Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Pasco hebu lete lile bandiko lako kwamba ccm itashinda kwa kishindo hiyo 2020. Je mbinu zitakazoipa ushindi hiyo 2020 ni hizi tunazoziona sasa?
 
Wewe kila kitu ni kutetea tu, uwe na utu hata kidogo basi nawe kuna siku utaonja machungu
Sio natetea hapa ninajaribu kuepusha lilo tokea jana lisitokee na leo na milele katika nchi yetu!
Na nitaendelea kuwaomba wanaharakati na kuwajulisha kuwa katika vurugu hizo MAJAMBAZI na VIBAKA !
WANASIASA wanatetea kitu wanacho kiita haki! LAKINI JAMBAZI ANAKWENDA KUMWIBIA ASKARI SILAHA YAKE AMBAYO ATAITUMIA KUKUUWA WEWE KESHO PAMOJA NA FAMILIA YAKO!

NI HATARI SANA KUJIWEKA KWENYE SITUATION KAMA HII!
Nasisitiza piga kura na kurudi nyumbani kwako kimya!
 
Pole Sana rafiki
 
Sikuzote za maisha yangu nitakua na mashaka na Huruma yako, kutokana na kusoma maandiko yako na kuyafanyia tafakari hata wanangu nimewaambia wawe makini na wewe
 
Kuna risasi zinazotakiwa kupita katika "vurugu"? Hivi, polisi mabomu ya maagizo yakupiga angani ili kutuliza "vurugu" au hata kutumia rubber bullets? Yaani, polisi aelekeze risasi kwenye daladala Halafu huo si uzembe? Duh!
Dala dala gani wewe ndugu yangu!
Kuna dereva wa Dar tena wa dala dala atapitisha gari lake kwenye vurugu?
 
Brother Mayalla, heshima iwe kwako, NA natoa pole kwa familia ya Marehemu, this is a great loose to the family and the nation.

Ni wajibu hapa haki itendeke, lakini tuwe wapenda haki NA wasema ukweli. Kwenye hili ni lazima polisi NA viongozi wa chadema waliokuwepo NA kuanzisha hayo maandamano haramu lazima wawajibike, look at the video and listen carefully to the words used and see when the police cars where arriving the instigations from the Chadema leaders. This has to be thoroughly investigated. We cannot keep loosing our future generations for the benefit of politics
 


..kweli hakuna fidia inayolingana na uhai wa mwanadamu.

..lakini kufungua kesi ya madai dhidi ya Polisi naamini kutapelekea jeshi hilo kujitafakari kuhusiana na mbinu zao za kutawanya waandamanaji.

..lingine ni jeshi la Polisi kulazimika kubeba lawama, na kuomba radhi, kwa kusababisha kifo cha Aqulina.
 
Je sehemu nyingine ya mkurugenzi aliyesababisha ifanyweje?
Kiuhalisia ofisi nzima yaMkurugenzi wanatakiwa kuwajibika juu jambo hili na bila kupindisha maneno, Ofisi ya Mkurugenzi,Chadema...Wamewaangushia Mzigo jeshi letu la polisi ama kwa uzembe wao ama kwa makusudi.maana wamekuwa sehemu ya hili tatizo
 
mh!too painfull!!!binti mzuri katoweka kwa kosa la waliolewa madaraka,VIP polisi hakufa hata mmoja?hapa ndio nnapowachukia watanzania!!!
 
Hilo ni kosa kubwa sana. Hawa polisi wamezoea kuanzisha vurugu. Tunaomba watu wa haki za binadamu walichukulie hili serious.
 
Madaraka yanawafanya wasijali utu...hutasikia hata kiongozi wao mkuu akitoa neno la pole na walisema "afe kipa afe beki lazima wao washinde". Sasa tumeona kweli kafa mtu na hawajali wao cha muhimu washinde. Mawaziri wameacha kazi wanapiga kampeni...wakati polisi wameambiwa na waziri wa mambo ya ndani wasizoee hivi vifo imetokea wameua tena na hayo yanatokea waziri yuko busy kupiga kampeni za udiwani huku akilindwa vilivyo.
Mungu yupo na atatenda kwa muda ufaao zaidi.
RIP Aqulina...
 
Kwa hiyo unataka kuniambia huyo binti aliwekwa target kabisa kama unaanza kuniambia niangalie na sura....!!?Chadema ni chanzo cha uvunjifu wa amani
Na wewe Utoe habari ya Mtulia ndiyo chanzo....thn ndiyo tujadili.!!!Hatuwezi kujadili tu kile unachopenda ukisikie wewe.....
Sitafuti chanzo, nalaani matumizi ya silaha za moto yanayoweza kusababisha vifo. Matumizi ya silaha za moto si jambo la kulipa uhalali kirahisi rahisi hasa kwenye mazingira ambayo raia wa kawaida pia wanakuwepo. Haya makosa ya namna hii hayatakiwi yapewe uhalali sababu maandamano mengine(halali na yasiyo halali) huko mbeleni yatafanywa na watu wa aina mbalimbali, sasa silaha za moto zikitumika kuzuia tutazika wangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…