Je, picha rasmi ya Rais Samia Hassan (Hijab Nyekundu) ilizingatia "Soccer Diplomacy" baina ya Simba na Yanga?

Je, picha rasmi ya Rais Samia Hassan (Hijab Nyekundu) ilizingatia "Soccer Diplomacy" baina ya Simba na Yanga?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
17,306
Reaction score
19,885
Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums

Official Portrait ya mkuu wa nchi/serikali sio lazima iwe ya rangi nyekundu. Watanzania acheni kukariri.
==========
ghbgfgtr.jpg

==========
Mama yetu anaweza kwenda na Hijab Nyekundu kutazama mechi ya Simba na Yanga? Ni nani alimshauri Rais wetu kipenzi mama Samia Hassan (bi' mkubwa - huku uswahilini kwetu mama huwa tunamuitaga bi' mkubwa) kupiga picha yake rasmi akiwa amevaa hijab nyekundu? She's was supposed to look neutral.
==========
images (3).jpg

==========
Je, hii ilizingatia diplomasia/siasa ya kimichezo (Sports/Soccer Diplomacy) baina ya simba na yanga? Je, mashabiki/Rais wa Yanga ana haki ya kugomea picha hii ndani ya ofisi yake? Kwanini asingevaa hijab ya rangi nyeusi au ya blue?

Ninaomba mkumbuke kuwa Rais sio Mbunge ndio maana haigemei upande wowote kati ya hao vijana wa Msimbazi na wale wa Jangwani. Najua baada ya kuandika mada hii wapo watu watakuja hapa na kuanza kuhoji kwanini nimesema Simba na Yanga ilhali ligi kuu ya Tanzania Bara inashirikisha vilabu vingi vya soccer. Hivi unaijua nguvu ya vilabu vya Simba na Yanga katika kandanda la Tanzania?

EroCYU1W4AA23b5 (1).jpg


Ni nini kilitokea punde tu baada ya kuahirishwa kwa mtanange baina ya majabali hayo mawili ya soccer hapa bongo? Ni mechi ya vilabu gani hujaza mashabiki wengi uwanjani na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa nchi (Mh. Rais na Waziri husika wa Michezo) zaidi ya mechi ya Simba na Yanga?

Diplomasia ya Michezo inatumika kama sehemu muhimu ya juhudi za kujenga uhusiano wa kudumu kati ya vikundi na makabila tofauti ya watu katika taifa moja. Diplomasia ya michezo hutumia mapenzi ya ulimwengu katika soccer/michezo kama njia ya kuondoa tofauti za kikabila na kidini na kuwaleta watu pamoja.

Tanzania inatumia soccer/michezo katika kuimarisha umoja wa watu wake na kusaidia kujenga ushirikiano na makabila mbalimbali yanayokaribia kufika 120. Hii nayo husaidia kwenye biashara na kukuza uchumi.

images (2).jpg


SWALI: Ni nani alimshauri mama yenu kipendi Rais Samia kuvaa hijab ya Simba?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hivi picha za marais wastaafu (wa kiume), walikuwa wamevaa tai za rangi ipi?

Tuanzie hapo kwanza
 
Hapo mama wala hajavaa hijabu unachoongelea wewe ni USHUNGI uliyofunga kichwa ni MWEKUNDU
HIJAB ni kitu kingine kabisa....
pia binafsi hiyo picha sikuona kama ni nzuri kwasababu mama alikuja kuoneka ana shungi nzuri zaidi ya hii iliyopigwa kwa haraka sana wangetulia tu
 
Duuh leo umekua mvivu saana kuliko siku zote?
Timu ya Simba inatumia bendera yenye rangi mbili...Nyekundu na Nyeupe. Sasa sijajua kama upo sahihi kubadirisha rangi rasmi za timu pinzani
 
Back
Top Bottom