya kimataifa na mikopo ya Vikoba,NMB,SONGESHA au Kausha Damu.umeeleza mambo mengi madogomadogo in details mno, lakini nadhani hayana umuhimu kabisa ukilinganisha na mtiririko wa maelezo yangu dhidi ya mtoa hoja, hususan kuhusu muswada wa haki za binadamu wa Ted Cruz.
Unadai kuwa Marekani haitafanya kitu na kwamba mswada huo ni "porojo nonsense." Tatizo lako kubwa ni kwamba hujasoma mswada wenyewe (uendeshwaji wake kisheria), bali unadhani ni tamko tu la mtandaoni.

Mswada huu unaitwa "Reassessing the United States-Tanzania Bilateral Relationship Act". (Nenda utafute soma)

Huu si mswada wa Ted Cruz peke yake; umeletwa kwa ushirikiano wa vyama vyote viwili (Bipartisan Bill) na Seneta wa Chama cha Demokratik (Jeanne Shaheen) na Seneta wa Chama cha Republican (Ted Cruz). Unajua maana yake? Iwe yuko madarakani Joe Biden, au Donald Trump wa Republican, mswada huu unaungwa mkono na pande zote mbili za bunge la Marekani (Congress).

Sheria za Marekani zinasema hivi: Mswada ukipitishwa na bunge kuwa sheria, Rais wa Marekani hana nguvu ya kuupuuza, analazimika kuutekeleza kisheria.
Mswada huu unaitaka Serikali ya Marekani kufanya yafuatayo ndani ya siku 90 hadi 180:
  • Section 5 & 6 (Sanctions): Kumpa Rais mamlaka ya kuzuia mali zote (Blocking of Property) na kufuta Visa zote za kuingia Marekani za viongozi wote wa Serikali ya Tanzania, Viongozi wote wa CCM, Viongozi wote wa Jeshi la Polisi, Viongozi wote wa JWTZ, na Viongozi wote wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ambao watatajwa kuwa wamehusika au kushiriki kwenye utekaji, ukandamizaji, au ukiukaji wa haki za binadamu uliotokea tangu kipindi cha uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.
  • Section 7 (Prohibition on Assistance and Investments): Inapiga marufuku kabisa taasisi kubwa za kifedha za Marekani kama Development Finance Corporation (DFC), Export-Import Bank (EXIM Bank), na Trade and Development Agency kutoa mkopo, ruzuku, au bima ya uwekezaji kwa mradi wowote nchini Tanzania.
  • Section 8 (MCC Funds): Inapiga marufuku kabisa fedha za Millennium Challenge Corporation (MCC) kutumika Tanzania.
Huu mswada unaruhusu mambo matatu tu kuendelea: Misaada ya kibinadamu (Humanitarian), misaada ya afya, na utawala bora. Miradi yote ya maendeleo, miundombinu, na uwekezaji inakatwa. Sasa mkuu, mswada unaokata mikopo na bima za uwekezaji wa mabilioni ya dola bado unaita ni "porojo"? hii inagusa uchumi mzima wa nchi!

Sasa veto ya Marekani ina athari gani kwa Tanzania wakati, mshirika wa kihistoria wa Tanzania, China pia anayo pia? Hata hivyo kuna jambo gani muhimu hivyo hata Marekani itumie veto dhidi ya Tanzania?
Mkuu sasa ninazidi kuamini kuwa nabishana na mtu asiyekuwa na elimu kuhusu hata tunadiscuss au kujadiliana nini ninajadiliana na mtu ambaye hana elimu ya anachokijadili hayuko well informed ya anachokiongea kabisa yaaan..

Unauliza "Veto ya Marekani ina athari gani wakati China anayo pia?" dah serious?

Mkuu, hivi kweli unajua jinsi Veto inavyofanya kazi ndani ya taasisi za kifedha (Bretton Woods Institutions)?

China ana Veto ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN Security Council) kuzuia vita au majeshi.
Lakini ndani ya Benki ya Dunia (World Bank) na IMF, China hana nguvu ya Veto! Marekani ndio nchi pekee yenye nguvu ya kura ya Veto (Voting power ya zaidi ya 15%) inayoweza kuzuia mswada wa kifedha peke yake.

