Je, ninunue gari gani kati VW Tuareg, VW Tiguan, Audi Q5 ama Toyota Fortuner?

Wakenya wengi sasa hivi wananunua magari South; yaani wamejua kutumia unafuu wa kodi kea kutumia SADC. Hebu tupe shule kidogo hapa.
Wakenya wananunua gari nyingi SA kwa sababu Nchi yao imepunguza miaka ya magari yanayohitajika kuingia na wakiangalia kutokana na wao wana kipato kikubwa wanaona SA gari zipo bei rahisi hata mimi wateja wangu wengi ni Wakenya na pia Nchi yao parts nyingi zipo na hawaulizani ulizani anunue gari gani kama kwetu kwa sababu ya kodi zipo juu sana..
 
Mtu anaetaka kuliendesha toka S.A mpaka bongo, kuna changamoto yeyote? Au vitu anatakiwa awe navyo?
 
No. Namaanisha mambo ya vibali au usajili wowote unaohitajika ili uweze pita hizo nchi.
Aah ok unalipia kwa agent ni road toll tuu kwa Botswana ni kama pula 500 mpaka 600 na SA kutoka agent unampa rand 500 pia ili arudishe taarifa za gari ministry of trade and export lionekane limetokea mpaka gani ingawaje watu wa Custom ndio kazi yao ila wao kufika taarifa zinachelewa kuliko Agent..Leseni unatumia hiyo hiyo kuendesha usumbuliwi upande wa Zambia wana Council levy na Toll ipo kwa 25 usd kwa gari ndogo na utamlipa Agent hela yake hapo kwa kazi hiyo basi hapo Kazungura boarder hakuna usumbufu wowote huko...ukiwa mwenyeji zaidi utapita Zimbabwe,Msumbiji kidogo kupitia Tete harafu Malawi kasumuru Mbeya mipaka yetu ipo vizuri sio wasumbufu kama unavyosikia hata ukiwa mgeni utaonyeshwa njia sahihi ila ukibeba truck ukaja Pombe habari yake utaisikia ingawaje ni biashara inayotoka haraka nadhani kuliko biashara nyingi sana...
 

Shukrani sana
Nadhani nitakupa kazi one day uniletee chombo tz
 
Pia gharama ya kwenda south kwa basi ikoje ili kama vipi nasafiri kwa basi alafu tunarudi na magari
Ndege ndio gharama nafuu kusafiri na kulipia Corona Tanzania na Zambia bora upae tuu na pia muda na mambo ya kulala Zambia ili upime Corona nishasahau mambo ya bus kipindi hiki ni usumbufu mno wanaweza wanaobeba mizigo kutoka SA kwa bus..
 
Mkuu mtu anawezaje kununua hii gari kutoka south Afrika. Kweli kodi yake ni kidogo sana tofauti na kutoa Japan.
 
Mkuu mtu anawezaje kununua hii gari kutoka south Afrika. Kweli kodi yake ni kidogo sana tofauti na kutoa Japan.
Nashangaa hii ishu ni ya muda mrefu ila TRA wameweka password kitengo chao cha Elimu hawazungumzii hili kabisaa kuhusu unafuu wa kodi kwa Nchi wanachama wa SADC kuhusu manunuzi ntakuelekeza baadae Mkuu
 
Toyota Fortuner Mnyama
 
Hawataki tuwe wajanja ili watukamue vizuri.
Wao wapo busy na upuuzi wa kukamatana risiti kwa vitu vya kwenye bahasha wakati bree unashusha Kontena hakuna hata anaekugusa anajua umelipa kodi na ukiuza nchi inapata mapato makubwa hapo Bongo wapo kwa ajili ya kukwamishana ndio maana bidhaa nyingi hakuna kama Nairobi ila sisi tuna bandari kubwa kuliko wenzetu sijui tumerogwa yaani Watanzania wanafata Nguo Uganda na mizigo imepita Transit kwenye Ardhi yetu....
 
Suala la mitumba Uganda nadhani wao hawana makodi mengi kwenye mitumba ndo maana kule nguo ni bei rahisi sana.

Kutokuwa na vitu vingi vizuri tanzania ni ushamba na kukosa hela. Asilimia kubwa ya wabongo hawana kipato cha kuinfluence vitu vizuri kuja.
 
Hapana kutokua na vitu vingi ni lundo la kodi na pia kukomalia vitu vichache kuona tuna vitu angalia tuu hapo Nairobi bidhaa zilivyo za kutosha au Lusaka Zambia sasa Tanzania wana mfumo eti polisi sijui na TRA wanakimbizana na mifuko ya risiti ni Nchi gani huo upuuzi upo? Hao wakija Bree street wanaweza kufa maana watu wanauza jumatatu mpaka jumatatu kinachozingatiwa ni kodi ya kuingiza mzigo nayo huwezi kukwepa Tanzania bidhaa zinaingia kwa masharti kibao makodi ya kutosha kwenye kuuza muuzaji anatishiwa tena kamata kamata Nchi nzima wakati huku nimetumiwa ujumbe wa kunishukuru kulipa kodi ya mwaka jana na kama pana tatizo lolote niwaone...vitu vingi vipo madukani Tanzania hasa Tv unaiona mpya ila toleo la zamani hasa kwa haya majina makubwa...kuishi vizuri tunaona kama anasa sio watu wanatakiwa waishi vizuri kwa kutumia kipato kidogo kupata bidhaa nzuri..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…