Je, Pesa za IMF zimeanza kupigwa? Wananchi wanasomba Mawe na Kokoto kwaajili ya ujenzi Madarasa

Je, Pesa za IMF zimeanza kupigwa? Wananchi wanasomba Mawe na Kokoto kwaajili ya ujenzi Madarasa

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
284
Reaction score
912
Tuliambiwa tozo za miamala ya simu ni kwaajili ya ujenzi wa madarasa. Kadhalika, juzi kati serikali ya mama samia imekopa kiasi cha zaidi ya trioni moja kutoka IMF ambapo zaidi ya mabilioni ya pesa kwenye huo mkopo yametengwa kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kama sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo january 2022.

Lakini katika hali ya kushangaza pamoja na makato ya tozo na mkopo wa IMF uliotolewa, wananchi katika maeneo mbali mbali wameanza kubebeshwa mzigo tena kwa kuamuriwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na molamu kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madrasa.

Maswali ya kujiuliza ni Je, pesa za tozo ya miamala ya simu wananchi wanazokatwa zinaenda wapi?

Je, zile milioni 20 kutoka kwenye mkopo kwaajili ya ujenzi wa madarasa zimeenda wapi? Zimeanza kupigwa?

Je waziri wa tamisemi anajua kama wananchi wanasombeshwa mchanga na kokoto kwaajili ya ujenzi wa madarasa ikiwa tayari kuna fungu la fedha limetengwa kwaajili hiyo?

Je, Rais Samia anayajua haya? Yana baraka kutoka kwake?
 
wafanyabiashara wako kwenye likizo ya kodi. Nimefanya uchunguzi wa masaa machache kwenye maduka ...munkari wa kutoa na kudai risiti za manunuzi umeshuka sana. Tena sana!nadhani nimeeleweka.
 
Hela lazima ziliwe mkuu.

Sehemu kubwa wananchi wanapoweza kufanyishwa hizi kazi ni vijijiji na hawawezi kuhoji hata kidogo
 
Kila darasa moja limetengewa milioni 20 sasa inategemea eneo lilipo mradi,kama vifaa vya ujenzi ni ghali wananchi watatakiwa kujitolea nguvu kazi kama kusanya mawe na kusafisha eneo la ujenzi na kuchimba msingi,na pia kwa uwazi zaidi kamati za ujenzi zinaundwa na wananchi wa eneo husika na kupitia bajeti ya ujenzi(BOQ) ili kijiridhisha.

Katika eneo letu tumepata madarasa mawili na tmepatiwa milioni 40 na wananchi wanatakiwa kusanya mawe na kuchimba msingi tu. Hayo madarasa ni pamoja na madawati.
 
Kila darasa moja limetengewa milioni 20 sasa inategemea eneo lilipo mradi,kama vifaa vya ujenzi ni ghali wananchi watatakiwa kujitolea nguvu kazi kama kusanya mawe na kusafisha eneo la ujenzi na kuchimba msingi,na pia kwa uwazi zaidi kamati za ujenzi zinaundwa na wananchi wa eneo husika na kupitia bajeti ya ujenzi(BOQ) ili kijiridhisha.Katika eneo letu tumepata madarasa mawili na tmepatiwa milioni 40 na wananchi wanatakiwa kusanya mawe na kuchimba msingi tu. Hayo madarasa ni pamoja na madawati.
Tozo za miamala zina kazi gani mbona mzigo bado anabebeshwa mwananchi? Kuna maana gani ya kuendelea kukatwa tozo?
 
Eneo ninaloishi Mbezi ipo njia kama unaelekea Makabe/Msakuzi ni mbovu haielezeki week mbili nyuma kuna sehemu pana mlima wameingiza vifaa kazi majuzi nilikuwa nauliza kwa mjumbe wangu wa mtaa akasema plan iliyokuwepo hata vikao walivyokaa kujadiliana ilikuwa barabara ijengwe kwa urefu wa km 4 ila kipande walichoplan wao mainjinia ni kama metre 70 tu na tena kilimani.

