Je, ninunue aina ipi na nizitunze vipi cadet na jeans zikae walau mwaka?

Tumia Sabuni za kipande hazina acid Nyingine ambazo unaweza kufulia na kuogea, usifulie MAJI ya chumvi, usiache Nguo juani kutwa nzima ikiwezekana anima kuani mda mfupi MAJI yakichuja zianike kimvulini zikauke kwa upepo utaratibu, nimeshawahi kukausha Nguo kwaupepo wa feni Nguo inakauka vizuri, pia wakati wa kunyosha tanguliza kitambaa Juu ya Nguo unayonyoosha na Pasi inazuia Nguo kupauka haraka, ni hayo tuu nawasilisha
 
Nunua maduka ya Woolworths (Posta au Mlimani City au Mikocheni - Kwa Warioba) hutajutia. Mimi nina uniform dress code yaani navaa nguo za aina moja kila siku na sio nguo nyingi ila huwa zinadumu muda mrefu sana.
 
Ongeza idadi ya nguo ,ukiwa na nguo nyingi nguo Moja inachukua siku nyingi hadi kuirudia hivyo idadi ya kufuliwa na kupigwa na jua inapingua kama mfuko hauruhusu usijipinde sana kununua za duka .

Tafuta mtumba uchanganye na za duka
Umemshauri vzr Sana huu ndio ushauri mzuri niishie hapo kusoma comment,
 
Wew Ni hasara tupu ucheze umeme Lisa kikadeti Cha elf 17
 
Ongeza idadi ya nguo.
Nguo kama ni qualify hazipauki kirahisi, , miaka ya nyuma kariakoo kulikuwa na Duka kuitwa Cadbury, jamaa alikuwa analeta nguo first class kutoka USA na Vietnam, , kuna t shirts nilivaa miaka 4 , na nikaja kuuza kama mtumba mbeya huko.
Siku hizi ukinunua shati ukalifua mara nne tu hata pasi halikubali tena
 
Nguo za mitumba cadet hiyo hiyo imetumika ulaya na hapa utavaa kufua na kuanika bila masharti .
Kuna shida kwenye ubora wa nguo mpya tunazoletewa , watu inaonekana wanachukua the lowest of the already low quality products.
 
Nimeachana na kadet kabisaa. Nanunua za vitambaa kama waimba kwaya

Kadet na jeans seems wanatumia rangi za chaki maana zinapauka utadhani ngozi ya mamba. Na zinanyambukanyambuka kwenye pindo balaa
 
Hili tatizo la cadet na jeans ni kubwa sana,Nunua za 15k,25k,35k, mpaka 45k wembe wa kupauka ni ule ule,tena ukifua mara moja tu kwisha kazi. Huwa naenda dampo pale Mwanza madukani nawaambia wauzaji ni heri zije nguo disposable,unavaa mara moja unatupa,kuliko kununua nguo elfu 45 unavaa mara moja alafu huwezi rudia tena kwa mtoko. Nadhan kuna haja serikali iingilie kati ubora wa nguo zinazoingizwa nchini. Iliwah kufanyika kwenye mabus,unakata tiketi bus luxury alafu ukija kuliona unachoka kabisa,baadae serikali ikayapa Class mabus yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…