Huyu mama ni mzalendo sana kwa nchi yake ya Zanzibar lkn hana uchungu hata chembe na Tanganyika . Anaipenda sana Zanzibar na anawapenda wazanzibari kiasi kwamba mpk anaonesha upendeleo wa wazi wazi.
1. Angalia jinsi alivyoingilia suala la Fatma Karume kupokwa uwakili.
2. Angalia alivyoingilia mgogoro wa Feisal na Yanga.
Zanzibar kuna ujenzi wa miundombinu usioendana na pato la kisiwa hicho.
1. Ujenzi wa flyovers kwenye kila barabara.
2. Majengo yote ya skuli, zahanati na hospitali kubadilishwa kuwa maghorofa.
3. Ujenzi wa bandari kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na kati...bandari ya Mangapwani.
4. Ujenzi wa viwanja vikubwa vya ndege.
5. Ujenzi wa viwanja vikubwa vya michezo.
Kwa makusanyo yapi ya Zanzibar? Kwa shughuli ipi ya kiuchumi ya wazanzibari?
Huku Tanganyika, bandari, mbuga na migodi ya madini vinauzwa kwa waarabu lkn huko Zanzibar mama hajauza hata unyasi.
Ktk kipindi ambacho wazanzibari wamekuwa watulivu kuhusu muungano na wamekuwa wamoja ni kipindi hiki. Kwasabb waliyemtuma kuchuma anachuma kweli kweli. Husikii tena madai ya mamlaka kamili ya Zanzibar wala koti la muungano kubana.
Huku bara kuna utekaji, mauaji na vurugu za kisiasa, mama anachojali ni kuwa anachuma. Hana habari na maisha ya watanganyika. Mapadri wanapigwa, makanisa yanafungiwa na wapinzani wanafungiliwa kesi za kubumba yeye ndiyo kwanza anakejeli.
Watanganyika tuendelee kushupaza shingo tu, watoto na wajukuu wetu watakula mawe .
NIMEMALIZA.