Wanafanya kazi leo wanakaa siku tatu wanarudi tena yaani hamna kitu mbunge naye sijui kafia wapi!!!wanasiasa hawa nyie acheni tu.
 
wafanyabiashara wako kwenye likizo ya kodi. Nimefanya uchunguzi wa masaa machache kwenye maduka ...munkari wa kutoa na kudai risiti za manunuzi umeshuka sana. Tena sana!nadhani nimeeleweka.
Acha tu waache kutoa hizo risit maana pesa zilikua zinaenda kujenga chato na kununua wapinzani.
 
Tozo za miamala zina kazi gani mbona mzigo bado anabebeshwa mwananchi? Kuna maana gani ya kuendelea kukatwa tozo?
Mimi sio msemaji ila nakumbuka tozo za mwanzo sijui bilion 48 kabla ya kupunguzwa kwa 30% zilitolewa kujenga vituo vya afya na Tamisemi walitoa orodha vituo hivyo kwa kila mkoa.
 
Mimi sio msemaji ila nakumbuka tozo za mwanzo sijui bilion 48 kabla ya kupunguzwa kwa 30% zilitolewa kujenga vituo vya afya na Tamisemi walitoa orodha vituo hivyo kwa kila mkoa.
bilioni 48 x 70% = bilioni 33.6. Kwa hiyo tozo tunakusanya bil 33.6. Punguzo hili ndilo linasababisha nguvu ya wananchi?

Hata hivyo, nakumbuka awamu ya kwanza ya Tasaf, Miradi ilikuwa inapelekwa vijijini wananchi wanafanya kazi kwa malipo kutekeleza miradi hiyo. Sina hakika ndiyo sitaili inayotumika kwa sasa.
 
Huo ndio mchango wa nguvukazi sasa nyie wananchi mnaopenda kukaa tuu kucheza draft hamtaki kuchangia maen deleo yenu ?
 
Ukidai risiti utapewa, usipodai muuzaji anakausha.
Si walisema hakuhitajiki kikosi kazi cha kukusanya kodi na tozo, kwa sababu wafanyabiashara wanapenda kulipa kodi isiyo ya dhuluma? Au nilielewa vibaya maelezo yale.?
 
Si walisema hakuhitajiki kikosi kazi cha kukusanya kodi na tozo, kwa sababu wafanyabiashara wanapenda kulipa kodi isiyo ya dhuluma? Au nilielewa vibaya maelezo yale.?
Hiyo kodi isiyo ya dhulma ndio tunailipa namna hii bila kuwa kumbukumbu halisi za mauzo maana hatutoi risiti

Kwenye tozo wametuweza ila kwenye risiti bado.

Wakubwa wanajipigia mamilioni huku wakishindwa kubuni muarobaini wa kukusanya kodi, na sisi ngoja tujipigie kidogo kidogo. Keki ya Taifa ni yetu sote
 
Tuliambiwa tozo za miamala ya simu ni kwaajili ya ujenzi wa madarasa. Kadhalika, juzi kati serikali ya mama samia imekopa kiasi cha zaidi ya trioni moja kutoka IMF ambapo zaidi ya mabilioni ya pesa kwenye huo mkopo yametengwa kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kama sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo january 2022.

Lakini katika hali ya kushangaza pamoja na makato ya tozo na mkopo wa IMF uliotolewa, wananchi katika maeneo mbali mbali wameanza kubebeshwa mzigo tena kwa kuamuriwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na molamu kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madrasa.

Maswali ya kujiuliza ni Je, pesa za tozo ya miamala ya simu wananchi wanazokatwa zinaenda wapi?

Je, zile milioni 20 kutoka kwenye mkopo kwaajili ya ujenzi wa madarasa zimeenda wapi? Zimeanza kupigwa?

Je waziri wa tamisemi anajua kama wananchi wanasombeshwa mchanga na kokoto kwaajili ya ujenzi wa madarasa ikiwa tayari kuna fungu la fedha limetengwa kwaajili hiyo?

Je, Rais Samia anayajua haya? Yana baraka kutoka kwake?
Kila darasa mil 20.

Wananchi mambumbumbu lazima wahenyeshe wote kijani hao
 
Back
Top Bottom