Je, Shekilango na Urafiki ndio Stendi mpya za Mabasi yaendayo mikoani?

Niliona zimbabwe kwenye stand yao harare abiria wa kwenye basi hasa wakati linatoka tulitoa dola moja na tukapewa vitiketi vidogo kila abiria aliekaa kwenye siti hapo achana na viingilio vya milangoni wakati unaingia roadport ambalo ndio jina la stand yao
 
Pale ni ofisini na pia hivi MTU anatoka Kongowe ya Mbagala kupanda bus Mbezi? Huna hata huruma
 
Aisee pale kuna ofisi ya newforce, shabiby, kidia 1, dar lux, kilimanjaro, n.k yapo mabas kibaooo
 
Tanzanite..Ally's sidhani kama yanaijua stendi ya magu

Nimepanda juzi tanzanite toka mbeya ilipita kushusha stendi ya mbezi.

Nilisafiri kwenda mwz na ally’s tulitoka shekilango tukaenda parade stendi ya mbezi
 
Kwani ukipanda bus kwenda mbezi si lazima uende hapo mbezi?

Mpaka wanaweka shekilango, manake kuna abiria wameshazoea kufika hapo. Na mabasi mengine yanapita njia ya Bagamoyo. Sasa stendi ya mbezi waende kufanya nini wakati wateja wao wanaweza kufika hapo?
 
Blaza magari yetu ya kusini stendi Mbagala...hao waache.
Ulienda Lupaso kusalimia Kilisimasi!!
 
1. Mabasi pale Urafiki yamepanga kwenye Kota za kiwanda cha Urafiki inamaana Serikali inapata mapato pia
2. Hili litasaidia Serikali kukusanya Data ya tabia za watu wake ni kitu gani hawapendi kwenye miradi ya maendeleo.
3. Wateja wanapenda Shekilango zaidi kuliko Mbezi.
4. Tupo kwenye Ubebari tuache kufikiri kijamaa less regulations ni kitu kizuri kwenye biashara.
5. Tupo 2022 Mteja now hataki shida that why Taxi inakufata nyumbani, unaletewa bidhaa nyumbani.
Tuwasaidie Wafanyabiashara wetu.
 
Hoja ya mtoa maada imejikita kwenye mapato yani anaamanisha hivi abiria wote wanaopanda basi kwa mfano wakiingia kupitia stand gate watalipia mia tatu kwa kila moja lakini wakija wakiwa kwenye bus hawatolipia badala bus ndo litalipa kiasi cha fedha ambacho ni pungufu ya kila ambacho wangelipa mtu moja moja pale gatini , hoja nyingine ya wadau humu ni umbali kwa kweli nikubaliane nao tu kuwa kuiweke stand nje mji iikuwa ni maumivu mengine kwa wasafiri wanaotoka pemebzoni mwa mji abiria anatola mashariki anilifuata basi magharibi kwakweli ni usumbufu bora serikali ingefanya namna stand ikakaa katikati ya jiji ili.kutoa fursa kwa abaria wote wanaotoka pembezoni kufika kwa urahisi .

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Wenye mabasi hawana uhuru wa kupita au kutopita stendi ya Mbezi
Ni lazima upite ili
1.Ukaguliwe
2.Utoe ushuru

Usipopita unapigwa fine.
Labda utuambie ni gari gani inatoka shekilango na haipiti stedi ya Mbezi au inatoka mkoani na kupitiliza shekilango.

Nb;
Magari yakishatoka stendi (Mbezi)wana uhuru wa kwenda kwenye ofisi zao binafsi kwa shuhuli za service na utawala.



Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Acha ujinga!
 
Paragraph yako ya kwanza ule ulikuwa mradi wa watu kupiga pesa
 
Hoja ya mapato ni ya kipuuzi kwa sababu abiria wa mabasi ya masafa, ambayo ndio yenye ofisi huko Urafiki na Shekilango, hukata tiketi kabla ya safari, na hukatia kwenye ofisi za mabasi ambazo ziko huko Shekilango na hata kwenye stendi ya Magufuli. Kwa hiyo wanapoenda stendi ya Magufuli kwa ajili ya kupanda basi hawalipi pesa yote stendi!
 

Bro umewaza vizuri sana na nna wasiwasi utakua na akili mingi sana zznice obervation.
 
Halipiti standi kwa sababu hakuna abiria wake huko, kwa nini lipoteze muda.
 
hamna shida wanaolipanda watajua pa.kulipata

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Acha umbea na roho mbaya wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…