Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Kwa akili gani walizonazo kuwa wao wajichukulie tu maamuzi ya nchi zote bila ya kushauriana na wengine?
 
Mkuu huyo dada yetu mchukulie poa tu, Sijui kadanganywa na nani kabisa hizo pumba, msamehe tu
 
Kwa akili gani walizonazo kuwa wao wajichukulie tu maamuzi ya nchi zote bila ya kushauriana na wengine?
Mkuu mwaka 1964 nchi hii ilikuwa bado ni pori.

Hakukuwa na hizi taasisi za kidemokrasia kama za leo. Pia nchi changa zilikuwa haziwezi kupinga matakwa ya wakoloni.

Tukijiweka katika nafasi za Nyerere na Karume ndio tunaweza kuelewa maana ya maamuzi ya kuwa na muungano.
 
Kushindwa hata kushauriana na Mabaraza ya mawaziri?

Hawa walikua ni Madikteta tu mkuu, acha kuwatetea
 
Kushindwa hata kushauriana na Mabaraza ya mawaziri?

Hawa walikua ni Madikteta tu mkuu, acha kuwatetea
Ndio maana nikakwambia dunia ile sio hii ya leo.

Kumbuka kulikuwa na ushawishi mkubwa wa mataifa yaliyotutawala na tulikuwa ndio tunaanza kujitawala. Hizi taasisi Za leo hazikuwepo, hao wasomi wenyewe hawakuwepo sembuse wenye mawazo yenye kuweza kuleta tija za kitaifa!.

Halafu visiwani na huku bara watu ni wale wale asili zao ni zile zile usidanganywe na hizi serikali ukadhani watu ni tofauti.

Waliojaa unguja na pemba ni wamakonde, wanyamwezi na watu wa asili ya mwambao wa pwani.
 
Kuwa ni watu wenye asili moja sio hoja ya kulazimishwa kuwa lazima wawe taifa moja
 
Unakimbia uhalisia mkuu, Nyerere na Karume walikua na madikteta. Sijui kwa upande wa bara Lakini Zanzibar kulikua na wasomi wa kutosha wakutoa maarifa na wengi walionekanwa wazi kutokubaliana nalo tokea mwanzoni. Jaribu kusoma historia vizuri.
 
Afrika yote ya miaka ya 1960 wakati wa kupatikana kwa uhuru iliongozwa na viongozi madikteta. Tatizo mimi na wewe hatukuwepo duniani.

Ukiwasikiliza waliokuwepo kwa maana ya Baba na Mama zetu utaelewa ni kwanini iliwabidi wawe madikteta.
 
Hakuna sababu za msingi Zaidi ya uchu wa madaraka na kujiona bora kuliko wenzao
 
Acha ubaguzi kijana. Kumbuka ukaribu uliopo kati ya Tanga na Pemba, kati ya Dar na Unguja.

Hivi mtu kudai haki yake nalo ni ubaguzi?

Je pia unakumbuka ukaribu uliopo baina ya TZ na Kenya au Uganda mbona hakuna muungano wa nchi?
 
Mara zote wanaotaka muungano uangaliwe upya huwa natamani kupata na kujua hatima ya nchi yao yaani Tanganyika. Nikiwa mtanganyika ambaye nafanya kazi Zanzibar nachelea kusema ukiwa huku ndo utajuwa kwa undani kuwa kuna Tanganyika. Kwa nini ikiwa wewe ni meneja ukamwajibisha mfanya kazi usishangae kuona kamati nzima nzima ya ulinzi na usalama asubuhi imehamia ofisini kwako. Hoja wanayokuja nayo ni nyepesi tu kuwa hutaki kufanya kazi na wazanzibar.
Kitachofuata utafuatilia mara utaambiwa siyo mtanzania na hapo ndo utashangaa kuona mzanzibar anahoji Uraia wa Mtanzania.
Ukitoa tenda kwa kampuni yenye makao yake bara utashangaa.
Maajabu zaidi ni pale utakapokamatwa kwa kuendesha gari ukiwa na leseni ya jamhuri ya muungano ili hali polisi anayekukamata amevaa crown ya jamhuri ya muungano nawe leseni yako ni ya jamhuri ya muungano. Ukiuliza hapa niko wapi? Siko ndani ya jamhuri ya muungano? Utaambiwa leseni si suala la muungano, lkn ukirudi kwenye mambo 22 ya muungano kuna usalama, polisi na usafirishaji. Leseni inaangukia kwenye hayo yote.
Huu muungano una mashaka matupu,
 
Hivi mtu kudai haki yake nalo ni ubaguzi?

Je pia unakumbuka ukaribu uliopo baina ya TZ na Kenya au Uganda mbona hakuna muungano wa nchi?
Unapoteza muda wako kudai haki ambayo hutakuja kuipata. Kwa ufupi kubali yaishe.
 
Hicho ni kiburi kinakusumbua mkuu, Dunia haipo hivo kabisa. Lolote linaweza kutokea ndani ya dunia.
Rais Samia anayo haki ya kuiongoza Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Amezaliwa Unguja ambako ni sehemu ya Tanzania.

Na leo kakabidhiwa CCM yenyewe. Mada nyingine ni kupoteza muda tu.
 
Tunalalamika sn km muungano umeanza leo.
 
Kiukweli Tanzania bara hatukuchulia hili serious ila sasa katiba imetupiga ndo tumeshtuka, iweje ss tusiwe na haki yoyote kwenye serikali ya smz ila wao wawe la loophole ya kutuongoza. Hapa umuhimu wa katiba mpya unahitajika.
 
Ningependa kujua hili.

Mh rais Samia ni raia wa nchi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…