China akitaka kutusaidia ndani ya Benki ya Dunia, hawezi kuipindua Veto ya Marekani. China anaweza kutupa mikopo yake binafsi ya kibiashara, lakini hawezi kutulipia ARVs za PEPFAR au kutulazimishia mikopo ya IDA ya Benki ya Dunia..

mkuu Tafuta elimu zaidi Kuhusu haya mambo ujue Athari yake kulko kukaza Fuvu Inaonekana bado sana kwenye haya maswala ni kwamba unatetea kitu ambacho hata hujui unatetea au kupinga kipi
Mkuu,Nikiri Kajifunze kuhusu Uchumi hujui uchumi wa kimataifa unavyofanya kazi especially mikopo ya kimataifa na rank zake nimekuelewesha post za nyuma lakini naona la kuvunda halina ubani hii ni mara ya mwisho..

nimecheka sana umesema "Yaani kwavile unanipa mkopo kwa masharti nafuu ndio uwe na haki au nguvu ya kunishinikiza?"

Hapa ndipo unapoonyesha kuwa hujui kabisa maana ya mikopo ya kimataifa. Unafikiri mikopo ya Benki ya Dunia (World Bank) au IMF ni kama ukikopa benki ya NMB, Songesha, au mikopo ya "Kausha Damu" ya mtaani kwamba ukionyesha una dhamana basi unapewa hela unaenda kufanya unachotaka.

Hapana gentleman!
Mikopo ya maendeleo ya kimataifa (Concessional Loans/IDA) haitolewi kwa sababu una "uwezo wa kulipa" kibiashara. Inatolewa chini ya mikataba inayoitwa "Policy-Based Lending". Hiyo mikopo inakuja na masharti magumu ya kisheria na kitaasisi (Governance reforms).
  • Ukitaka hela ya kujenga reli au shule kutoka Benki ya Dunia, sharti lao la kwanza ni lazima nchi yako iheshimu utawala wa sheria, uwazi wa matumizi, na haki za binadamu.
  • Ukikiuka masharti hayo, hawaji kukudaidai kwa fimbo; wanazuia tu awamu inayofuata ya malipo (disbursement tranche). Miradi yako inasimama, makandarasi wanaondoka, uchumi unakwama.
na nikukumbushe tu huu sio "utumwa" kama unavyouita kwa mihemko,
hii ni Mkataba wa Kisheria (Binding Agreement). Kama hautaki masharti yao, kwanini unakwenda kuomba fedha zao?
Ukisema "Hao wanaokopa kwenye masharti magumu walichochewa na nini?"

nchi zinakimbilia mikopo ya masharti magumu ya kibiashara (Eurobonds) pale tu zinapokuwa zimegombana na wahisani na kukataliwa mikopo ya bei nafuu. Na matokeo yake tunayaona: nchi kama Zambia na Kenya zilipoingia kwenye mikopo hiyo ya kibiashara, uchumi uliyumba na wananchi wakaingia barabarani kwa sababu ya kodi kubwa za kulipa madeni hayo.

Mkuu, hapa ndipo unapoonyesha wazi kuwa unaleta mihemko ya jukwaani na mifano ya kufikirika badala ya kuelewa misingi ya sheria za fedha za kimataifa (International Financial Law). Unazungumzia habari za kupewa ratiba za ndoa kama mfano kwenye mjadala wa Kitaifa kama huu, lakini unashindwa kujibu hoja kwa hoja.

Ngoja nikujibu kwa nini hoja yako kuhusu "mkopo sio hisani" na "mikopo ya masharti magumu" ni upotoshaji mkubwa wa kiuchumi:
Unadai kuwa nchi kupewa mkopo wa masharti nafuu ni ishara ya "uwezo wake wa kiuchumi." Huu ni ujinga mkubwa wa kiuchumi gentleman!

