Bado hujaelewa vyema mkuu
DR Mambo AMP .
Unachanganya MUSWADA na SHERIA.
Pia unachanganya tarehe za kupitishwa rasmi kwa hizo instruments mbili respectively.
Sasa tuliza akili vizuri, unisome tena Kwa umakini hapa chini. Utaelewa tu...
1. MUSWADA ni nini?
MUSWADA ni 'mapendekezo' ya kuanzisha Sheria mpya, au 'mapendekezo' ya kubadili/kurekebisha/kuboresha Sheria iliyopo.
Bunge ndiyo chombo pekee chenye dhamana na mamlaka ya kujadili MUSWADA na kuupitisha au kutoupitisha kuwa SHERIA.
Katika kutimiza jukumu hilo, Bunge laweza kuyapitisha mapendekezo yote ya MUSWADA kama yalivyowasilishwa; ama kupitisha mapendekezo baadhi tu; ama kutopitisha/kuyafuta/kuyakataa mapendekezo yote; ama kuyarekebisha kwa kadri Bunge litakavyoona inafaa kwa manufaa na ustawi wa nchi.
2. Kiutaratibu na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, MUSWADA ni lazima kwanza utangazwe kwenye Government Gazette, kwa siku 21, kisha ndipo uwasilishwe Bungeni.
Hivyo, MUSWADA husika ulikuwa Gazetted rasmi tarehe 15 MAY 2023.
View attachment 2733314
3.0 MUSWADA huu ulikuwa na mapendekezo ya kubadili/kurekebisha vifungu kadhaa vya Sheria ya TISS ya mwaka 1996. Mapendekezo hayo yanajumuisha marekebisho katika "kifungu cha 6" ambacho sasa ndiyo basement ya andiko lako kwenye uzi huu.
View attachment 2733516
3.1 Katika hii "Section 6", mapendekezo ya marekebisho yalikuwa matatu: Kuongeza subsection 2 mpya (pichani 'A'); Kuongeza subsection 6 mpya (pichani 'B'); na Kuondoa baadhi tu ya maneno kwenye subsection 5 iliyopo ya zamani (renumbered as 7) (pichani 'C').
View attachment 2733540
Hapo kwenye pendekezo la 'subsection 6' mpya (pichani 'B') ndipo ilipo hoja yako kuu ya uzi huu.
3.2 MUSWADA huu sasa ukawasilishwa Bungeni rasmi kwaajili ya mchakato wa kuyajadili mapendekezo yake yote ili upitishwe ama usipitishwe.
4.0 Bunge likahitimisha kazi yake. Kisha Bunge likaupitisha rasmi MUSWADA huu mnamo tarehe 8 JUNE 2023.
View attachment 2733576
4.1 Specifically katika SECTION 6, Bunge likawa limepitisha mapendekezo mawili tu: Kuongeza subsection 2 mpya (pichani 'A'); na Kuondoa baadhi tu ya maneno kwenye subsection 5 iliyopo ya zamani (pichani 'C').
View attachment 2733594
Huu sasa ni MUSWADA officially passed by the National Assembly (Bunge). Hayo ndiyo mapendekezo yaliyopitishwa na Bunge kuirekebisha SECTION 6. Lile pendekezo la Kuongeza Subsection 6 mpya, halipo. Halikupitishwa.
5.0 MUSWADA wowote uliopitishwa na Bunge, ili uweze kuwa Sheria kamili ya nchi, ni lazima kwanza Rais aupe kibali kwa kusaini.
MUSWADA huu ukawa umesainiwa rasmi na Rais Samia mnamo tarehe 5 JULY 2023.
View attachment 2733629
Kuanzia tarehe hii Rais aliyosaini, nyaraka hii sio MUSWADA tena. Ni Sheria kamili.
6.0 Sheria yoyote inaposainiwa na Rais, ili iweze kuwa enforceable na kutumika nchini, ni sharti kwanza Sheria hiyo iwe Gazetted, yaani umma utangaziwe kuwa sasa kuna hii Sheria mpya ya nchi.
Sheria hii ya Marekebisho ya Sheria ya TISS, rasmi ikatangazwa kwenye Government Gazette, mnamo tarehe 14 JULY 2023. Kuanzia tarehe hii, tayari Sheria hii ya Marekebisho (ACT SUPPLEMENT) ikaanza kutumika nchini Tanzania.
View attachment 2733650
6.1 Hivyo basi, kwa muktadha huo, maboresho/Marekebisho ya Sheria yaliyofanywa kwenye KIFUNGU CHA 6 cha Sheria ya TISS, weweza kuyang'amua kiurahisi kwa kusoma hizi picha mbili tu hapa chini:
A) Sheria Kuu ya TISS (PRINCIPAL LEGISLATION) ya mwaka 1996. Section 6:
View attachment 2733662
B) Sheria ya Marekebisho (ACT SUPPLEMENT) ya Sheria ya TISS, mwaka 2023. Section 6:
View attachment 2733697
--------------------------------------
SECTION 6 ya Sheria ya TISS imefanyiwa law reform kwa taswira hiyo. Pendekezo la Subsection 6 mpya halikupitishwa na Bunge. Wiped out by the National Assembly.
As such, Mh Rais Samia hajavunja Sheria ya TISS Kwa kumteuwa ex DG ndugu Massoro kuwa mtumishi wa umma kwa nafasi ya ubalozi.
Cc:
Richard .
-Kaveli-