Je Rais ajaye atakubaliana na katiba pendekezwa?

Je Rais ajaye atakubaliana na katiba pendekezwa?

Tanzania inaongozwa chini ya utawala wa sheria Na si kwa kupiga ramli chinganishi!kwa kuwa rais ajaye lazima atazingatia utawala wa sheria na atakuwa amepokea kijiti cha kazi ataendelea kufanya kazi na pia si pekee yake!sasa swali lako unadhan Urais ni MAAMUZI ya Mtu mmoja!na pia hiyo katiba yenyewe ni suala ambalo ni la kitaifa sasa ni kuulize wewe kwanini unafikiri kukataliwa kwa katiba na rais ajaye?ama wewe ndo umeikataa?acha ubashiri wa mawazo yako mwenyewe
 
Sheria iliyoestablish mchakato hawaijui, naona mtoa mada anafikiri suala la upatikanaji wa Katiba ya nchi ni matakwa ya mtu mmoja,ingekua hivyo mbona fasta tungekua tumeshapata hiyo katiba!Tujifunze kusoma na kufuatilia tusilete mihemuko na mapenZi ya vyama ambayo hayana msingi hapa!
 
Najiuliza endapo Rais ajaye akiikataa katiba pendekezwa je anaweza kutengua maamuzi ya Rais aliyemtangulia je sheria inasemaje? Au lazima arudishe mswaada bungeni?
Aikatae kwa baya gami lililopo ndani ya katiba hii nzuri? Hawezi kufanya hivyo maana atakuwa mtu mwenye busara!
 
Mabadiliko yoyote au jambo lolote kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya litafanywa kwa kuzingatia sheria na wala si matakwa ya mtu!
 
mbona wameshashinda hata kabla ya uchaguzi

Kwa matakwa yako wewe wawajua hao washindi. Ila kwa matakwa ya kisheria ambayo ndiyo msingi wa maamuzi wa mambo yote ambayo Tanzania inasimamia, ipo Tume ya Uchaguzi ambayo ndiyo wenye mamlaka kusimamia hilo. Wote tu mashahidi uchaguzi mkuu wa Tanzania ni Oktoba 2015. Uongo huo BOKO HALALI ameutoa wapi? Acha piriri piriri zako wewe!
 
Kwa upande wa rais ccm haina mpinzani upinzani utakuwa kwenye udiwani na ubunge
 
Kwa upande wa rais ccm haina mpinzani upinzani utakuwa kwenye udiwani na ubunge

Sala ya Watanzania ni kupata viongozi watakaolifikisha taifa kwenye malengo ya nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Masuala mengine acha utaratibu uitwe utaratibu na ufuate utaratibu ili mambo mema yenye kuratibiwa kiutaratibu kwa mujibu wa sheria na taratibu zake yafuate mkondo wake. Wewe na mimi tutekeleze wajibu wetu wa kupiga kura na kuchagua viongozi hao ambao tunatarajia kuwapata kwa njia ya uchaguzi 0ktoba 2015.
 
Lowasa kama anataka uraisi na ashinde kwa kishindo basi awaahidi watanzania rasimu ya Warioba ndiyo itakayopitishwa. Maana bila hivyo hawezi kuibadilisha nchi kwa utawala huu na viongozi hawa hawa

Kweli akili zako hamnazo.....warioba alipeleka mapendekezo kwenye bunge maalum la katiba lililoundwa kisheria na kujumuisha makundi yote katika jamii ikiwamo wanasiasa wote(wabunge),hawa ndio wenye jukumu la kutunga katiba...kingine unajua ni vitu vingapi vilivyoachwa kwenye rasimu ya warioba....acheni ubinafsi usiokuwa na maana...kama warioba aliona wasanii,wakulima na wanawake hawana haki kikatiba basi bunge maalum liliona kuna haja ya baadhi ya mambo muhimu kwenye makundi hayo kuwemo.....coz wao pia wanahaki hiyo..tena wasanii ndo walitia huruma hawakuwepo kabisa kwenye rasimu ya warioba...si uwehu huo...ACHENI MIHEMKO YA KISIASA NA KUFUATA MKUMBO BILA KUJIELEWA
 
Tunataka Rais ajaye ahitimishe issue ya katiba mpya, katiba pendekezwa iliyopitishwa ifanyiwe marekebisho tena ili mambo makubwa na ya msingi ambayo wananchi wanayataka, hasa kurekebisha utawala bora, yarejeshwe.

Kazi ya Rais na watendaji wengine itarahisishwa sana endapo katiba iliyopendekezwa na kupitishwa kibabe hasa kupuuza maoni ya wananchi itarekebishwa bila woga na kwa kuangalia maslahi mapana ya Taifa, sio kikundi kidogo cha watawala. Mungu atusaidie.
 
Rais ajaye ni wazi atakubaliana na mchakato uliopo maana hata kwenye kampeni zao sijawasikia wakipinga jambo hili.
 
Back
Top Bottom