Ukweli ni kwamba, ili nchi ifuzu kupata mikopo ya masharti nafuu ya IDA (International Development Association) ya Benki ya Dunia, kigezo cha kwanza kabisa si kuwa na uchumi imara, bali ni kuwa nchi masikini yenye kipato cha chini kwa kila mtu (Low-income/Lower-middle-income GNI per capita).
  • Mikopo ya IDA inatolewa kwa mataifa ambayo hayana uwezo wa kukopa kibiashara kwenye masoko ya kimataifa kwa sababu yakikopa kibiashara yatashindwa kulipa na kufilisika.
  • Hizo fedha za IDA si za biashara; ni rasilimali zinazochangwa kama ruzuku (grants) na nchi tajiri, huku Marekani akiwa mchangiaji mkuu. Ndio maana ina riba ya 0% hadi 1% na miaka 40 ya kulipa. Kuitwa "mkopo" ni mfumo tu wa kisheria ili nchi ijifunze kuwajibika, lakini kiuhalisia ni msaada uliorandishwa mkopo (concessionality element).
Mkuu, nakubaliana na wewe kwa 100% kwenye suala la amani. Hatuhitaji kufurahia nchi yetu kuingia kwenye matatizo, na sote hapa lengo letu ni kuona "Mama Tanzania" anasonga mbele kwa amani na usalama. Hakuna mwenye hati miliki ya uzalendo, sote tunaitakia mema nchi yetu.
 
Vifo vya vya watu zaidi ya 3000 tena kwa makusudi? No way! Tukifanya kosa kama hili siku zijazo watarudia tena kuua wengi zaidi.
 
Hiyo busara wenzako wanaogopa itawatoa madarakani ndio maana hawaitaki
 
Mataifa yetu ha
Umeeleza vyema sana, nami nimepata darasa hata kwa ambayo sikuyawaza kwa harakaharaka. Lakini pia linaposemwa taifa huru; ni ngumu kuwa huru kama unategemea misaada au mikopo kutoka kwa wakubwa ambao nao wana interest zao. Utakuwa huru kama unaweza kutengeneza na kutumia kilichochako. Na huwezi kuwa jeuri kwa watu ambao unahitaji msaada wao.
 
Njia pekee ya kuondoa mkwamo ni kurekebisha ya ndani kwanza....

1. Kesi ya Tundu Lissu ni moja ya kaa la moto sana.
2. Kurekebisha demokrasia yetu kama tumekubali vyama vingi why unang'ang'ania mfumo wa chama kimoja? Dunia imebadilika sana miaka 30 ya kuwadanganya wahisani kama kuna demokrasia ishapita hizo enzi. Watu wana information. Tuwe na katina bora maisha yaendelee nchi ni yetu sote.

3. Tuache kutekana kuumizana. Tusije geuka gang state....

Marekani akikubana tutaanza kukimbiaba humu ndani....
 
Kuna watu nadhani wanalala na kushinda kwa waganga, na wamepewa masharti ya kuua, kutesa na kuteka watu.

Imagine, mtu anaambiwa aache kutesa, kuua na kuteka watu, anasema kwanini anashinikizwa, anatakiwa asiingiliwe aache aendelee kuua, kuteka na kusweka watu rumande.

Huku kama siyo kuchanganyikiwa ni nini?
 
Mkataba na Shetani haujawahi kuwa na mwisho mwema!
 
Unaweza rudia kusoma huu upuuzi wako?
 
Wakaapishana kwenye Kambi ya jeshi wakadhani mambo yataishia hapo.
Sasa ni miezi nane kabisa bado wanatafuta legitimacy
Na wakishupaza shingo. Itafika 2030 bado mambo hayajakaa sawa

Kazi wanayo
 
Gentleman,
msaada hautegemewi, kwasababu ni hiyari yake atoae, kwamba atoe au asitoe, na ndio maana hata muasisi wa taifa letu alisisitiza sana taifa kujizatiti kikamilifu, watu kujifunga mkaja na kufanya kazi kwa bidii ili hatimae kujitegemea.

