Tuliambiwa tozo za miamala ya simu ni kwaajili ya ujenzi wa madarasa. Kadhalika, juzi kati serikali ya mama samia imekopa kiasi cha zaidi ya trioni moja kutoka IMF ambapo zaidi ya mabilioni ya pesa kwenye huo mkopo yametengwa kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kama sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo january 2022.
Lakini katika hali ya kushangaza pamoja na makato ya tozo na mkopo wa IMF uliotolewa, wananchi katika maeneo mbali mbali wameanza kubebeshwa mzigo tena kwa kuamuriwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na molamu kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madrasa.
Maswali ya kujiuliza ni Je, pesa za tozo ya miamala ya simu wananchi wanazokatwa zinaenda wapi?
Je, zile milioni 20 kutoka kwenye mkopo kwaajili ya ujenzi wa madarasa zimeenda wapi? Zimeanza kupigwa?
Je waziri wa tamisemi anajua kama wananchi wanasombeshwa mchanga na kokoto kwaajili ya ujenzi wa madarasa ikiwa tayari kuna fungu la fedha limetengwa kwaajili hiyo?
Je, Rais Samia anayajua haya? Yana baraka kutoka kwake?