Je, PM ndio Tatizo? Je, ni uhaini kujadili mitandaoni Uwezo wake?

Je, PM ndio Tatizo? Je, ni uhaini kujadili mitandaoni Uwezo wake?

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Ujasusi, Uwezo binafsi wa kuchanbua Na kuchakata Mambo ni Jambo la kuiga hata Kama si kipaji chako

Yapo Makundi mawili yanayoshnikiza PM kuondoka katika nafasi yake nayo ni kama hivi

1.wapinzani , hao ni kawaida kusema fulani aondolewe Na hata mara nyingi maneno Yao uwa hayatishi kwakuwa kameshakuwa ka slogan kao ka Kwamba fulan ajiuzulu haijaanza Leo maana hata ukiwa Na nafasi ukasikia wanasema fulani aondoke Na wanaosema ni wapinzani haishtui Sana aliyekuteua Na wananchi pia maana Neno hilo kwao limetamkwa kwa kila mtu au kila Waziri Kwamba hafai aondoke!

2. Kamfumo ka wapigaji ambako kame Back up agenda Ya wapinzani Kwamba PM aondoke PM aondoke, Haka ni hatari zaidi maana kapo ndani Ya CCM Na Utawala wake narudia Haka ka kundi ni hatari mno maana Baada ya kuona 2025 kama tumewashtukia wakaona angalau basi tupate U PM ili mambo Yao baadhi yaende bila tabu, Usiku kucha ni Vikao mahotelini mpaka video Conference , kuna wanne wametenga ka private Room Club house kujadili how to eliminate Majaliwa, na ubaya zaidi wanapata pa kuanzia ni ndege Ya Precision kuanguka na wakapata Back up zaidi Ya wasmema hovyo wa Neno ajiuzulu

Maoni yangu !

Ninajaribu kuangalia jambo hili katika mtazamo tofauti kidogo na huu wa wao.
Mara zote tunapotafuta suluhu ya jambo tulijifunza kutatua tatizo sio kwa kutengeneza tatizo jingine bali kwa kuhakikisha tumezuia tatizo la aina hiyo.

Ninapoangalia mtazamo wako na wa wengi naona sana uko kwenye utashi binafsi zaidi bila kuangalia Taifa na walipa kodi.... PM anaweza kuwa ni tatizo, lakini tunafikiri hili ni tatizo lake kwa maana ya uwezo binafsi? Au tunaakisi hili katika uwezo wetu na ukomo wetu wa kufikiri? Kwangu sijawahi kuona PM kuwa tatizo hata kama ana mapungufu yake mengi binafsi... Natazama sana katika uhalisia wa mfumo.

Tunapowaza na kushinikiza Waziri Mkuu ajiuzuru tumeangalia mbadala wake? Lakini je tumeangalia mfumo mzima ulivyo na nafasi ya mteule tunayemuwaza kuweza kufikia matarajio na matamanio yetu wengi? Anaenda kufanya kazi kwenye mazingira gani hasa ya watu gani kuweza kufikia hayo matarajio?

Ninawaza sana kuwa labda hatujui tunataka nini, AU tunatumia akili kubwa sana kutengeneza Ujinga.

Kwani kama maamuzi haya ni wazi kutubebesha mzigo walipa kodi, je busara ni nini? Kulinda kodi zetu kwa kutoingiza mtu kwenye mfumo uleule ambao haujaonesha kubadilika au tuendelee kuongeza mzigo kwa walipa kodi kwa kucheza kamari kila mara juu ya matarajio?

Tunapowaza hili leo tumeangalia aina za watu tulionao na uhakika wao? Wamethibitisha wapi kuwa wataweza kutupa tunachohitaji?

USHAURI:
Kwa mtazamo yakini, tunapaswa kuakisi mfumo wetu (Overhaul), haya yote yanayosemwa kuwa makosa ya PM sio tu hayana mantiki ukiyanyambua bali pia yako wazi kabisa kuwa ni ya kimfumo, tusichukue dhana ya kuwajibika kama kitu cha kuturidhisha bali inapaswa kuwa hakika na yatupasa tuangalie maisha katika picha kubwa ya yanayoenda kutokea tukitazama kila pande na kila kitu na sio kuiishi siasa ikituendesha kadiri inavyotaka.

