Je Rais ajaye atakubaliana na katiba pendekezwa?

Je Rais ajaye atakubaliana na katiba pendekezwa?

Sidhani kama mimi ndiye niliyoleta hoja...inasikitisha kuona mtu anayetumia Smartphone kutokuelewa mleta hoja na mchangiaji.kutumia smartphone naona kama ni kigezo kimoja cha kuelewa

Wewe naona umechanganyikiwa na MB 8 zinakaribia kuisha teh teh Smart phone unatumia mwenyewe message sent naona kakuchanganya, hayo ndo madhara ya kushadadia mada usiyoijua!!
 
Najiuliza endapo Rais ajaye akiikataa katiba pendekezwa je anaweza kutengua maamuzi ya Rais aliyemtangulia je sheria inasemaje? Au lazima arudishe mswaada bungeni?
Acha kuwa na dhana potoful kama umetumwa nahc njaainakusumbua, katiba hii imetulia na inamjali kila mmoja, kwanini aikatae? Tumia akili na epuka ushawishi mbaya na upotoshaji kijana.
 
Wewe naona umechanganyikiwa na MB 8 zinakaribia kuisha teh teh Smart phone unatumia mwenyewe message sent naona kakuchanganya, hayo ndo madhara ya kushadadia mada usiyoijua!!

Kwani Smartphone iko vipi kwa namna unavyoelewa wewe.Control yourself kabla hujajibu,kwa kufanya hivyo unaweza kuja na angalau jibu zuri
 
Kwani Smartphone iko vipi kwa namna unavyoelewa wewe.Control yourself kabla hujajibu,kwa kufanya hivyo unaweza kuja na angalau jibu zuri
Nawe kunyuni umetokea wapi wewe? Weka hoja mambo ya simu hayakuhusu hapa
 
Kwani Smartphone iko vipi kwa namna unavyoelewa wewe.Control yourself kabla hujajibu,kwa kufanya hivyo unaweza kuja na angalau jibu zuri

Rudi kwenye hoja iliyomezani,Rais atakekuja ataendwlwza agenda hii ya Taifa hatakua na muda wa kupoteza isipokuwa kukamilisha kazi ilobaki!!
 
Rudi kwenye hoja iliyomezani,Rais atakekuja ataendwlwza agenda hii ya Taifa hatakua na muda wa kupoteza isipokuwa kukamilisha kazi ilobaki!!

Good......Rais ajaye ni lazima afuate sheria za nchi kama anataka kufuata utaratibu wa utawala wa kisheria..kinyume atakuwa Dictator.
 
Good......Rais ajaye ni lazima afuate sheria za nchi kama anataka kufuata utaratibu wa utawala wa kisheria..kinyume atakuwa Dictator.

Kwa muktadha huo tupeane ufahamu tu endapo zoezi la kura ya maoni likifanyika Baada ya Oktoba 2015 baada ya uchaguzi tukiwa tumepata katiba mpya na Rais mpya nini kitafuata??
 
Kuna mengi yakufanywa kama katiba ikipita...kutengeneza sheri na kanuni ili ziendane na katiba mpya na katiba inaweza tumika kikamilifu takriban baada ya miaka minne.kipindi chote kitakuwa mpito chini ya implementation commitee itakayoundwa
 
Tujikumbushe kwa usahihi hapa,Katiba Inayopendekezwa,

IIbara ya 293.- (1) Muda wa mpito utakuwa muda wote kuanzaia tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 hadi kupita miaka 4 baada ya kuanza kutumika kwa katiba hii, Hii ni kuelewa tu lazima kipindi cha mpito kiwepo na huo ndo utaratibu kisheria,hili haliepukiki!

kifungu cha Pili (2) cha Ibara hiyo kinasema Bunge ambalo ndio wawakilishi wa wananchi linaweza, kwa azimio litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge wote, Kuongeza muda wa mpito uliotajwa katika Ibara ndogo ya 1 kwa kipindi kisichozidi miaka 2 ili kukamilisha mambo ya mpito yatakayokuwa hayajafanyika au kukamilika.

KATIKA KIPINDI HICHO CHA MPITO MAMBO YAFUATAYO YATAFANYIKA.

Ibara ya 294. (a) Kurekebisha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.

