Je, Pesa za IMF zimeanza kupigwa? Wananchi wanasomba Mawe na Kokoto kwaajili ya ujenzi Madarasa

Tuliambiwa tozo za miamala ya simu ni kwaajili ya ujenzi wa madarasa. Kadhalika, juzi kati serikali ya mama samia imekopa kiasi cha zaidi ya trioni moja kutoka IMF ambapo zaidi ya mabilioni ya pesa kwenye huo mkopo yametengwa kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kama sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo january 2022.

Lakini katika hali ya kushangaza pamoja na makato ya tozo na mkopo wa IMF uliotolewa, wananchi katika maeneo mbali mbali wameanza kubebeshwa mzigo tena kwa kuamuriwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na molamu kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madrasa.

Maswali ya kujiuliza ni Je, pesa za tozo ya miamala ya simu wananchi wanazokatwa zinaenda wapi?

Je, zile milioni 20 kutoka kwenye mkopo kwaajili ya ujenzi wa madarasa zimeenda wapi? Zimeanza kupigwa?

Je waziri wa tamisemi anajua kama wananchi wanasombeshwa mchanga na kokoto kwaajili ya ujenzi wa madarasa ikiwa tayari kuna fungu la fedha limetengwa kwaajili hiyo?

Je, Rais Samia anayajua haya? Yana baraka kutoka kwake?
Lini waliwahi acha kusomba mawe na kokoto? Huo ni utaratibu wa miaka yote ku cut cost unafanyika hivyo kwenye miradi yote ya P4R kwenye sekta zote ni njia ya kuwashirikisha kwenye ujenzi .
 
Either utakua mtoto sana au huelewi maana ya maendeleo

Wananchi kijiti Lea ni jambo la kawaida hata Kama tungepata mkopo kutoka Kwa yesu

Tusijitoe ufahamu na kuwa wadekaji na legelege… waasisi wa taifa hili hawakua hivyo

Hakuna maendeleo utakayopata huku ukiwa umekunja nne
 
Lini waliwahi acha kusomba mawe na kokoto? Huo ni utaratibu wa miaka yote ku cut cost unafanyika hivyo kwenye miradi yote ya P4R kwenye sekta zote ni njia ya kuwashirikisha kwenye ujenzi .
Hivi vitoto vya tube light ni shida sana

Hajui tumetoka wapi

Miradi ya maji vijijini tulichimba sana mitaro na kutandika mabomba

Ndio dhana halisi ya ushirikishwaji umma
 
Kila darasa mil 20.

Wananchi mambumbumbu lazima wahenyeshe wote kijani hao
Kwahiyo kwenye zabuni ya mradi Mkandarasi aliambiwa kwenye bajeti yake asiweke gharama za usombaji mawe na kokoto? Au fedha za mikopo ya wafadhili huwa hazina fungu la usombaji mawe na kokoto? Sina hakika kama mikopo hii inawezatupeleka kwenye
Ricardian Equivalence Theorem

Ricardian equivalence is an economic theory that argues that attempts to stimulate an economy by increasing debt-financed government spending are doomed to failure because demand remains unchanged.
 
Hao ni watuwa mandno mkuu! Huyu mama analetewa miradi hewa na akina na mwigulu Nchema anasaini tu! Nakuhakikishia hata uwexo wake wa kufatilia miradi ni mdogo na uzuri hata yeye alikili kuwa hawezi kufanay hivo ila anaangali graph ndo anachoweza sasa kikubwa mwandaa graph hewa anajeza nae kwa akili tu! Wanamletea wageni wa kizungu kila siku Ikulu kupiga nae stori na kumpangia ziara! Mwisho wa siku hela na miradi haikamiliki! Mda utaongea!
Edit hueleweki,soma kabla ya kupost
 
Mimi sio msemaji ila nakumbuka tozo za mwanzo sijui bilion 48 kabla ya kupunguzwa kwa 30% zilitolewa kujenga vituo vya afya na Tamisemi walitoa orodha vituo hivyo kwa kila mkoa.
Tuliambiwa tozo ni kwaajili ya ujenzi wa madarasa ili kuwapunguzia wananchi mzigo na kuna kiasi cha pesa kama bilioni kadhaa zilitengwa kwaajili ya shughuli hiyo + mkopo wa IMF. Sasa kama malengo yalikuwa ni kupunguzia wananchi mzigo, kwanini wachimbishwe tena msingi na kusombeshwa mchanga na kokoto kwaajili ya ujenzi wa madarasa? Ina maana hii serikali inatuhadaa wananchi?
 
Lini waliwahi acha kusomba mawe na kokoto? Huo ni utaratibu wa miaka yote ku cut cost unafanyika hivyo kwenye miradi yote ya P4R kwenye sekta zote ni njia ya kuwashirikisha kwenye ujenzi .
Bwana mkubwa huu ujenzi nazungumzia madarasa yanayojengwa kwa zile pesa za mkopo kutoka IMF ambapo imetengwa mil 20 kwa kila darasa, iweje sasa wananchi waenyeshwe ikiwa pesa ya ujenzi ipo? Huoni kama kuna dalili za upigaji hapa?
 
Wakizipiga watajuwa #RANGI YA MAMA.
 
Back
Top Bottom