Na mataifa mengi duniani yanajitegemea na kutegemeana kwa kiasi, kulingana na mahitaji yao na maslahi mapana ya wananchi wao.

Lakini pia,
ni wapi unaweza kukopeshwa bila interest? Ni nani pia anaweza kukopa bila ya kua na interest ya anachokikopa? hata kausha damu tu wana interest zao, na wakopaji pia wana interest zao, kwa kuamua kwa uhuru kwenda kukopa kwa huyu, na sio kwa yule. Na hapo ndipo unaonekana uhuru wa mkopaji.

Kuna mambo mataifa yanaweza kutegemeana, hususani kiteknilojia, kwenye raw materials mbalimbali, kibaashara n.k
Na kwenye biashara, hakunaga kushurutishana kama ilivyo kwenye mambo mengine ya ndani ya taifa moja dhidi ya jingine.

Tanzania haihitaji kua na kiburi dhidi ya taifa lolote lile dunia, kwasababu liko huru kufanya mambo yake ya ndani kulingana na utamaduni na standards zake yenyewa.
Hayupo wa kuishurutisha au kuipangia Tanzania jinsi ya kuendesha mambo yake ya ndani. Full stop πŸ’
 
Huna akili.Sisi hatuna hiyo nguvu ya kujiamulia mambo.Sisi ni kanchi kadogo tu na masikini hatuwezi kupanga hata bei za bidhaa zinazouzwa soko la dunia.
 
Piga hilo kenge
 
Gentleman,
ni muhimu uwe bize kidogo kutafuta videtails kwenye mambo madogomadogo yasiyo muhimu sana but yanasaidia kuongeza uelewa na ufahamu wa watu walio serious kujifunza ndani ya jukwaa,

najua nakuchosha but, nivumilie tu na ifahamike tu kwa wadau wote wa JF, kama vile ambavyo pato la taifa letu huongezaka sambamba na pato la mTanzania moja moja mwaka hadi mwaka kutokana na jitihada za makusudi zinazofanywa na serikali sikivu ya CCM kwenye uchumi, wafuata mkumbo wengi huwa wanapinga na kuchanganywa sana na ukweli huo.

Na ndio maana ninasisitiza hapa kwamba, taifa letu Tanzania ni huru kisiasa, kijamii na kiuchumi. Halipo taifa lolote lile duniani linaweza kuishurutisha au kuipangia Tanzania namna ya kufanya mambo yake ya ndani. Hakuna taifa kama hilo duniani na halitawahi kutokea.

Tulipambania uhuru wa taifa letu kwa jasho na damu ya waTanzania pekeyao, bila msaada wa yeyote yule, na hizo World Bank, IMF, IDA na taasisi zingine za fedha unazozijua wewe na wanazozisimamia hawakua sehemu ya mapambano hayo. So, hakuna namna taasisi hizo zinaweza kuingilia uhuru wa taifa letu hata kama zitashinikizwa na na nchi wanazozipa fedha taasisi hizo. Tanzania hawezi kitishwa hivyo gentleman.

Kwamba tutishwe na Marekani halafu tuwaachie uhuru wa taifa letu tulioupigania kwa jasho na damu? halafu waje kutupangia na kutuamilia mambo ya nchi yetu, kwasababu tu wanatukopesha au kutupa misaada kwa hiyari yao?🀣

huenda huo utakua umaskini wa aina mpya, na huenda ukawa ndio umaskini mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.

Diplomasia ya Tanzania, inakwenda kubadili kabisa hali ya mahusiano baina ya Tanzania na Marekani, na kufanya mahusiano hayo ya kihistoria, kua bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote, na yenye maslahi zaidi kwa wananchi wa pande zote husika.

Hayo mengine yabaki kama darasa kwa wanaopenda kujifunza zaidi na kujua mambo, lakini muhimu zaidi ni hayo niliyoyaeleza hapo juu.

Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania hana sababu hata moja ya kubadili serikali yake kwa sasa, nadhani ni muhimu sana akafanya hivyo ikimpendeza baada ya tume ya jinai kumaliza jukumu lake.

Mungu Ibariki Tanzania πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…