Ukisikiliza hotuba zake JPM kwa umakini sana, utagundua jinsi alivyokuwa anaiona hatari ya Kuuliwa. Hata mimi kwa uelewa wangu mdogo wa security nilikuwa nishaanza kunusa hiyo hatari ya kifo chake.
Sasa inakuwaje TISS ambao wamepewa dhamana ya kumlinda masaa 24 wasiweze gundua hatari iliyokuwa inamkabili? inaelekea hiyo taasisi imejaa watu wasio sahihi na wasio na uzalendo kabisa. Na watakuwa wanaitumia hiyo taasisi Vibaya.
Katika uongozi wa Tanzania, ukiwaangalia marais 6 utagundua kuna makundi 2 yenye style tofauti za uongozi. Kundi la kwanza ni viongozi wenye msimamo mkali wa raslimali za nchi ambao ni Nyerere, Mkapa na Magufuli. Wote walikuwa wazalendo kwa nchi yao na wameleta impact kubwa sana nchini. Walikuwa wanatetea raslimali za nchi na walikuwa hawacheki na mabeberu. Na wote watatu vifo vyao ni vya utata utata.
Kundi la pili ni ili kundi la viongozi wenye msimamo soft soft ambao ni Mwinyi, Kikwete na Samia. Wote hawa misimamo yao sio mikali hasa hasa kwenye raslimali za nchi. Mwinyi alikuwa mzee wa ruksa, Kikwete mzee wa bata na Samia mmemsikia akiamuru madini yachimbwe, wafanya biashara waachwe hata wakihujumu uchumi na kadhalika. mitazamo yao ya uongozi iko tofauti kabisa na kundi la kwanza.
Hii inatuonesha kwamba viongozi wenye msimamo mkali kwenye raslimali za nchi wanauliwa mapema sana kwani wanakwamisha mipango ya mabeberu kuiba raslimali za nchi. Na kiongozi mwenye msimamo mkali hata TISS hawawezi kumlinda.
Kama ukiwa rais na ukalegeza msimamo wako kwa mabeberu, basi utakuwa umejisalimisha na mabeberu hawatakuua, kwahiyo kazi ya TISS kukulinda itakuwa raisi kwao kwani hutadhulika.
Swali la kujiuliza, kama moja ya kazi ya TISS ni kuhakikisha vongozi wako salama, sasa ni kwanini viongozi wanauliwa kwasababu ya kulinda na kutetea raslimali za nchi?