GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #21
Mkimminya Kende ( Pumbu ) zake ndiyo mtakuwa mmetatua tatizo la Kimsingi?Siku ukija kuminywa ndeke zako kwa kumtukana Rais katika kila thread akili itakurudia sawa
Sasa kama Kuua Watu, Kuwatishia na hata Kuwatesa mlidhani kuna Tija mbona bado Watu wanafunguka tu?
Nitafutie duniani Taifa ambalo limeminya Uhuru wa Watu Kujieleza na kutoa Hisia zao kwa Uozo wa ama Marais wao au Serikali zao limekuwa na Amani au Maendeleo.
Kiongozi ukidhihakiwa au Serikali ikidharauliwa ni Jukumu la Mhusika au Taasisi husika ' Kujitathmini ' kwa Kina na ubadilike.
Yaani mnaacha Kufanya Kazi ya Kumsaidia Rais Kujenga na Kurekebisha Kasoro mpo ' busy ' kuja Kutishia Watu Mitandaoni kama ulivyofanya.
Hamjakoma tu Mtishaji Mkuu Mwenzenu wa Maisha ya Watanzania Yeye kaondoka zake lakini ' Watishiwaji ' tuliotukuka ' tunadunda ' zetu tu duniani huku wengine hata ' Mkituua ' leo tutawashukuruni kwani Mawazo na Mabandiko yetu ya Ukweli na Haki yatabaki Milele na katika Vizazi mbalimbali vya Watanzania.
Mkipatia akina GENTAMYCINE tutawapongeza na tumekuwa tukifanya bila kuhitaji ' favors ' zozote za Kipesa au Uteuzi kutoka Kwenu ila mkikosea ( mkikengeuka ) tu katika Utendaji wenu tutawasemeni ( tutawasilibeni ) hapa hapa ili mbadilike.
Ninachukia sana tabia za Kutishia Watu.