Je, ninunue aina ipi na nizitunze vipi cadet na jeans zikae walau mwaka?

Je, ninunue aina ipi na nizitunze vipi cadet na jeans zikae walau mwaka?

Tumia Sabuni za kipande hazina acid Nyingine ambazo unaweza kufulia na kuogea, usifulie MAJI ya chumvi, usiache Nguo juani kutwa nzima ikiwezekana anima kuani mda mfupi MAJI yakichuja zianike kimvulini zikauke kwa upepo utaratibu, nimeshawahi kukausha Nguo kwaupepo wa feni Nguo inakauka vizuri, pia wakati wa kunyosha tanguliza kitambaa Juu ya Nguo unayonyoosha na Pasi inazuia Nguo kupauka haraka, ni hayo tuu nawasilisha
 
Nunua maduka ya Woolworths (Posta au Mlimani City au Mikocheni - Kwa Warioba) hutajutia. Mimi nina uniform dress code yaani navaa nguo za aina moja kila siku na sio nguo nyingi ila huwa zinadumu muda mrefu sana.
 
Ongeza idadi ya nguo ,ukiwa na nguo nyingi nguo Moja inachukua siku nyingi hadi kuirudia hivyo idadi ya kufuliwa na kupigwa na jua inapingua kama mfuko hauruhusu usijipinde sana kununua za duka .

Tafuta mtumba uchanganye na za duka
Umemshauri vzr Sana huu ndio ushauri mzuri niishie hapo kusoma comment,
 
Tumia Sabuni za kipande hazina acid Nyingine ambazo unaweza kufulia na kuogea, usifulie MAJI ya chumvi, usiache Nguo juani kutwa nzima ikiwezekana anima kuani mda mfupi MAJI yakichuja zianike kimvulini zikauke kwa upepo utaratibu, nimeshawahi kukausha Nguo kwaupepo wa feni Nguo inakauka vizuri, pia wakati wa kunyosha tanguliza kitambaa Juu ya Nguo unayonyoosha na Pasi inazuia Nguo kupauka haraka, ni hayo tuu nawasilisha
Wew Ni hasara tupu ucheze umeme Lisa kikadeti Cha elf 17
 
Ongeza idadi ya nguo.
Nguo kama ni qualify hazipauki kirahisi, , miaka ya nyuma kariakoo kulikuwa na Duka kuitwa Cadbury, jamaa alikuwa analeta nguo first class kutoka USA na Vietnam, , kuna t shirts nilivaa miaka 4 , na nikaja kuuza kama mtumba mbeya huko.
Siku hizi ukinunua shati ukalifua mara nne tu hata pasi halikubali tena
 
Cadet na Jeans zina kanuni zake za utunzaji!
Wewe bila shaka ulizianika kwenye jua, ulizifua kwa kutumia sabuni ya unga, unatakiwa uzipige pasi nje ndani(naamini hukufanya hivyo), ulitumia maji ya chumvi kuzifua, ulizikamua na kuzikung'uta!
Zitatamanikaje sasa...!?
Nguo za mitumba cadet hiyo hiyo imetumika ulaya na hapa utavaa kufua na kuanika bila masharti .
Kuna shida kwenye ubora wa nguo mpya tunazoletewa , watu inaonekana wanachukua the lowest of the already low quality products.
 
Kuna kale karaha mtu upo huko katika shughuli zako umevaa nguo bado zipo fresh, Sio unapita sehemu nguo imepauka / rangi zimefifia yani hata mtu akikuangalia mara mbili unajua tu hapa kipengere ni nguo.

Nilinunua jeans 2 na cadet 2, kwa ufinyu wa bajeti yangu nilinunua jeans elf 25 kwa pair na cadet zilikuwa elf 28 kwa pair.

Nilitegemea walau zinivushe huu mwaka lakini hali imekuwa ndivyo sivyo, Kwa sasa naanza kuona hata soo kuzivaa.

nawaza hapa nikanunue cadet na jeans aina ipi ambazo zitaweza kunivusha salama huu mwaka na pia nizitunze vipi.

Jamani nguo zinanipasulia bajeti naombeni ushauri please.
Nimeachana na kadet kabisaa. Nanunua za vitambaa kama waimba kwaya

Kadet na jeans seems wanatumia rangi za chaki maana zinapauka utadhani ngozi ya mamba. Na zinanyambukanyambuka kwenye pindo balaa
 
Hili tatizo la cadet na jeans ni kubwa sana,Nunua za 15k,25k,35k, mpaka 45k wembe wa kupauka ni ule ule,tena ukifua mara moja tu kwisha kazi. Huwa naenda dampo pale Mwanza madukani nawaambia wauzaji ni heri zije nguo disposable,unavaa mara moja unatupa,kuliko kununua nguo elfu 45 unavaa mara moja alafu huwezi rudia tena kwa mtoko. Nadhan kuna haja serikali iingilie kati ubora wa nguo zinazoingizwa nchini. Iliwah kufanyika kwenye mabus,unakata tiketi bus luxury alafu ukija kuliona unachoka kabisa,baadae serikali ikayapa Class mabus yote
 
Back
Top Bottom