Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Mungu wangu...

Sikujua hela ya Tanganyika inaenda kununua meli za Zanzibar
 
Usinipangie cha kufanya, hii nchi ni yetu sote.
Kwani ni nani aliitisha referendum kuhusu muungano wetu kupata popular puplic opinion? Yupo?

Tanzania ya 1961 sio ya sasa, wengine hatukuwepo, tuna haja ya kuhoji
Nikuulize swali dogo tu, Ulishawahi kwenda Zanzibar hasa pale unguja na sio kule pemba na ukakaa japo mwezi mmoja? Ukinijibu hili ntakuuliza lingine
 

Iko hivi, hatuwezi kuacha kuhoji mambo ya muungano kwa vitisho kutoka Serikalini.

Jambo la msingi tuhoji kwa hekima na busara. Kwani huu Muungano umekua Biblia au Msahafu kwamba usihojiwe??

Huyo VP mwenyewe ametokana na Katiba ambayo ndiyo tuna raise query zake hapa.

Uzalendo sio kuogopa kuhoji mapungufu yaliyopo waziwazi.

No, Never
 

Hakuna anayempinga Mama kutawala, jielekeze kwenye hoja. Je? Kuna mahala nimeongea uongo?
 

Hoja yako ni mufilisi. Huwezi kutenganisha Urais alioupata Samia bila kuweka Uzanzibari wake.

Katiba imetamka, Rais akifariki, Makamu( ambaye ni lazima atoke Zanzibar) anarithi kiti. Sasa unatenganishaje haya mawili.

Lakini hoja yangu sio Samia kuwa Rais wa JMT. Hoja yangu ni Samia kuongoza mambo ambayo siyo ya muungano as per constitution. Over!!!!!
 
Ndiyo maana nyie “Team Bashiru”, mulitaka mama SSH asiapishwe kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Sasa ndiyo nimegundua kwanini mulitaka kufanya hivyo.

Hata hivyo, ingekuwa kinyume cha katiba kumpa urais speaker Ndugai au waziri mkuu Majaliwa kama tetesi zilivyokuwa zikisema. Nadhani tulitizame hili mama ongoze kama taasisi na siyo kuanza ubaguzi. Kama ni marekebisho, katiba mpya inaweza kusaidia kuyapata.
 

Hoja ni kwamba, Tumekubaliana kuungana kwenye (mf.) Mambo ya Nje na Uhamiaji, lakini mambo ya Ujenzi na Maji hatujakubalina kuungana.

Sasa Iweje zao la muungano kutoka upande wa pili wa muungano aje kuongoza kwa mambo ya Ujenzi na Maji ambayo siyo ya muungano?

Mantiki iko wapi hapa??? Nn shida kuelewa hoja hii
 
Yeye kuwa zao la muungano haimpotezei uhuru wake wa asili wa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano.

Alipokuwa makamu wa rais hakuwa na huo uhuru wa kushughulika na masuala yote kwa ujumla wake?.
Halafu Mama sio rais wa kwanza kutoka Zanzibar.
Haya maswali ya kipuuzi yana toka wapi leo?
 
Yeye kuwa zao la muungano haimpotezei uhuru wake wa asili wa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano.

Alipokuwa makamu wa rais hakuwa na huo uhuru wa kushughulika na masuala yote kwa ujumla wake?.

You could have raised that query by then, ila kwa sasa usinipangie cha kuuliza. Baki kwenye hoja yangu, ila usinipangie cha kuuliza sasa au kwa nini sikuiliza kabla.
 
Samia Suluhu Hassan ataongoza Tanzania kama ambavyo Mzee Ali Hassan Mwinyi alivyoongoza. Wote wana asili ya Zanzibar.

Hoja hii ingekuwa ya mjadala murua na mashiko kama ingetolewa wakati wa enzi zile za Mzee Rukhsa..kwa sasa imepitwa na wakati! Vinginevyo watu wanasumbuliwa na husda, kijicho na hiyana tu!
 