(b) Kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za Jamhuri ya Muungano, sheria ambazo si za Muungano zinazohusu Tanzania Bara na Sheria za Zanzibar ili kuwiana na mashari ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014,

Haya kifungu C kinaeleza kuanzishwa kwa mahakama ya juu

Kifungu D ni Kuundwa kwa Tume Na Taasisi nyingine za Kikatiba zilizoanishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 na Kifungu E kinaelezea kufanyika kwa kazi ya uteuzi katika nafasi za madaraka kwa taratibu zilizoainishwa kwenye katiba hiyo.

kifungu F ni kufanyika maandalizi ya mambo yote muhimu kwa ajiali ya utekelezajia bara wa masharti ya kikaktiba yaliyomo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaya mwaka 20014.

IBARA YA 295 . Kifungu cha 1 kinaeleza kuwa Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masharti ya sura hii Rais kupitia hati ya uteuzi atateua kamati ya utekelezajia wa Katiba katika muda wa mpito.Kifungu cha 2 kinasema kuwa majukumu ya Kamati ya Utekelezaji wa Katiba yatakua kama yalivyoanishwa katika hati ya uteuzi.

IBARA YA 296 inaweka wazi kuwa baada ya kumalizika kwa muda wa mpito, masharti ya sura ya 9 yatakoma na hayatakuwa na nguvu ya kisheria.

YAANGALIE MASHARTI HAYO YATAKAYOKOMA YA SURA YA 19 AMBAYO NDO MTOA HOJA PASIPO KUELEWA AU KWA MAKUSUDI AMEAMUA KUPOTOSHA SOMA IBARA ALIZOZITAJA NA MIMI NAMUONGEZEA NYINGINE KUANZIA YA 282 , 283 , 284 ,285 na kuendelea kwenye sura yote yatakoma.

Mwisho kwa kuyazingatia haya Bakishuu nipe uhalali wa hoja iliyopo mezani na vifungu vitakavyo tumika facilitate jambo hilo!!
 
Kama yote uliyo andika yapo katika sheria husika basi hamna budi yafuatwe.
 
Kama yote uliyo andika yapo katika sheria husika basi hamna budi yafuatwe.

Issue hapa ni Rais atakayekuja kama yuko against na hii process je ataweza kutengua maamuI ya Rais alyemtangulia???!mtoa hoja kaandika hoja hii as if jambo hili ni la Rais akasahau kuwa suala hili lipo kisheria!!Je hapo unasemaje nipe majibu mkuu!!
 
Mimi naona uko sahihi,hii nchi siyo ya Rais bali Rais tumempa majukumu ya kutuongoza.Rais atakayekuja madarakani anawajibika kufuata yote yaliyopitishwa na bunge la wananchi
 
Mimi naona uko sahihi,hii nchi siyo ya Rais bali Rais tumempa majukumu ya kutuongoza.Rais atakayekuja madarakani anawajibika kufuata yote yaliyopitishwa na bunge la wananchi

Hoja hii imekaa kisheria zaidi sijui mtoa hoja alikua na maana gani?au uelewa wake juu ya jambo hili ulikuaje?tungempata akarudi hapa kusema ili tupate cha kushare!! Ila kwa uelewa wangu alifikiri kuwa Rais wa nchi ndio kila kitu, unaweza kuamua mambo kienyeji bila kufuata sheria, mambo haya ni magumu hasa siasa zikiachwa zikaingia, RULE OF LAW must prevail hapa, Rais atakayekuja no matter awe wa chama gani CCM AU UKAWA atalazimika kufuata sheria za nchi zilizopo!!
 
kwa taifa hili nchi ni raisi kumbuka raisi kapewa madaraka makubwa sana na hamna wa kumshtaki nadhani tumekosea kwenye mfumo katiba bila mfumo nisawa na bure.
 
kwa taifa hili inawezekana kumbuka raisi kapewa madaraka makubwa sana na hamna wa kumshtaki hata kama akiikataa nadhani tumekosea kwenye mfumo katiba pendekezwa bila mfumo nisawa na bure.
 
kwa taifa hili inawezekana kumbuka raisi kapewa madaraka makubwa sana na hamna wa kumshtaki hata kama akiikataa nadhani tumekosea kwenye mfumo katiba pendekezwa bila mfumo nisawa na bure.

Umeielewa hoja lakini? Hapa hakuna ushabiki wa siasa?narudia tena umeielewa hoja???
 
Back
Top Bottom