Je, Rais Samia kutoa kauli ya "Mwanaume ni yule anayejiamini" ni kijembe Kwa Hayati Magufuli?

Mkuu wewe nikisoma mada zako ambazo hazina mlengo wa kisiasa huwa uko vizuri sana na wajua mambo mengi, lakini unapomzungumzia jiwe yani nikama wajizima data. Hivi unajua kweli ujinga aliofanya kwenye nchi hii??
Hakufanya ujinga, nadhani wewe ndiye unayesoma mada zangu kwa mlengo wa kisiasa zaidi kuliko kuangalia ukweli wake. Watu wengi waliowahi kuishi nje ya Tanzania wanaojua jinsi serikali za wenzetu zinavyoendesha mambo yao ambazo ndizo baadaye huwa zinatupatia "misaada" wanakubaliana nami kuwa jiwe alikuwa anayoosha nchi. Lazima serikali iwe principled, siyo mambo ya kufurahisha vikundi vya watu bila kuwa na mwelekeo wowote.
 
Shukrani sana Mkuu.
 
Ni fumbo kwa mtangulizi wake... maana yake ni kuwa yy anajiamini ndo maana karuhusu mikutano ya kisiasa ...kama asingekuwa anajiamini bc mikutano ingeendelea kupigwa pin

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hata mimi nimeshakaa nchi zaidi ya saba japo sijatoka nje ya hili bara letu, lakini kunyoosha watu kwa kuwaua siyo sahihi. Ndiyo maana mpaka Watanzania wakamwombea kifo na akafa kweli. Yes nchi kuwa principled kwa hili uko sahihi kabisa lakini isiwe kwa kuiba pesa za watu ama kuwaua raia
 
Yeye sio mwanaume kwa kauli hiyo kauli ni mfu kama aliitamka kumsafisha ila aliyemtangulia ndiye alikuwa mwanaume ndio maana anakiri kwa kuzunguka mbuyu " mwanaume ni yule anayejiamini" akifikiri na yeye ni mwanaume kumbe........................siasa mazingaombwe ya hadaa
 
Hakuna aliyewahi kutoa ushidi kuwa Magufuli aliuwa watu ili awachukue mali zao. Ni kwamba alibana watu wasitumie njia za mkato mkato kinyume cha sheria au kukwepa kodi. Hiyo ndiyo sababu ya watu waliozowea njia za mkatomkato kumchukia. Mwaka jana nimetumia muda mrefu sana Tabora, Mwanza na Dar sikuona kama watu wengi walikuwa wanamchukia kama inavyoandikwa hapa. In fact watu wengi sana walikuwa wanasikitioka kumkosa..
 
Wacha porojo zako na kumhusisha Mhe. Rais. Jadilini story zenu kwa kufikiri kabla ya kuandika. Mhe. Rais anawezaje kumpiga kijembe Hayati? Kutwa ni porojo tu mara hivi mara vilee. Why hukufikiria labda asiyejiamini ni mwanasiasa aliyekimbia nchini kwa woga wa madeni? πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Hawezi kupiga marehem vijembe labda useme machawa ndio mmepigwa nyundo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…