Poor minds discuss’ people/ personalities, intelligents discuss’ issues, i think you belong to the prior
 

Sasa una hakika gani kwamba nilikuwepo kipindi cha Mzee Ruksa? Au, what if IQ za watu wa sasa zimeongezeka kuliko kipindi chenu hicho?

Kama wewe mtu mzima hukuwa na akili za kuhoji kipindi hicho ukiwa kijana, ndo hutaki sisi vijana wa sasa tuhoji?

Oooh please!!!
 
Kwanza nikurekebishe kitu kimoja, Tanganyika haijawahi kufutwa, na kama ilifutwa ni kwa Sheria gani na ya mwaka gani? Na hili ndio moja kati ya kero kubwa la Muungano wanalolilalamikia Wazanzibari kua Tanganyika ndio hio hio Tanzania. Sasa kama kweli Muungano huu una nia njema, ilikuwa mulione hilo Tokea mwanzo, kuwa jee ikitokea Raisi anatokea Zanzibar si Atakuwa anaendesha Mambo ya Tanganyika ambayo hayamuhusu. Lakini waswahili husema ukificha Chongo iko siku utaadhirika tu maana utapewa Barua usome na macho hayaoni. Kifo cha Magufuli kimewaweka Uchi, mulidhani Wazanzibari watabakia na Umakamo mpaka dunia imalizike. Sasa Option ni Mbili aidha Mukubali matoke mumuachie Mama Samia aongoze kama anavyopenda, au Badilisheni Katiba Zanziba iendeshe Mambo yake, na Tanganyika iendeshe ya kwake na Tukutane kwenye Bunge la Muungano, na Uraisi tutapokelezana kwa zamu
 
Unafiki wa Watanganyika hasa wana green ndiyo tatizo kubwa. Kila zilipo kuwa zikiletwa hoja za maslahi ya Tanganyika, watu walikemewa na kufungwa midomo. Watu hawa wliamini Zanzibar ni koloni la Tanganyika, na hawakutaraji kama kuna siku Rais atatoka Zanzibar.
Sasa mambo yame badilika. Hoja hizi hazitokani na nia ya kweli ya kuboresha muungano au kuhitaji uwepo wa Tanganyika, bali ni choyo na uroho wa madaraka. Kitumbua kimeingia mchanga.
Hayati mtikila alihubiri juu ya udhaifu wa muungano waziwazi lakini aliishia kuoneka mwehu.
 
Hakuna anayempinga Mama kutawala, jielekeze kwenye hoja. Je? Kuna mahala nimeongea uongo?
Wewe unajikanganya hapa, kama unasema hakuna anayepinga Bi Mkubwa kutawala Tanzania hii hoja kwa nini umeileta hapa? Na kwa nini umeileta baada ya kifo cha Dikteta ?, na kwa nini hukuleta hoja sababu ipi CCM imemteua VP mwenye asili ya zanzibar, je ulikuwa hujui kama Rais atashindwa kutimiza majukumu yake kwa ugonjwa au kifo makamu wake ndiye ataapishwa kuwa Rais. Wewe hilo ulikuwa hulijui? Na kumbuka katiba ya mzee warioba ilipendekeza mfumo wa serikali tatu lakini haikupendekeza asili ya mtu ametokea wapi sababu ya kuepusha ubaguzi, kumbuka pengine labda utoto tu unakusumbua kule Zanzibar Raia wengi wana asili ya Bara ambao walipelekwa kulima mashamba ya karafuu pemba ambayo yalimilikiwa na waarabu. Kifupi Mwl. Nyerere ndiye aliyemshawishi Hayati Mzee karume waungane baada ya karume kuomba msaada wa kuunganisha tabaka mbili la wapemba na waunguja ambao wana asili ya bara, suala la vita baridi ilikuwa ni kisingizio tu. Na baada kuondolewa utawala wa sultan Jamshid bin Abdulla mwaka 1963 Mzee karume aliwataka Wazanzibar weusi na weupe (waarabu) waoane ili kuondoa chuki baina yao iliyotokana na kukandamizwa kwa watu weusi. Hivyo kwa muktadha wa huko tulikotoka hakuna mtu anayeitwa mzanzibar wala mtanganyika wote sisi ni waTz. Hoja yako haina mashiko bali unataka kutugombanisha
 