PM ANAWEZA KUWA ANAPWAYA SANA TENA MNO, ILA WHO THE CAP FIT? NA HUO MVINYO MPYA TUNAUTAKA UTAWEKWA KWENYE CHOMBO GANI TOFAUTI NA KILE CHA ZAMANI?

Tusiendelee (Walipa Kodi) kujitia mzigo wa gharama za kuendesha ofisi mpya ya Waziri Mkuu kwa Siasa za bei nafuu bila ya kutumia akili.


Britanicca
 
Dalili za PM kuondoka pale zipo wazi siku nyingi, sababu ndiyo imekuwa ikisubiriwa ipatikane na 2023 akiimaliza bwana Maja ashukuru.

Wapinzani wanachokiongea hawajakiwaza wao Bali kimetoka kule kule aliko PM mwenyewe. PM kama anasoma alama za nyakati ajue nafasi yake ilishatafutiwa mtu siku nyingi na anasubiri tu Kula kiapo.
 
Kwangu kama ikitokea Majaliwa akaomdolewa, basi itakuwa ni kwasababu ya mvutano wa ulafi wa kugombea madaraka ulioko huko CCM, kwasababu tayari nimeshaanza kuona jina la Makamba likihusishwa na uwaziri mkuu.

Hivyo, hizi kelele zinazozuka kila kukicha ni kutoka kwa walamba asali, wakitumia akili kuwahusisha na wapinzani wasiojielewa kuwaaminisha Majaliwa ana mapungufu kadhaa kutokana na matukio yanayotokea, kumbe walamba asali wana ajenda ya siri.

Nimekuwa nikitazama mengi ya yale anayolalamikiwa nayo Majaliwa, chanzo chake kikuu ni Rais, kwasababu Rais amekuwa mtu asiyejihusisha kufuatilia jambo lolote kwa ukaribu, anamuachia Majaliwa mpaka yale yaliyopo nje ya uwezo wake.

Mfano, utendaji wa baadhi ya mawaziri hauridhishi kwenye wizara zao, Makamba na Mwigulu in particular, ajabu, hawa hawalaumiwi, atalaumiwa Majaliwa pekee linapotokea tatizo, hapo ndipo utaona kabisa kuna vita ya chini chini huko CCM.
 
Bahati mbaya kwa sasa hakuna atakaye fikiria hivyo, mfumo uliopo umejikita zaidi kwenye maslahi binafsi na Kuziba pale walipopoteza tangu 2015. Mkuu wa muhimili hana maamuzi ya mwisho hajiamini kwa nafasi aliyoipata hivyo basi muda mwingi anategemea maoni au mitazamo ya 'wakongwe' katika kufanya maamuzi, huu ni Udhaifu mkubwa sana alionao kwasababu 90% ya anaowategemea ni wahanga wa utawala uliopita ambao ulijipambanua kama utawala wa 'wanyonge'. Ndugu. PM siku zake zinahesabika.
 
Kwanza heshima kwako Mzee, Pili ni kweli Pm ana mapungufu tena mengi kuzidi alivyo na kwa kawaida hafai kuendelea, Je ! Unataka kusema kuwa hakuna mtu ambae anaweza kubeba mikoba hii japo akasafisha upofu uliopo leo hii kwa wananchi ?
 
Siwezi kuingilia ugomvi wa Ndugu ila in a nutshell, CCM ni genge la Wapigaji na hawajahi kuwa na huruma na nchi hii hata siku Moja.

Hawa jamaa ni walafi na wako tayari kuuwa, kutesa na kuumiza Ili tu wabakie Madarakani.

Hata akiondoka Kassim ni Yale Yale tu, CCM imejaa Majizi na Wapigaji tupu Mwanzo mwisho.
 
Yeyote anaiyeitetea CCM au Mwana CCM ujue ana maslahi binafsi na mfumo au na mtu mhusika! Lakini chama kama chama hakijawahi kupendwa
 
Kumuacha mtu mbovu madarakani kwa kisingizio cha kukwepa gharama , ni Ujinga usiopimika !
 
Back
Top Bottom