Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Good lesson?but why should we?
 
Just to add few more names Names Kamanda Mawazo, Nassari and few more innocent civilians including Mwananchi’s employee.

 
My blood
Yet more your blood
Shall irrigate our victory...

I don't see my son future in this country....
 
My blood
Yet more your blood
Shall irrigate our victory...

I don't see my son future in this country....
hapafai tena aisee, you can clearly see wanavyofurahi watesi hawa,they are power hungry,watawala wabovu kabisa kuwahi kutokea Tanzania,waliishaiharibu,mioyo ya watu ni mizito mno,huzuni tu
 
Bashite is safe
anatenbea na lundo la walinzi,wanakula bata haoooooo tena ana motorcade kuuubwa kuliko waziri mkuu,ukifika mwanza Igoma anamjengea baba yake hekalu,juzi tu kanunua udongo wenye rutuba wa kumwaga kwenye garden kwa million 6...milango madirisha ,taa na zagazaga nyinginezo kwa milion 54...na baba yake ana roho mbaya kuliko huyo dogo akikuta hata fundi anakunywa maji ya bomba la nje ni timbwili...dogo ana enjoy maisha aisee,pia anamiliki ghorofa tano mtaa wa rwagasore katikati ya jiji la mwanza
 
Sihitaji kuwa mwanasiasa ili nione makosa makubwa ya dunia hii ktk polisi ya TZ. Haya yaliyotokea Dar, ni aibu. Kwa tabia hii ya polisi lazima tuwaeleze wanasiasa wote kwamba, waonyesheni washika silaha wote kwamba hawako juu ya sheria. Binadamu siyo mwema kama utamfanya kuwa juu ya sheria. Tumeona raia wakipigwa hovyo hovyo eti tu kwa sababu askari kaporwa lakini raia akiporwa hakuna anayepigwa. Mtindo huo umewafanya askari kujiweka kundi la kipekee. Naamini wanajielewa kwamba hawatakiwi kuchezewa. Ni miamba.

Kumuua msafiri ndani ya daladala! Risasi hewani, hewa ya usawa wa daladala bado mtu wa ngazi ya juu anasema ni bahati mbaya. Ukishasema ni bahati mbaya unaanza kumuondolea makosa mkosaji. Lakini, mbele ya wazazi wa marehemu haiwezi kuwa bahati mbaya. risasi hairuki yenyewe! Tumeona kila wakati Polisi akiuwawa huchukulia kwamba ni msiba mzito sana kuliko wao wanapoua raia asiye na hatia.

Hisia yangu ni kwamba Polisi hufanya haya yote kwa umwamba kwamba hatuchezewi. Ni kuonyesha kwamba hawawahitaji raia na kama wanasiasa pia watawaona polisi ni kinga yao ya lazima hata ktk makosa makubwa kiasi hiki, basi raia tutakwisha. Siasa zipo, maandamano hayakuanzia TZ, yapo kote. kwa maana hiyo wataendelea kutumia risasi za moto kutawanya waandamanaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…