Poor minds discuss’ people/ personalities, intelligents discuss’ issues, i think you belong to the prior
Aren’t you discussing Samia instead of the president as an institution? I don’t wanna argue with a fool. This one is a jab under a belt.
 
Hoja iko wazi na inahitaji wachangiaji
Tatizo jukwaa naona limepungukiwa na watu wafuatiliaji wa mambo na wenye kuijua historia na katiba ya nchi.
Lakini kutwa wakidai katiba mpya ili hali iliyopo hawaijui.
Kwa upande wangu nakiri kabisa kuwa, licha ya ueledi mkubwa wa baba wa taifa Hayati Mwl. JK Nyerere aliokuwa nao lakini kuna sehemu alifanya pasipo kujua madhara yake hapo baadae ijapo siwezi kulaumu sana kwani huenda alikuwa na nia njema tu kwa wakati huo.
Suala la katiba hususani upande wa mambo ya Muungano, kuna pahala sijui alizidiwa kete na Mzee Karume ama ilimbidi tu akubaliane na baadhi ya vipengele kwa sababu aliihitaji sana zanzibar minimume na zanzibar kutuhitaji sisi zaidi. Ndipo akajikuta anakubaliana na huu uwenda wazimu wa baadhi ya vipengele vilivyomo ndani ya katiba.
Moja ya mambo ya hovyo kabisa pamoja na
1. umiliki wa ardhi, ajira za umma ikiwa ni pamoja na mamlaka za juu za serikali, 2.kodi na ushuru bandarini, mgawanyo wa mapato kwa usawa ili hali kuna tofauti kubwa ya idadi ya watu baina ya hizi pande mbili,
3. uwekezaji,
4. mamlaka ya uongozi wa zanzibar kwa maana ya kiti cha rais,
5. Vitambulisho vya kitaifa,
Mimi nafikiri huu muungano inaonekana wazi kabisa kuwa watanganyika ndio tunaoutaka zaidi kuliko kwa wazanzibar wenyewe na ndio maana wanaendelea kutunyonya zaidi pasipo usawa ili pengine tusalimu amri wenyewe na tuwaachie kisiwa chao wajitawale.
Hata hivyo Mama inaonekana kabisa kuwa anataka atumie mamlaka aliyo nayo kwa sasa kuinyonya Tanganyika vilivyo kwa kufanya mambo pasipo kuzingatia uwiano wa idadi ya watu baina ya hizi pande mbili za muungano.
Hata hivyo sisi watanganyika imefikia hatua sasa ya maamuzi magumu ya kujitoa katika pingu hii ya kinyonyaji ya muungano na tuwaache wajitawale wanavyotaka wao na sio kuendelea kutuona machoko tusiojitambua kwa minyororo ya baba wa taifa.
Haileti sensi mzanzibar anakuwa Rais wa JMT ili hali hajui ata tamaduni z mtanganyika na kero zake,
Anakuwa DC, RAS, DED huko karagwe, musoma ama Maswa kweli, hivi huyu anayajua matatizo ya msukuma, mjita, mkurya, mhangaza kweli? Uongo mbaya,
Ndio maana ata yeye Mh Rais SSH hana mda tena kudhurura kujichosha na na Watanganyika asio kuwa na maslahi nao.
Hapa ni kwamba kufanyike maamuzi magumu tu, hamna kukumbatia muungano usio kuwa na tija kwa watanganyika zaidi ya kunyonywa na wazanzibar wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…